Legal documents na uchambuzi wa masuala ya kisheria hapa

Legal documents na uchambuzi wa masuala ya kisheria hapa

Naombeni sana sana mwenye document, kitabu ama chochote kile kielezeacho TANZANIA CONSTITUENT ASSEMBLY.
 
Hapa tutakuwa tunatoa documents (nyaraka) mbalimbali za kisheria ambazo mtu atahitaji kama vile case laws, hasa ambazo ni unreported, legislations, law books n.k.

Binafsi nina e-library kubwa sana ya hivi vitu na sitokuwa mchoyo kwa lolote, isipokuwa kuna baadhi ya vitabu vina kopyright so sitoweka hapa kwenye public itabidi nikutumie kwa email adress au vinginevyo.

Pia mjadala wowote wa kisheria (kwa wanasheria tu) ni vizuri ukawekwa hapa ili tuwekane sawa.

Wanasheria karibuni sana
Bwana Dragon,
Kuna mvulana alimpa mchumba wake figo, sasa wamekorofishana anadai arudishiwe figo yake. Imekaaje kisheria
 
Bwana Dragon, naomba unisaidie kesi hii tafadhali. Ni unreported. Civil Appeal No.67/01 – James Gwagilo vs A.G. CAT at Dar.
 
Mkuu naomba kitabu kinachohusu legislative drafting

Na Black's law dictionary
Mkuu McNair tafadhali ni PM email yako nikupe Black's Law Dictionary.
Vitabu vinavyohusu Legislative Drafting tayari vipo humu, angalia post zilizopita. Hata hivyo ongezea na hivi hapa chini.
Furahia.
 
Attachments

Attachments

Bwana Dragon,
Kuna mvulana alimpa mchumba wake figo, sasa wamekorofishana anadai arudishiwe figo yake. Imekaaje kisheria
Mkuu Retired kwa sheria za Tanzania hilo halitawezekana. Mahusiano ya uchumba hayaendi mpaka kwenye biashara au tuseme utakatishaji wa viungo vya binadamu. Kwa tanzania kuuza kumpa mtu kiungo chako ipo kwa sababu za kiafya tu. Sasa huyo mvulana anapodai arudishiwe figo yake anakuwa hana LEGAL JUSTIFICATION sababu hakuna mkataba wowote kama huo unaoruhusuwa Tanzania. Kifungu cha 23 cha sheria za mikataba Tanzania, sura ya 345 kinakataza makubaliano kama haya, ambayo yako kinyume na sheria.
kwa hiyo huyo mvulana kwa hapa Tanzania hatoweza kulazimisha arudishiwe figo yake kwa namna yoyote ile na akaonekana ana haki.
 
Bwana Dragon, naomba unisaidie kesi hii tafadhali. Ni unreported. Civil Appeal No.67/01 – James Gwagilo vs A.G. CAT at Dar.
Mkuu Retired hii kesi ipo reported. Itafute kwenye Tanzania Law report ya mwaka 2004 ukurasa wa 161. ([TRL] 2004 161).
 
Mkuu Retired kwa sheria za Tanzania hilo halitawezekana. Mahusiano ya uchumba hayaendi mpaka kwenye biashara au tuseme utakatishaji wa viungo vya binadamu. Kwa tanzania kuuza kumpa mtu kiungo chako ipo kwa sababu za kiafya tu. Sasa huyo mvulana anapodai arudishiwe figo yake anakuwa hana LEGAL JUSTIFICATION sababu hakuna mkataba wowote kama huo unaoruhusuwa Tanzania. Kifungu cha 23 cha sheria za mikataba Tanzania, sura ya 345 kinakataza makubaliano kama haya, ambayo yako kinyume na sheria.
kwa hiyo huyo mvulana kwa hapa Tanzania hatoweza kulazimisha arudishiwe figo yake kwa namna yoyote ile na akaonekana ana haki.
asante sana. kijana anamtishia . Tumepata pa kuanzia. thanks a lot1
 
Mkuu Retired hii kesi ipo reported. Itafute kwenye Tanzania Law report ya mwaka 2004 ukurasa wa 161. ([TRL] 2004 161).
Hapa TLR ipo maana najaribu kuangallia docs ulizotusaidia sijaona. Ngoja nitafute zaidi. UBARIKIWE SANA. NI WACHACHE WAKO KAMA WEWE
 
Hapa TLR ipo maana najaribu kuangallia docs ulizotusaidia sijaona. Ngoja nitafute zaidi. UBARIKIWE SANA. NI WACHACHE WAKO KAMA WEWE
Mkuu ya mwaka 2004 humu haipo. ninayo kwenye files zangu. humu haikubali ku upload sababu ni kubwa na humu JF wanataka file lisizidi MB 25. Ukinipatia email adress yako naweza kukutumia mkuu
 
Hapa tutakuwa tunatoa documents (nyaraka) mbalimbali za kisheria ambazo mtu atahitaji kama vile case laws, hasa ambazo ni unreported, legislations, law books n.k.

