Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Mzee mwinyi ni mtu muungwana sana na huwa katu hawezi jikweza ndo maaana kila mara huwa anasifia mwingine na sie yeye.

Hata alipoulizwa kuhusu mwalimu nyerere alisema "ukijaribu kunilinganisha mimi na mwalimu basi mimi ni kichuguu yeye ni mlima kilimanjaro"

Alhaj mwinyi muungwana sana bwana yule...!!


Duh, Mzee Mwinyi kwa heshima na taadhima, alichosema siyo sahahi, yaani Urais wake plus wa Mkapa plus wa Kikwete unazidiwa na miaka 3 ya Magufuli?
Mzee Mwinyi angejisemea nafsi yake tu lakini kauli yake inaharibu legacy za wenzie
Ina maana madaraja yote makubwa, plus mabarabara, mavyuo vikuu, mavivuko, mashule ya kata, Umeme Kinyerezi 1, Bomba la gesi, uwanja wa ndege terminal III, mwendokasi aliyojenga Kikwete plus uchumi mzuri aliouacha Mkapa vyote hivyo Magufuli kavizidi ndani ya miaka 3?
 
Personal assement yangu kwa maoni yangu serikali zilizopita kabla ya Magufuli Kuanzia Raisi Nyerere .Nyerere alikuwa Yuko vizuri mno kwenye matumizi ya pesa za serikali kama alivyo Magufuli Lakini wote wawili Nyerere na Magufuli Sio wazuri kwenye Uwezo wa ku encourage na KU groom vyanzo vya mapato sustainable .Maraisi waliobaki Kuanzia Mwinyi,Mkapa,na Kikwete walikuwa wazuri mno kwenye strategy za mapato Lakini kwenye matumizi usimamizi ulikuwa mbovu.Nyerere alikuwa mzuri mno kuhakikisha Pato la nchi linanufaisha mwananchi mlalahoi kwa elimu bure ,afya bure ,ajira nk Lakini strategy za kuingiza mapato sustainable hakuwa vizuri matajiri aliwaona Kama SI rafiki na sekta binafsi kwake aliona Kama wezi tu baadaye biashara zikafa kibao akashindwa kupata pesa za Kodi za kuhudumia walala hoi .Raisi Maguli Yuko vizuri mno kwenye matumizi lakini kwenye issue ya strategy ya sustainable income generatinon hayuko vizuri kabisa.Kwenye hili ni photocopy ya Nyerere ambaye alikuwa mtumiaji mzuri sana wa pesa kuhakikisha zinawafaidisha wanyonge Lakini kwenye kuzalisha pesa sustainable na KU encourage private business sector na kuiwekea mazingira rafiki Sana hayuko vizuri .Yeye na Nyerere wanafanana.Hao Maraisi waliobaki tatizo kubwa walilokuwa nalo ni kwenye matumizi kwenye strategy ya mapato walikuwa vizuri strategy za matumizi hawakuwa vizuri na hawakusimamia vizuri.Raisi Magufuli Yuko vizuri matumizi stigler gorge,SgR ,barabara ,zahanati nk matumizi Yuko vizuri issue Ni sustainability ya mapato na income strategy eneo hili hayuko vizuri kabisa

Nakuona siku hizi unaleta vitu vinavyo make sense na siyo ushabiki uchwara kama zamani. Hongera mkuu japo sijui umepatwa na nini.
 
Nchi ilikuwa na haki mbaya hili jamani acha!Vijijini watu walikua wanavaa magunia na mifuko ya simenti,,,kunguni na chawa vilikua sehemu ya mwili wa mwanadamu,,,Mwinyi aliistaarabisha nchi hii sema watu wamesahau tu
Duh!.
 
KIkubwa alichofeli ni KUKUSANYA KODI na ndipo ilimbidi Mkapa alipoingia aanzishe TRA.

RUKSA RUKSA ilikuwa RUKSA kwlei kweli watu walikuwa wanahela mbaya na vitu vilipatikana kwelikweli.( Mfano w ahili ni show ya Kanda Bongo Man ndani ya Kilimanjaro Hotel Miaka hiyo ya 90 kiingilio ilikuwa 100,000/= na bado ilijaza)

Nyerere alimpiga dongo sana kuwa anashahuriwa na Mkewe au tuseme wake zake.
Sasa ulitaka akusanye kodi kwa washindia KAMANYOLA moja tena ni kauka nikuvae?.
 
