Nahisi huruma sana jinsi hii kitu inayolazimishwa legacy ya Magufuli kwa sababu, kwanza ni nature ya Mwanamke kuwa na Huruma, pili asili ya mtu na makuzi yake.
Ninapojaribu kuwaza jinsi ambavyo itakuwa ngumu kuenzi mambo ya Mtangulizi wa Samia! Ni kwa hulka za hawa wawili kutofautiana sana. Hivyo watanzania watakuwa ama wakumbuke kuendelea kunzi ukatili katikati ya mtu mwenye huruma, au waenzi ukatili ulio kinyume na mtawala wa sasa ambae kwa hulka ya asili yake na makuzi yake sio mtu KATILI. Ukijaribu kurejea hotuba za mwanzo kabisa za Samia unakutana na maneno 'sitaki fedha ya dhulma'.
Viongozi tuwe kitu kimoja, fungueni vyombo vya habari, na mengine mfano wa hayo utajua kwamba hii kitu inayohimizwa sana na kambi ya D7 (legacy) itakuwa ngumu kudumu kwa sababu Magu atakumbukwa sana kwa ukatili kuliko mambo mengine kwa sababu ya aina MRITHI wake.
Hivyo kambi D7 tuwe wavumilivu
Legacy sio maneno ni vitendo.
Atakumbukwa kwa watoto walioende shule zaidi ya milioni kumi, hospitali zahanati, vituo vya afya, nidhamu serikalini, utendaji wa ukweli, barabara nchi nzima, umeme, maji wa uhakika, alithibiti mfumuko wa bei, alijali wakulima, bei za pembejeo, Masoko ya madini nchi nzima.
Alibana Acacia na makampuni yote makubwa duniani kutuibia rasilimiali zetu, madini yetu, tumepata mikataba mipya itayotunaifaisha wewe, vizazi vya sasa na vijavyo.
Zaidi atakubukwa kwa kuongea kwa uwazi, sisi ni nchi tajiri sana, tutembee vifua mbele, tujiamini, tushirikiane, tumtangulize Mungu.
Alijaribu kubadilisha mindset (uwezo wa kufikiri, kutafakari, kujitambua, utajiri wetu) ya Watanzania.
Alifungua upeo wa wengi kufikiri. Sababu yeye mwenyewe alitokea, alizaliwa kwenye familia maskini, kwahiyo alijua matatizo ya Watanzania wengi.
Of course kuna vitu alikosea, lakini legacy yake itadumu milele, haifutiki.
Mtoto wa maskini akienda shule hii ni moja ya legacy yake. Ukiweza kusafiri kutoka popote kwenye barabara za lami kutoka Mtwara, Bukoba hadi Dar hiyo ni legacy yake kufanya shughuli, biashara zako hiyo ni legacy yake.
Unafuta vipi legacy ukisafiri, barabara unazopita zimesimamiwa na yeye, ukiumwa unatibiwa bure, watoto wako shule wanaenda bure. Legacy yake haifutiki.