Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

U
Foleni zilikuwa za kusukumana kwani watu walikuwa wengi kuliko bidhaa. Ndiyo kusema, wengine walirudi nyumbani mikono mitupu baada ya jitihada za kusukumana ili kulifikia dirisha la duka kushindikana. Wengine walizirai kwenye foleni! Ugumu hasa ulikuwa katika kupata sukari au mchele uliokuja kwa nadra.

Teh teh teh
l
Mkuu foleni ya mkate wa siha, ambao ulikuwa unatengenezwa na national milling, kiwanda tulichotengenezewa na Canada(bakery). Tulikuwa tunanunua tshirt za mikono mifupi ukifua mara mbili imeshakua ya mikono mirefu.
Hall 3, wakati ule bweni la wasichana aka serengeti(UDSM) tulikuwa tunaopoa kwa sabuni ya lux au imperial kutoka kenya.
Jamani tuna historia, chonde chonde tusirudi tena huko.
 
Unatukumbusha mbali sana tena sana, watu tumetoka mbali, Mzee Mwinyi ndie aliyefanya watanzania wengi wajue kama tv. Nchi kabla yake iliongozwa kidikteta hakuna aliyethubutu kusema lolote baya kwa Mwalimu.

Na bado wengi hawajui kazi aliyoifanya
 
Pia enzi hizo za kulikuwa na maduka ya kaya.

Unga wa sembe wa njano.

Ukimuona mtu amevaa raba nzuri(raba mtoni) ujue ana ndugu ulaya au bahari.
Mtaani kwetu kulikuwa nyumba moja tu ina TV kwa dr Mhando.

Dah!!! Hata kandambili ilikuwa shida.
Tumevaa sana katambuga za matairi ya gari.

Yale maisha yalikuwa si mchezo.

Miaka hiyo sisi tulikuwa na friji peke yetu mtaani
mtaa mzima mtu akitaka maji baridi anakuja kuomba kwetu...haha haaa
kweli Nyerere alijua kuwanyoosha watz
na bado wanamuita mtakatifu na Mwinyi ndo walimtukana
 
Mkubali msikubali siyo wewe tu,bali na mwenzako Fayza Fox na The big show, nyerere ndio atabakia kwa ni kielelezo cha viongozi walio wahi kuwa bora kabisa hapa tanzania

Sukari kilo moja kaya moja kwa wiki.
 
1978 hadi 1979 mbona hujauliza madhara ya hivyo vita kiuchumi kwa nchi masikini kama tanzania kipindi hicho viliiathiri vipi?

Dhiki na umasikini wa kutupwa Tanzania ulianza mwaka 1967 mara tu baada ya kutangazwa azimio la Arusha. Kumbuka hilo.
 
Baba aliniambia kipindi cha Mwinyi walikua wanaenda kutembea mitaani wakiangalia chini ili waokote pesa iliyodondoshwa na watu, kweli pesa ulikua nyingi kipindi hicho
 
Mzee Mwinyi alikuwa na roho nzuri n I won't try throw a f*ck to him.

He was a good man.

Ila Awamu yake aliyekuwa anatawala bado alikuwa ni Nyerere.
 
Dhiki na umasikini wa kutupwa Tanzania ulianza mwaka 1967 mara tu baada ya kutangazwa azimio la Arusha. Kumbuka hilo.
Hivi ni kwanini yule kijana wa kiislam alimzaba Mzee Mwinyi Kibao?

Miaka hiyo sisi tulikuwa na friji peke yetu mtaani
mtaa mzima mtu akitaka maji baridi anakuja kuomba kwetu...haha haaa
kweli Nyerere alijua kuwanyoosha watz
na bado wanamuita mtakatifu na Mwinyi ndo walimtukana
 
Mzee Mwinyi alikuwa na roho nzuri n I won't try throw a f*ck to him.

He was a good man.

Ila Awamu yake aliyekuwa anatawala bado alikuwa ni Nyerere.
Awamu yake kuanzia 91 alikuwa tofauti sana na mzee wa "Booty Hammer", na ndio maana Mchonga alikuwa akimpiga vijembe kama alivyosema "anaongozwa na mkewe".
 
Wanaomlaumu Mwinyi kutokusanya Kodi, Ni Tax base gani iliyokuwepo baada ya Mwinyi kuingia Madarakani?, kulikuwa kuna viduka vya Wahindi tu.

Alichokifanya Mwinyi ni kuwawezesha wananchi wawe na kipato, ili wenye kuanzisha biashara waanze, Then unatoa Tax Incentive kwa kutowatoza kodi ili Biashara zikomae, then Ukishapata watu wa kutosha wa kuwatoza kodi Unaanza kuwatoza kodi.

Mkapa alipoingia Madarakani angalau aliwakuta watu wachache ambao ni Taxable, ambao walipata utajiri wao kipindi cha Mwinyi. Mzee Mwinyi hakuwa na Privilege hii, alikuta nchi hohehahe na wananchi hohehahe Angekusanya kodi kutoka kwa nani?
Uko sawa kabisa
 
Nashukuru nimemjua Mwinyi kupitia Uzi huu, ila ni kwanini media zimemtenga, hatupati hata hotuba zake?
 
ritz,
usishangae watz ni watu wa ajabu sana. hawapendi kuambiwa ukweli na wanaweza muwekea chuki mtu bila sababu. hawajui mtumba ulikuwa unapita hapo bandarini dar unakwenda burundi halafu unarudi uapo kwa magendo tunakimbizana na jkt kwa kuuza mashati ya mpira na mtu atalivaa mpk litabaki wavu mgongoni tumetoka mbali acheni jamani!!!!!!!!!!!!!!!!
 
ritz,
usipate shida, watz ni watu wa ajabu sana. wanaweza kukuchukia kwa chuki binafsi, na kukunyima heshma na sifa yako kwa sababu anakuchukia tuu. wengi wao hawafahamu mitumba ilikuwa inapita hapo bandarini dar, kwenda burundi halafu tunaifuata kuileta hapo kwa magendo kutoka banda tunakimbizana na jkt mitaani kwa kuuza shati za mpira mtu anavaa mpk unabaki wavu mgongoni. tumetoka mbali!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
bw. mdogo mbona hushangai mzee sepetu na mzee adam wote asili yao ni mbeya lkn ni watumishi wa serikali ya zanzibar? ukisoma hata historia darasa la nne utajua. hata waziri mkuu wa kwanza baada ya uhuru wa zanzibar mzee shamte alikuwa mndengereko hebu chekecha mbori kidogo!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom