Nilitaka kushangaa usingejitokeza kwenye huu uzi haya mbona umeyasahu.
16. foleni za unga wa njano na magendo ya bidhaa. Hata ‘sigara kali’ achilia mbali ‘sports’ na SM, ziliuzwa kwa bei ya kuruka
17. Kabla ya mikokoteni kufikisha magunia mawili-matatu ya unga wa njano, au mchele mdundiko, au kitumbo uliotoka Japan, watu kwanza walipanga mawe au makorokoro yoyote yale kwa sababu ya jua kali la saa nane mchana.
18.Foleni zilikuwa za kusukumana kwani watu walikuwa wengi kuliko bidhaa. Ndiyo kusema, wengine walirudi nyumbani mikono mitupu baada ya jitihada za kusukumana ili kulifikia dirisha la duka kushindikana. Wengine walizirai kwenye foleni! Ugumu hasa ulikuwa katika kupata sukari au mchele uliokuja kwa nadra
19.Mara nyingi, mchele na sukari vilipatikana kwa magendo majumbani mwa watu. Walanguzi walikuwa wakitazama au kuangalia huku na kule kabla ya kukupimia kibaba cha sukari, na wakati mwingine vibaba vyenyewe vilikuwa “mkude”
20.Vibaba-mkude” ni vibaba vya kupunjia. Kwanza unalanguliwa lakini pili unapunjwa. Ilikuwa ukienda sokoni unatazamwa usoni. Kisha unaulizwa unataka nini. Kama ulitaka mchele, basi mtu alibonyea bonye uvunguni mwa kikazi chake cha biashara na kubenjua gunia lililofichwa vizuri.
21.Unapimiwa kibaba mkude bila wewe mwenyewe kuona. Kwa kuwa ulihitaji mchele, na umeupata baada ya kuhangaika sana, basi huulizi tena. Tangu hapo, unatakiwa uondoke haraka sana baada ya kupimiwa, usiweke kiwingu cha kuleta “manjagu” bure
22.Mteja alitakiwa awe ‘shapu’, hakuna kuzubaa-zubaa! Na mtu alipokwenda kwenye nyumba yenye mchele au sukari ya magendo, hakutakiwa kupitia mlango wa mbele, bali azunguuke uchochoroni na kupitia mlango wa nyuma. Ukitoa sauti kali kuuliza sukari au mchele, hupati! Hawakuuzii ng’o, unaambiwa hakuna
23.Mameneja wa RTC ndio walioshamirisha magendo kwani walikuwa wakiwatumia “watoto wa mjini” kutoa bidhaa kwa mlango wa nyuma kutoka kwenye magodaoni ya Shirika la Ugawaji
24Nyerere aliamini kuwa, kwa kutumia sekta ya Umma kuhodhi bidhaa labda alikuwa anashinda vita dhidi ya ubepari kumbe alijenga mazingira ya kuwatesa wananchi wake na kuwanufaisha Maafisa wabadhirifu
25. Kiwango cha ubadhirifu wa mali ya Umma kilikuwa ni kikubwa kinyume na madai ya baadhi ya watu kuwa wakati wa Nyerere hakukuwa na ufisadi na ubadhirifu!
Wengine wataongezea....