Heshima kwako kiongozi,
Naomba msaada nina matatizo kazini. Mimi ni mwl ktk shule moja ya private hpa Dar es salaam.
Wameniundia zengwe kuwa nimewapa wanafunzi mtihan, wakanizuia nisiingie kazini
Nilianza kurahisisha, wakamalizia wao. Sasa wametafuta mwl mwingine.
Swali langu
Vp sharia inasemaje kumsimamisha mwajiriwa na kumfukuza bila hata ya kumhoji.
Sijahojiwa, sijaandika maelezo yoyote
Mwisho
Kisheria taratibu zikoje ktk kumsimamisha na kumfukuza mwajiriwa wa miaka takriban tisa (9)
Maana hata barua ya kumsimamisha hawajanipa. Zaidi ya mkuu wa shule kutoa tamko kwa walinzi pale getini kuwa nisiingie.
Natanguliza shukran
.
Mkuu
KUCH KUCH , Kufuatana na maelezo yako, japo ni kwa kifupi, nimekuelewa kwamba mwajiri wako kakuzuia kuingia kazini. Japo hujanieleza kuhusu malipo ya masilahi yako kama vile mshahara au posho, nitakupa ushauri kwa kadri ya maelezo yaliyopo.
Kwa alichofanya mwajiri wako kiko sahihi kisheria. Kulingana na maelezo yako (kwamba una tuhuma za kulikisha mtihani), mwajiri anayo fursa au sababu ya
kukugomea . hii inaitwa Lock Out, na ipo kisheria, chini ya kifungu namba 75 (b) cha sheria za kazi (Emmployment & Labour Relations Act), no. 6 ya mwaka 2004. kifungu hiki kinasema kwamba
(b) every employer has the right to lockout in respect of a dispute of interest. Hapa inamaanisha ya kuwa mwajiri anayao mamlaka ya kumzuia kuingia kazini mwajiriwa yeyote kama kutakuwa na mgogoro wa kimasilahi.
Kama Lockout itakokea, mwajiriwa bado anakuwa na haki ya stahili zake kama vile pesa za kujikimu, malipo ya pesa za pensheni au mifuko ya kijamii nk. Stahiki hizi zimeainishwa katika kifungu cha 83 (4) cha sheria ya mahusiano kazini (6/2004). Hatua hii ya Lockout haimaanishi kuwa mwajiriwa kafukuzwa kazi. Pia hatua hii inatakiwa iwe ya mda flani, si ya kudumu, kulingana na aina ya madai aliyonayo mwajiri. Hatua nyingine ya msingi kisheria ni ya mwajiri kumpeleka mwajiriwa katika kamati za maadili, mabaraza ya usuluhishi au mahakamani kama akiona lockout haijasaidia na mda unakwisha.
Kwa suala lako, ni wazi kuwa mwajiri wako kachukua hatu dhidi yako. hata hivyo sijajua madai yake, maana si madai ya kila aina yanampa wasaa mwajiri kufanya Lockout (kifungu cha 82 cha sheria ya mahusiano kazini). kwa maelezo yako mwajiri angepaswa kukupa barua ya kujieleza huku ukiendelea na kufanya kazi, au angeruhusiwa kuchuka hatua za kinidhamu kama anao ushahidi kamili. Kwa hatua hii aliyochukua, japo ni halali kisheria, inahitaji maelezo ya ziada.
Kama sheria inavyotaka, mwajiri angelipaswa kukupa notisi ya
Lockout. Kama hakuna written notice (kulingana na maelezo yako), notisi ya maneno pekee inatosha. Pia mwajiri hajakufukuza kazi na bado unayo haki ya kupewa stahili zako kipindi chote utakapokuwa nje ya ofisi. Lockout haiishi kinyemela, lazime kuwe na maridhiano baina yako na mwajiri au baina yako na mwakilishi wa mwajiri au msuluhishi. Ua suala lenu linaweza kumalizwa na mahakama kama sheria zinavuoeleza, na mpelekaji wa suala si wewe, bali mwajiri wako.
Kwa sasa tulia na fuatilia kwa mwajiri wako notisi ya maandishi kuhusu hatua iliyochuluwa na nini maoni ya mwajili kuhusu mustakabali ya mgogoro wenu. Kama mwajiri atakuwaka nje ya kazi bila maelezo ya ziada na ya kueleweka zaidi ya siku 30 (thelasini), una haki ya kuchukua hatua dhidi yake. Kwa sasa unatakiwa umuone mwanasheria aliye karibu nawe kwa usaidizi zaidi.