Legal documents na uchambuzi wa masuala ya kisheria hapa

Legal documents na uchambuzi wa masuala ya kisheria hapa

Naombeni mwenye notice za refugee law anisaidie.
Umepata email yangu?

Sasa naweza kukusahihisha.
Unapokuwa katika majukwaa kama haya jitahidi sana kutumia lugha sanifu au kutumia lugha kwa ufasaha, nimekuuliza zaidi ya mara mbili juu ya matumizi ya NOTICE badala ya Notes kwenye maandishi yako.

Pili, hizo nilizotuma ni chache kati ya nyingi ambazo unaweza ukapata hapo Chuoni, unaweza onana na Madame Dr. Massabo (Associate Dean) ni mmoja wa wakufunzi wa hilo somo ukamuomba materials za Sheria za Wakimbizi na atakusaidia bila hiyana pamoja na kuwa wanafunzi wengi hawampendi huyu mama kutokana na u_serious wake.

Lakini pia, unaweza mtafuta Prof. Rutinwa akusaidie materials za hilo somo na huyu ndio yupo vizuri zaidi kwani ndiye Course Coordinator, na huwa anatoa hadi Books, Statutes na Resources zingine ambazo ulipaswa kuzinunua bure kabisa.

Mwisho ingia Maktaba, Maktaba na Mwanasheria ni vitu visivyotengana, jenga mazoea ya kwenda kuyasaka maarifa Maktaba, Maktaba ya UDSM hasa LAW COLLECTION imesheheni vitabu ambavyo wanafunzi wa vyuo vingine wanavisikia tu na kama wanavyo basi ni kama shule za kata kitabu kimoja Darasa zima.

Narudia tena jijengee mazoea ya kwenda kujisomea vitabu pale Maktaba, kukazia hoja yangu nakupa hii toka kwa Benjamin Nathan Cardozo: "A law student is more than a walking library, more than a soldier in the army..."

Nakutakia mafanikio mema katika masomo yako, Mwenyezi Mungu akusimamie.
 
Bado sijaipata na pia na shukuru kwa ushauri mzur nakuahid ntaufanyia kazi ipasavyo.

Asante sana
 
Mkuu sagaciR unaonaje ukiweka inviting link ya ku-join hilo group au namba ya admin tum-inbox atuunge? I would love to join!
 
swali zuri lakin jibu lake ni refu sana. tutaftane kama unahitaji kufanya hivyo ila kama ni kwa ajili ya kujifunza tu pia siyo mbaya, but i need sometime kukaa online ili niandike majib hapa
 
Msaada tartibu za kufuatwa kuandaa urithi/mirathi.
Kisheria....
Mkuu kisheria mirathi ina mtiriririko wake maalum. Kwa ufupi unaanza kikao cha ndugu/warithi cha kupendekeza jina la msimamizi wa mirathi, baadaye msimamizi anafungua shauri mahakamani (inaweza kuwa mahakama ya mwanzo au mahakama kuu, kutegemea mazingira ya shauri jenyewe). Baada ya mahakama kusikiliza shauri hilo (huanza kusikilizwa baada ya mda uliowekwa kupita, ili kutoa fursa kwa anaetaka kupinga mirathi ile), msimamizi wa mirathi hutauliwa rasmi na mahakama.

Kuandaa urithi ni kitu tofauti na usimamizi wa mirathi katika misingi ya sheria. Kwa mazingira flani msimamizi anakuwa mwandaaji na msimamizi mkuu wa mali ya urithi kwa ajili ya warithi.
 
Naomba case
Hapa tutakuwa tunatoa documents (nyaraka) mbalimbali za kisheria ambazo mtu atahitaji kama vile case laws, hasa ambazo ni unreported, legislations, law books n.k.

Binafsi nina e-library kubwa sana na napenda kushirikisha wengine kwa hivi vitu, isipokuwa kuna baadhi ya vitabu vina kopyright so sitoweka hapa kwenye public itabidi nikutumie kwa email adress au vinginevyo.

Pia mjadala wowote wa kisheria ni vizuri ukawekwa hapa ili tuwekane sawa.

Wanasheria karibuni sana
law ambayo inakataa jaji kujitoa kwenye kesi
 
Back
Top Bottom