Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Mwinyi alikuwa tofauti kabisa na Nyerere. Mwalimu alikuwa kwa kiasi fulani very simple, aliishi maisha rahisi sana.
Nakumbuka enzi zile za awamu ya kwanza, kulikuwa na nyumba fulani ambayo ilikuwa pale mbele ya ile ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, kama unaelekea wizara ya fedha.
Mwenye ile nyumba alikuwa anafuga mbuzi zaidi ya mia moja, halafu anawaachia asubuhi watembee kutafuta majani, basi wakawa wanapenda kula zile nyasi zilizo pembeni ya Ikulu, wakati wakielekea maeneo ya ocean road.
Halafu jioni wanarudishwa nyumbani. Sisi tuliona poa tu kwa sababu ya akili za kitoto, lakini yale yalikuwa ni mambo yanayofanyika jirani kabisa ya Ikulu!. Na hakuna mtu aliyeonyesha kujali, very simple life enzi za Mwalimu Nyerere.