Binafsi nina e-library kubwa sana ya hivi vitu na sitokuwa mchoyo kwa lolote, isipokuwa kuna baadhi ya vitabu vina kopyright so sitoweka hapa kwenye public itabidi nikutumie kwa email adress au vinginevyo.

Pia mjadala wowote wa kisheria (kwa wanasheria tu) ni vizuri ukawekwa hapa ili tuwekane sawa.

Wanasheria karibuni sana
Dragon, kuna hiki kitu:
Kanuni za bunge zinampa Ndugai madaraka makubwa. Kanuni hizi zisipobadirishwa zitaleta maafa makubwa kwa nchi hii. Bunge halina maana tena. Bahati mbaya Ndugai hana busara za kutumia madaraka hayo makubwa bila ku- corrupt! Power corrupts; absolute power corrupts absolutely. Ni sawa na madaraka ya Rais, ni makubwa mno! But thank God the arbitrary acts of the President can be challenged by judicial review!
Nyerere aliweza kuishi na absolute power but he did not corrupt! Busara kama hizi za Nyerere ni za pekee, si watawala hawa wa sasa. Siyo kizazi hiki.
MY QUESTION: Can the arbitrary actions of the SPEAKER from his absolute power be subjected to judicial review?
 
Mkuu Retired naweza kukujibu kama ifuatavyo:

Can the arbitrary actions of the SPEAKER from his absolute power be subjected to judicial review?

Kiongozi,

Swali lako nitalijibu kwa Kiswahili, na inapobidi nitachanganya na kingereza. Katika kujibu swali lako nitajikita zaidi katika kadhia iliyotokea hivi karibuni bungeni, yaani ya John Mnyika kufukuzwa bungeni na kusimamishwa kuhudhuria baadhi ya vikao vya bunge la Jamhuri wa Muungano. Pia nitajikita kwa yaliyowakuta wabunge Halima Mdee na Esther Bulaya. Hii ni kwa sababu swali lako halijaweka nadharia maalum (specific).

Kiongozi na ndugu Wana JF wote,

Spika wa bunge la JMT kapewa mamlaka na Katiba ya JMT, na mamlaka hayo kupanuliwa au/na kufafanuliwa zaidi na Kanuni za Kudumu za Bunge (Kanuni). Mamlaka hayo yanalindwa pia na Katiba na Kanuni. Spika wa Bunge la JMT anayo mamlaka katika bunge ambalo yeye ndiye kiongozi wake, ambayo yamegawanyika katika sehemu maalum mbili, Mamlaka ya lazima na mamlaka ya hiyari (mandatory and discretionary powers).

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni dola yenye mihimili mitatu, utawala, bunge ma mahakama. Mamlaka ya mhimili wa mahakama, pamoja ma mambo mengine, ni kupitia maamuzi ya mihilili migine katika utendaji haki, ikiwemo mahakama yenyewe. Hii ndiyo inaitwa Judicial Review. Judicial review hufanyika ili kujiridhisha kama haki imetendeka katika utekelezaji wa majukumu ya chombo cha dola yaliyotolewa au yaliyopo kisheria.

Katika kutoa maamuzi yake katika suala hili la judicial review lazima mahakama ijiridhishe na uwepo wa mambo yafuatayo:

1. Uamuzi umetolewa na mamlaka ya dola (Public authority).

2. Mamlaka ya dola ilitoa uamuzi huo katika kutekeleza majukumu yake iliyopewa kisheria.

3. Hakuna namna nyingine ambayo mlalamikaji angeweza kufanya zaidi ya kuomba judicial review.

4. Kinacholalamikiwa kufanyika au kutofanyika kiwe ni cha lazima (mandatory) kufanywa au kutofanywa, kisiwa cha hiari (discretional).

5.

Kama nilivyoeleza hapo juu, spika wa bunge anatekeleza majukumu yake kwa mamlaka aliyopewa kisheria. Kanuni za kudumu za bunge (2016), kanuni ya 67 (1) na (2) zinampa mamlaka spika kukataza majadiliano na anaweza kumkataza mbunge yeyote kuzungumza. Kanuni hizi zinasomeka hivi:

67.-(1) Spika anaweza kulihutubia Bunge wakati wowote na kwa

ajili hiyo, anaweza kumkatiza Mbunge yeyote anayezungumza.

(2) Endapo Spika atasimama wakati wa mjadala, na kuanza

kuzungumza, Mbunge yeyote ambaye atakuwa anazungumza

wakati huo au ambaye atakuwa amesimama mahali pake akisubiri

kuanza kuzungumza, ataketi mahali pake, na Bunge litabaki kimya

ili Spika aweze kutoa maelekezo au taarifa yake.