Na ukizingatia serekali ndo ilikuwa inafanya biashara kuanzia uzalishaji usambazaji hata uuzaji rejareja, kodi alilipa mtumishi wa serekali tu. Nyuma kdg kila raia alitakiwa kulipa kodi ya maendeleo (ya kichwa)
Wazee wetu walikuwa wanaondoka majumbani mwao saa 10 alfajiri kwenda kujificha kwa sababu ya kukosa hiyo kodi ya kichwa.
 
Kwweli mbweha ni mbweha hata akivaa kanzu. Wewe watu wanalia na ufisadi uliokithiri kumbe wewe kwa ko ndiyo marekebisho?

Ndiyo maana mmerundikana kwenye wakwepa kodi, watorosha makontena bandarini na waingiza malori kibao kwa jina la kusalia. Mmezowea vya kunyonga. Sasa tumewashtukia na hatuwapi nchi tena!

Watu wanahangika makisha magumu, wizi kila mahala huduma muhimu hakuna, nini wacheza bao mnahujumu uchumi halafu bila haya hata huoni unasifia hadharani!. Tumewatambua... Tanzanai si ya mafisadi na wapenda hujuma.

Sasa utasubiri sana mtu wa kutuharibia nchi kwa manufaa ya wacheza bao, hutampata tena!!!!! nakuambia.
[emoji12][emoji23][emoji1787]
 
Nilishauri mwanzo kabisa vijana wa miaka ya 90 wangekuwa wasomaji wangejifunza mengi kwenye huu uzi.

Hamna mtu anayemfananisha Nyerere na Mwinyi kila mtu katawala kivyake.

Unasema Nyerere alijaribu kuiweka nchi kwenye mstari vikaibuka vita vya Uganda siyo?

Nyerere kachukuwa nchi mwaka 1960 vita vya Uganda vimetokea mwaka 1978.

Hiyo miaka 18 alikuwa anafanyaje kwenye utawala wake?
Duh!.
 
Inawezekana ulipatikana baada ya babako kunywa pombe za kienyeji. Vinywaji vya kienyeji vinaendelea kukulevya mpaka leo.

Angalia kwenye list ya mafisadi watu gani waliopelekwa kwa wingi mahakamani?

Mtake msitake, Mungu akitaka mtaachia tu. Vibakwa wakubwa nyie
Mama Samia tayari.Mungu apangiwi.
 
1. ALIFUATA TORATI YA MUSA NA KUWANYONGA WOTE WALIOHUKUMIWA KIFO NA MAHAKAMA KWA MUJIBU WA SHERIA ZA TANZANIA BILA MZAHA WALA UPENDELEO AKIWEMO KANALI MMOJA TOKA TABORA NAMPENDA SANA KWA HILO
2. ALIWABEBA SANA WAFANYABIASHARA KIASI KWAMBA AJIRA IKAONEKANA NI UPUUZI NA WENGI WALIACHA KAZI SERIKALINI KWAKUWA MISHAHARA ILIKUWA HAIPATIKANI MPAKA WAFANYABIASHARA WAPELEKE FEDHA BANK NDIPO MFANYAKAZI APATE MSHAHARA NI KATIKA KIPINDI CHAKE ALINISABABISHIA NIACHA KUSOMA BAADA YA KUONA KUAJIRIWA HAKULIPI KAMA KUFANYA BIASHARA
3. ALIMDEKEZA SANA WAZIRI WA FEDHA MAREHEMU PROF. KIGHOMA ALI MALIMA AKAJENGA MSIKITI WIZARA YA FEDHA.
4. NI KATIKA KIPINDI WAISLAM WALITAKA TANZANIA IONGOZWE KIDINI NA MKAKATI HUO ULIONGOZWA NA MAREHEMU SHEIKH YAHYA HUSSEIN KWA KUANZISHA BALKUTA NA KUANZA KUVUNJA MABUCHA YA NGURUWE NA NI KIPINDI HICHO NYAMA YA NGURUWE ILIITWA KWA UTANI "YAHYA" AU MBUZI KATOLIKI
5. NI KATIKA UTAWALA WA MWINYI SERIKALI ILIKUWA HAIKUSANYI KODI NA WAFANYABIASHARA WALIKUWA NA NGUVU YA KUFANYA LOLOTE NA IKULU PALIKUWA PANAINGILIKA KIRAHISI SANA HATA UKIWA NA SHIDA YA ADA YA SHULE ULIRUHUSIWA KUMUONA RAIS NA UKIHITAJI KUCHEZA BAO NA PRESIDAA UNAOMBA NA UNAINGIA KAMA ALIVYOFANYA MWENYEKITI WA YANGA NA MBUNGE WA KILOMBERO MAREHEMU ABBAS GULAMALI. NAISHIA HAPO.
Huyu kweli alikuwa kiongo wa watu.
 
