Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Kukusanya kodi wapi tufahamishe tupate darsa kidogo.

Ali Hassan Mwinyi alikuwa na kibarua kigumu cha kufufua uchumi uliokufa kabisa. Jambo la msingi lilikuwa ni kubadili fikra kutoka zile za Mwalimu zilizoididimiza nchi kiuchumi kuja zile za kufunguka kiuchumi.

Akina Kolimba na Malecela walifanya chini juu kuhakikisha kuwa Mwinyi anatekeleza fikra mpya, na kuachana na zile zilizoshindwa za Nyerere. Madai ya Mwalimu kwamba wanasiasa hao walikuwa wakimshauri vibaya Rais Mwinyi yalitokana na upinzani wao dhidi ya fikra zake.

Sasa ulikuwa ni wakati wa kufungua milango kukaribisha wawekezaji wa kiuchumi kutoka pande zote za dunia ukiwemo ulimwengu wa Magharibi.
 
viongozi wa hii nchi wapowapo tu. mambo tunayowasifia yametokea kingekewa na siyo by design. kuingia kwenye demokrasia na kubadili sera za uchumi ni kutokana na mashinikizo ya WB na IMF. hao ndiyo ditch designers, wakina Mwinyi ni ditch diggers tu, wafuata upepo. hatuna viongozi wenye maono. kidogo Nyerere alikuwa nayo.
 
Legacy?!? ni IPI?! Labda ya kuiporomosha nchi na Mkapa kuja kuiinua. Ni kama JK alivyoiangusha na sasa JPM anavyohaha kuiinua.
Alkua anaambiwa na WB na IMF Nate anatimiza so hapakuwa na ujuzi wala ubunifu kupigia mfano!! Ruhusu demokrasia- sawa! ruhusu soko huria-sawa! nk. nk. Kuhusu legacy may be that but for me there was nothing best in particular!
na amini kabisa kama mngevaa matairi ya magari miguuni na kujifunga kaniki na mawingu na waume zenu kuvaa zile nguo za kaki zisizo na kola na kupanga foleni kwenye duka moja (tu) la kijiji kununua mche moja wa sabuni, kipimo kimoja cha mafuta ya taa, kiberiti kimoja na kipakti kimoja cha chumvi (tena isiyo na iodine) wala msingeandika haya.
Huyo mzee namkumbuka kwa kutuondolea adha nyingi sana zikiwepo za upatikanaji wa bidhaa muhimu kabisa katika maisha ya kila siku ya binadamu.
 
Kukusanya kodi wapi tufahamishe tupate darsa kidogo.
...Hapa tukubaliane tu, Mzee wetu kwenye suala la kodi, hakujishughulisha kihivyo. Serikali ilifika wakati ikawa imekauka fedha, ila mtaani, imejaa tele.

...Kimsingi nakubaliana na hoja yako ya kufufua uchumi, ila, kodi ilipaswa kukusanywa kwa kiasi fulani.
 
kabla ya kuingia mzee ruxa bidhaa zilipatikana kwa tabu sana,nadhani ni baada ya mwinyi kukubaliana na mpango wa National economy Recovery programme ndo nchi iliianza kurecover,ikifuatiwa na ule mpango wa structual Adjustiment Programme,
kiufupi alifungua milango ya kidemocrasia na kuruhusu uchumi huria
 
Tulishaliona hilo siku nyingi
 
Wanaomlaumu Mwinyi kutokusanya Kodi, Ni Tax base gani iliyokuwepo baada ya Mwinyi kuingia Madarakani?, kulikuwa kuna viduka vya Wahindi tu.

Alichokifanya Mwinyi ni kuwawezesha wananchi wawe na kipato, ili wenye kuanzisha biashara waanze, Then unatoa Tax Incentive kwa kutowatoza kodi ili Biashara zikomae, then Ukishapata watu wa kutosha wa kuwatoza kodi Unaanza kuwatoza kodi.

Mkapa alipoingia Madarakani angalau aliwakuta watu wachache ambao ni Taxable, ambao walipata utajiri wao kipindi cha Mwinyi. Mzee Mwinyi hakuwa na Privilege hii, alikuta nchi hohehahe na wananchi hohehahe Angekusanya kodi kutoka kwa nani?
 