Kanuni ya 68 inatoa taratibu mbalimbali na taratibu mbalimbali. Kanuni za 68 (4) na (5) zinasomeka hivi:

4) Spika anaweza, ama papo hapo kutoa uamuzi wake juu

ya jambo la utaratibu lililotajwa au kuahirisha uamuzi ili alifikirie

zaidi jambo hilo na kutoa uamuzi baadaye au kutoa uamuzi na

baadaye kutoa sababu za uamuzi huo, vyovyote atakavyoamua.

(5) Katika kufikia uamuzi wake, Spika anaweza kuitaka Kamati

ya Kudumu ya Kanuni za Bunge au Kamati nyingine yoyote ya Bunge

impe ushauri kuhusu jambo husika.​

Mbali na hayo, spika amepewa majukumu na mamlaka ya kudhibiti fujo na kusimamia utaratibu bungeni. Kanuni namba 72 (1), (2) na (4) zinasomeka namna hii:

72.-(1) Spika atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa, utaratibu

bora unafuatwa Bungeni, na uamuzi wa Spika kuhusu jambo lolote

la utaratibu utakuwa ni wa mwisho.

(2) Mbunge atakayekiuka utaratibu uliowekwa na Kanuni

hizi anaweza papo hapo kutakiwa na Spika afuate utaratibu na

vilevile Mbunge mwingine yeyote anaweza kusimama na

kumfahamisha Spika kuhusu ukiukwaji wa utaratibu huo na katika

kufanya hivyo, atalazimika kutaja Kanuni ya Bunge iliyoweka

utaratibu uliokiukwa.

(4) Endapo Mbunge atafanya kosa ambalo alikwishawahi

kuadhibiwa kwa mujibu wa fasili ya (2) na (3) ya Kanuni hii, Spika

atalipeleka suala lake kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka

ya Bunge kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 71 ya Kanuni hizi ili

Kamati hiyo ilishauri Bunge kuhusu hatua za kinidhamu zinazostahili

kuchukuliwa dhidi ya Mbunge huyo.
Kanuni ya 68 (10) inampa spika kuwa na kauli na uamuzi wa mwisho. Kanuni hii inasema:​

(10) Uamuzi wa Spika kuhusu suala lolote la utaratibu utakuwa

ni wa mwisho.

Kwa sababu bunge ni chombo chenye mamlaka yake na utaratibu wake, adhabu zimewekwa kisheria kwa yeyote anaekiua utaraitibu na utaratibu wa utekelezaji wake umewekwa. Utaratibu huu upo katika kanuni ya 73. Kanuni za 73 (1) na (2) sinasomeka:

73.-(1) Mbunge au Waziri atakayezungumzia jambo au mambo

ambayo hayaruhusiwi na Kanuni hizi, anaweza kuamriwa na Spika

au Naibu Spika au Mwenyekiti akatishe hotuba yake na kukaa mahali

pake.

(2) Endapo Mbunge au Waziri atatumia maneno au lugha

isiyotakiwa Bungeni, yaani lugha ya matusi, usafihi, uchokozi au

lugha ya maudhi na akitakiwa na Spika ajirekebishe kwa kufuta

maneno au lugha hiyo atakataa kufanya hivyo, Spika anaweza

kumwamuru Mbunge huyo atoke mara moja nje ya Ukumbi wa

Bunge na abaki huko nje kwa muda wote uliosalia wa kikao cha

siku hiyo.

Bunge nalo limepewa mamlaka ya kutoa adhabu kufuatia ukiukwaji wa taratibu au utovu wa nidhamu. Kanuni namba 74 (1), (2) na (3)(b) zinahusika. Hizi zinasomeka kama ifuatavyo:

74.-(1) Spika anaweza kutaja jina la Mbunge kwamba amedharau

Mamlaka ya Spika na kisha kupeleka jina hilo kwenye Kamati ya

Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ikiwa:-

(a) kwa maneno au vitendo, Mbunge huyo

anaonesha dharau kwa mamlaka ya Spika; au

(b) Mbunge huyo atafanya kitendo chochote cha

makusudi cha kudharau Shughuli ya Bunge au

Mbunge yeyote anayeongoza shughuli hiyo.

(2) Ikiwa maneno au vitendo vya Mbunge vilivyoainishwa

katika fasili ya (1) ya Kanuni hii vimetokea wakati Bunge likiwa katika

Kamati ya Bunge Zima, basi Mwenyekiti atasimamisha shughuli za

Kamati na ataagiza Bunge kurudia ili kumpatia Spika fursa ya kutoa

taarifa kwa Bunge kuhusu mwenendo wa Mbunge huyo na

kuwasilisha suala hilo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka

ya Bunge.

