.
Kiongozi
Retired ,
Power of attoney ni hati inayotoa na kudhibitisha mamlaka ya mtu fulani kufanya kitu fulani kwa niaba ya mtoaji. [the power of attorney is defined to be
a document executed by a person in favour of another empowering the latter to do any lawful act or acts for and on behalf of the donor:… (Ahmed Ibrahim Bora v. Mehboob Abdulkarim Shivji & Another, Misc. Commercial Cause No. 17 of 2007)]
Power of attorney kimsingi zipo za aina mbili:- (1) inayompa mtu au kampuni kusimamia na kutekeleza shughuli mbalimbali zinazohusu mali na haki za mtu au kampuni, na (2) inayompa mtu au kampuni haki ya kusimamia kesi katika mahakama za Tanzania. Aina zote hizi mbili ni sharti zisajiliwe kisheria ili kuwa halali. Ile ya kwanza inasajiliwa chini ya the Registration of Documents Act, cap 117 na the Land Registration Act, cap 334.
Mtu yeyote mwenye age of majority na mwenye akili timamu anao uwezo wa kutoa Power of Attorney au kupewa Power of Attorney, kulingana na matakwa na dhamira ya Power of Attorney yenyewe. Pia kampuni inaweza kutoa na kupewe Power of Attorney. Hata hivyo hati hii ya Power of Attorney lazima iwe katika mfumo wa kiapo, na isainiwe na wakili au kamishina wa viapo.
Kama nilivyoeleza hapo awali, kampuni pia inao uwezo wa kutoa POA. Inaweza kutoa kwenda kwa kampuni, wakili au kwa mtu binafsi. Inaweza hata kutoa POA kwa mteja wake, kulingana na dhamira ya POA yenyewe. Kuhusu kampuni kumpa mtu POA kusimamia kesi ya Ardhi ni tata. Kwa Tanzania hairuhusiwi mtu kusimamia kesi katika mwavuli wa POA isipokuwa katika mazingira yafuatayo:
1. Anayewakilishwa awe nje ya mipaka ya Tanzania na hawezi kufika nchini kirahisi. [
Zarina Mohamed v Leonida Sakulo, Land Case No. 166/2010 (unreported);
Georgia Celestine Mtikila Vs. Registered Trustees of Dar es salaam Nursery School & Another [1998] TLR 512;
Property Consultancy v Seemi Probil Co Ltd & Others, Land Case No. 258/2008;
Naiman Moiro Vs Nailejiet K. J. Zablon [1980] TLR 274]
2. Anayewakilishwa isiwe kampuni au corporate body, Kampuni inawakilishwa na wakili au athorised officer (afisa wa kampuni) lakini sio wakala. Mtu mwenye hisa katika kampuni anao uwezo kuwakilisha kampuni katika shauri kwa niaba ya wanahisa wengine pekee, si kwa niaba ya kampuni [
Ahmed Ibrahim Bora v Mehboob Abdulkarim Shivji & Another, Misc. CC No. 17/2017. Angalia pia
John Nyaronga v Captain Ferdinando Ponti & 2 others, CC No. 62/2009 (Mruma, J.)] Kampuni itawakilishwa na meneja wake, mwanabodi wake au katibu wake lakini ni lazima iidhinishwe na Bodi ya kampuni (company resolution) – Kanuni ya 30 (3) ya Court of Appeal Rules, 2009.
3. Kwa baadhi ya mashauri mtu anaweza kuwakilisha mtu kwa mwavuli wa POA katika mahakama za mwanzo, ambako CPC na sheria zingine hazitumiki na wana kanuni zao za kuendesha mashauiri [
Deemay Sikay v Neema Magoni, CAT Civil Appeal No. 3/2011 (unreported)]
4. Mwakilishi anaeshikilia POA sharti aidhinishwe na Msajili wa Mahakama ya Rufani kusimamia kesi hiyo kama kesi iko mahakama ya Rufani, kama ni mahakama kuu ni lazima iidhinishwe na Msajili wa mahakama kuu.
Kwa ufupi POA haifanyi kazi kama mwenye kesi yupo ndani ya mipaka ya nchi [Angalia kanunu ya 30 (2) ya Court of Appeal Rules 2009, ambapo hata Mahakama za chini hufuata utaratibu huo. Pia angalia kesi za
Abbas Khatib Haji v Haidar Thabit Kombo, CAT Civil Appeal No. 5/2002 (unreported) na
Hamisi Kirumbini v Pantaleo Asenga, CAT Civ. Appl. No. 157/2005 (unreported)].
Kwa maelezo haya kampuni hiyo ya wahindi kama ulivyoeleza haina msingi kisheria kumpa mtu POA kusimamia kesi yao.
Karibu sana.....