Mbatia na genge lake waliongoza harakati za kumchora mzee ruksa
 
angekusanyaje kodi wakati amekuta serikali haina hela na wananchi hawana hela? cha kwanza alichofanya Mwinyi kupitia kushauriwa na akina Prof. Lipumba ni kuwajaza mahela wananchi. katika miaka 10 aliwawezesha sana wananchi kujijenga kiuchumi na kila aliyeweza alipiga hatua kimaendeleo kadiri alivyojituma. Na ndipo alipokuja Mkapa na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji kodi kama vile TRA, VAT nk kwa sababu tayari wananchi walishawezeshwa kiuchumi. kwa hiyo Mwinyi asingeweza kukusanya kodi hasa pale mwanzoni mwa uongozi wake kwa sababu wananchi hawakuwa na kitu kabisa.
 
Alkua anaambiwa na WB na IMF Nate anatimiza so hapakuwa na ujuzi wala ubunifu kupigia mfano!! Ruhusu demokrasia- sawa! ruhusu soko huria-sawa! nk. nk. Kuhusu legacy may be that but for me there was nothing best in particular!
Mkuu nakubaliana nawe!! lakini wakati huo TZ ilikuwa inatoka ktk Comminiisum/inatoka ICU yaani mgonjwa bado yupo wodini..hivyo Dokta huumba miiko na matibabu kwa dawa chungu !!
DON'T BLAME THE PAST for TODAYS value !!!
 
sio kweli kuwa Mkapa alikuta watu wachache amabo ni taxable bali walikuwa wengi tu wa kutosha.
 
Anafanya vema sana kwenye afya yake (angalau kwa muonekano wa nje)! Namuona akigonga miaka 100 kirahisi kabisa akiwa bado anatembea bila msaada wowote! Analo la kutufunza ni kwa vipi ameweza kutunza afya yake kwa kiasi hicho (pamoja na kuwa bigamist?)
 
Alipokea kijiti cha uongozi wakati nchi ikiwa katika hali ngumu mno kiuchumi.

Sijui kama ulikuwepo kipindi hicho mkuu.

Kama ungekuwepo sijui kama ungeandika hayo uliandika labda kama unaleta ubishi na ushabiki sawa.
Legacy ingine ni kumuibua JK toka Masasi akiwa Katibu wa CCM Wilaya kumteua Naibu Waziri maana alishasahaulika kama si yale mafuriko ya Masasi na J S Warioba kumuombea msamaha..........
 
kipindi mwinyi anachukua nchi asilimia 90 ya mashirika yalikuwa ni ya umma na yalikuwa yanakufa,watu walikuwa wanamzunguka nyerere na kuyamaliza mashirika ya umma kwahiyo ukusanyaji kodi usingekuwa mkubwa kama wa awamu zilizofuata,
watu mitaani walikuwa na pesa kwani hicho kipindi ndo biashara huria zimeanza na private sector ndo imeanza kukua,na katika kipindi cha mwinyi sijawahi kusikia kuadimika kwa bidhaa iwe sukari ama sabuni.
Kama alivyosema mdau,kipindi hiki bidhaa zilianza kutafuta wateja badala ya wateja kutafuta watu,kwa logic hiyo lazima watu wangekuwa na pesa mifukoni,sioni tatizo la wananchi kuwa na fedha mifukoni,kama suala la kukusanya kodi waliofuata walianza kuweka system ya kukusanya kodi baada ya mwinyi kuweka msingi wa watu kufanya biashara na kupata pesa za kulipa hiyo kodi
 
sio kweli kuwa Mkapa alikuta watu wachache amabo ni taxable bali walikuwa wengi tu wa kutosha.
kipindi cha mkapa sawa walikuwa wameshaanza kukomaa kulipa kodi,kipindi cha mwinyi hao kina barheresa walikuwa bado ndo wanaanza kumiliki mashine za kawaida tu za kusaga nafaka,
mashirika kama Bora,voil,etc yalikuwa yanamalizikia kukata roho hayangeweza kulipa kodi
 
Mzee wa gemu ana legacy zenye positive na negative faces
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…