Muda mfupi tu baada ya Mwinyi kuingia madarakani na kubadili mtazamo wetu wa kiuchumi, mambo yakaanza kubadilika kiasi cha kuwashangaza watu. Magenge ya ulanguzi yakatoweka baada ya bidhaa kupatikana kwa wingi.
Watanzania wakaanza kufanya biashara na nchi nyingine, waliokwenda Kenya kupeleka machungwa, na wao kurudi na sabani za kufulia na kuogea, waliokwenda Uganda, waliokwenda Uarabuni, Ulaya, Marekani, alimuradi kila mmoja alikwenda alikotaka.
Soko la bidhaa mbalimbali likashamiri. Badala ya watu kutafuta bidhaa, bidhaa zikatafuta watu. Nguo mpya za dukani bwerere, mitumba bwerere, sabuni kibao, fegi hahahah teletele, magari makubwa na madogo kibao, Televisheni kibao, Radio kibao.