Mimi kama mfanyakazi nitakuwa wa mwisho kumpongeza Rais Mwinyi maana katika utawala wake ndo kipindi wafanyakazi walidharauliwa hata na wauza machungwa barabarani, kilikuwa kipindi kigumu sana kwa kundi la wafanyakazi wa umma. Bila Rais Mkapa kubadilisha mambo sijui nchi hii kama ingekuwepo hadi leo. Maana ni kipimdi ambacho serikali ilikuwa dhaifu sana haikuweza kabisa kukusanya kodi nakumbuka hadi Nyerere alisema serikali dhaifu huwa zinaacha kukusanya kodi kwa wafanya biashara na kufukuzana na machinga barabarani. Sasa Kiongozi aliyeomgoza serikali dhaifu kiasi kile labda akumbukwe kwa hiyo sifa ya kuwa na serikali dhaifu sana.
Wafanya kazi wa nchi kipindi hicho walikuwa asimilia ngapi ya watz wote?.
 
Wengine wazazi wetu walifungwa kwa kudhaniwa kuhujumu uchumi eti wamekutwa na vyakula kutoka nje ya nchi!

Mimi Babu yangu aliwekwa ndani kwa kesi ya uhujumu uchumi wakati wa Utawala wa awamu ya kwanza kwa kua alijaribu kufanya biashara.
Watawala wengine walikua ni watu wa ovyo sana
 
angekusanyaje kodi wakati amekuta serikali haina hela na wananchi hawana hela? cha kwanza alichofanya Mwinyi kupitia kushauriwa na akina Prof. Lipumba ni kuwajaza mahela wananchi. katika miaka 10 aliwawezesha sana wananchi kujijenga kiuchumi na kila aliyeweza alipiga hatua kimaendeleo kadiri alivyojituma. Na ndipo alipokuja Mkapa na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji kodi kama vile TRA, VAT nk kwa sababu tayari wananchi walishawezeshwa kiuchumi. kwa hiyo Mwinyi asingeweza kukusanya kodi hasa pale mwanzoni mwa uongozi wake kwa sababu wananchi hawakuwa na kitu kabisa.
Sawa mkuu
Niko hapa napitia madini yenu
Mliyotema
 
Viwanda vyote havikudumu kwa sababu ya kukosa tija.

Ni kweli viwanda kama Mwatex, Mutex vilikuwepo mwisho wa mwezi wafanyakazi badala ya kupewa mishahara wanapewa carton za kanga na vitege wakauze ili wapate pesa soko hamna wananchi hawana vipato.

Mipaka ilifungwa kisiasa na kuzuia bidhaa za nje. Sekta ya Umma aliyotumia Nyerere kuzalisha bidhaa ilifeli vibaya hamna wa kumuuzia.
Sawa mkuu
 
Mimi ninayokumbuka wakati wa Mwinyi ni haya;
  1. Rukhsa, nchi kugeuzwa kokoro
  2. Kaburi la Azimio la Arusha
  3. Kupotea kwa tausi viwanja vya Ikulu na Karimjee
  4. Kushuka kwa hadhi ya Ikulu
  5. First Lady kuitwa shemeji
  6. Kuzuka kwa mihadhara ya kidini
  7. Mgogoro wa Loliondo na Waarabu
  8. Mwanzo wa biashara ya Wanyama
  9. Ukwepaji wa kodi kushika kasi
  10. Mwanzo wa kuingia mikataba mibovu
  11. Kuzaliwa kwa IPTL, hadi leo inatutafuna.
  12. Kutothaminiwa kwa wasomi na wataalamu
  13. CCM kutekwa na wafanyabiashara na walanguzi.
  14. Kampuni za mfukoni na utapeli kushika kasi
  15. Nchi kuendeshwa kwa mtindo wa yupo yupo
Mengine nawaachia...
[emoji107]
 
Wewe unapaswa kuelewa hakuna Nchi ya Ujamaa na kujitegemea iliyoshindwa hata kusambaza Unga wa ugali kwa raia wake (tena sio bure) isipokuwa Tanzania ya Nyerere tukawa tukihoji tunadanganywa Oscar Kambona kakimbia na hela zote za Serikali kakimbilia kwa Makabaila na Mabeberu Uingereza
[emoji16]
 
Back
Top Bottom