(3) Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itajadili

suala hilo na ikithibitika kuwa Mbunge husika ametenda kosa

inaweza kushauri kwamba:-

(a) ikiwa ni kosa lake la kwanza Mbunge huyo

asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi kumi; au

(b) ikiwa ni kosa lake la pili au zaidi Mbunge huyo

asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi ishirini;​

Mbali na hayo yote, Bunge limejiwekea miiko yake lenyewe. Bungeni kuna mambo ambayo hayaruhusiwi, miongoni mwa hayo ni yale yaliyomo katika kanuni ya 64 (1)(e), (f) na (g). kanuni hizo ni kama ilivyoainishwa hapa:

64.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 100 ya Katiba yanayolinda

na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge,

Mbunge:-

(a)

(d)

(e) hatazungumzia mwenendo wa Rais, Spika, Mbunge, Jaji, Hakimu au mtu mwingine yeyote anayeshughulikia utoaji wa haki, isipokuwa tu kama kumetolewa hoja mahususi kuhusu jambo husika;

(f) hatamsema vibaya au kutoa lugha ya matusi kwa Mbunge au mtu mwingine yeyote;

(g) hatatumia lugha ya kuudhi au inayodhalilisha

watu wengine.

Kwa hiyo basi ni dhairi kwamba spika wa bunge hakuenda kinyume na kanuni yoyote ya bunge kwa kumtoa mbunge Mnyika nje ya ukumbi wa bunge na kutoa adhabu palepale pasipo uwepo wa Mnyika mwenyewe. Pia spika alitumia misingi ya kanuni kuwashtaki Halima Mdee na Esther Bulaya kwenye kamati ya maadili ya bunge, na uamuzi uliotoka ni sahihi.

Sasa tunarudi kwenye swali letu. Tumeona hapo juu namna judicial review inaweza fanyika, yaani zile test tano zilizoainishwa. Spika alikuwa anafanya kazi ya mamlaka ya dola, na alikuwa anafanya maamuzi kulingana na utaratibu.

Pia judicial review, ikumbukwe sana, haitakuwa na meno kama kilichofanywa kilikuwa ni hatua za kinidhamu. Hapa ieleweke kwamba hatua ya kinidhamu ni ile ya kumchukulia hatua (kutoa uamuzi) mtu ambae ameonekana kafanya kosa dhahili pasipo kumpa mda wa kujitetea. Mnyika hakupewa mda wa kujitetea, Halima na Esther suala lao lilipelekwa kwenye kamati.

Kama chombo kinachotoa uamuzi kinatakiwa kumuita mshukiwa ili ajitetee, hii huitwa quasi judicial action na kimsingi inaweza pitiwa na mahakama katika judicial review.

Tukirudi nyuma, kanuni za buge zimetungwa kwa mamlaka ya katiba, kama bunge lenyewe lilivyo na kiti cha spika kilivyo kwa mujibu wa katiba. Ibara ya 100 ya katiba ya JMT inatoa uhuru wa majadiliano wa shughuli bungeni kwa mujibu wa kanuni na taratibu. Pia kifungu hiki kinatoa zuio kwa mahakama au chombo chochote kuhoji yaliyotokea bungini wakati bunge lipo katika kazi yake. Ibara hii inasimeka ifuatavyo:

100. Uhuru wa majadiliano na utaratibu wa shughuli Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 14

(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge, na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

(2) Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanyw ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.

Kwa vyovyote vile basi Bunge, ikiwa ni pamoja na spika wake, haliko subject to judicial review. Hii ni kwa sababu ya kinga iliyowekewa na katiba. Ikitokwa spika amekuwa so arbitrary kama swali lilivyouliza, hakuna namna ya kufanyia uamuzi wake judicial review. Kuna mamna wanasheria huwa wanapinga baadhi ya vifungu vya sheria zikiwemo ibara za katiba kwa sababu zinakuwa zinakinzana ka Katiba (unconstitutional). Hata hivyo, hata kwa kutotilia maanani ibara ya 100 ya katiba ambayo mwingine anaweza kusema iko kinyume na katiba kwa kuzuia mamlaka ya mahakama, bado spika hatakuwa subject wa judicial review kwa sababu kafuata utaratibu, na kama kuna malalamiko kwamba katumia vibaya madaraka yae labda kwa sababu “Katoa uamuzi wa kukurupuka na uonevu/chuki” bado yuko upande salama. Maamuzi ya kumfukuza mtu bungeni, mbali tu ya kuwa yapo katika kanuni, yanatekelezwa katika misingi ya uamuzi huru au hiari. (Discretional).

Karibuni sana
 
Back
Top Bottom