Legends of the Land – Tuinue Utalii wa Ndani, Tuoneshe Nguvu ya JamiiForums!

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Hoja Yangu kwa Wanajukwaa na Wasimamizi wa JamiiForums:

Wana JF wenzangu,

Nchi yetu imebarikiwa kwa natural wonders ambazo dunia nzima inazitamani – kutoka kilele cha mlima mrefu barani Afrika, Mlima Kilimanjaro, hadi Ngorongoro Crater yenye historia ya kipekee, Serengeti yenye migration ya kipekee duniani, hadi Tarangire yenye msitu wa miombo na tembo wakubwa zaidi. Lakini cha kusikitisha, mara nyingi ni wageni tu ndio wanaopata nafasi ya kuyaona maajabu haya, wakati sisi wenyewe, wazawa na wenye nchi, tunabaki kuwa watazamaji kwenye postcards na documentaries.

JamiiForums ni zaidi ya platform – ni movement. Hapa kuna fikra, nguvu na sauti kubwa kuliko tunavyofikiria. Tukiamua kama jukwaa, tunaweza kuonesha kuwa sisi sio tu wachambuzi wa habari bali pia ni washiriki hai wa maendeleo ya utalii wa ndani. Hebu tufanye kitu kikubwa na cha historia:

Tuanze na expedition ya kupanda Mlima Kilimanjaro, tukibeba bango lenye alama ya JamiiForums kwenye kilele cha Uhuru Peak (5,895m). Hii itakuwa symbolic statement kwamba JF ni jukwaa linalogusa anga zote za maendeleo – hata literally, from the grassroots to the rooftop of Africa. Baada ya hapo, tuendelee na expeditions Ngorongoro, Serengeti na Tarangire, tukionyesha kwa vitendo kwamba tunathamini na kuwekeza katika urithi wetu wa kiutalii.

Kwa urahisi wa uratibu na majadiliano ya kina zaidi (ambayo hayawezi kufanyika vizuri humu kutokana na thread limitations), nimeanzisha group la WhatsApp linaloitwa:

“Legends of the Land – Tanzania Explorers”

Lengo lake ni kurahisisha mawasiliano, kupanga ratiba, kuchangia mawazo na kuweka mikakati ya namna ya kufanya haya maandalizi kwa usahihi mkubwa.

Naomba kwa heshima kubwa Admins wa JF waturuhusu wana-Jukwaa wenye nia kujiunga ili tufanikishe hii movement.

Hii siyo tu safari, bali ni statement ya kizalendo na kitalii – kuwa sisi WanaJF tunaweza kuhamasisha watanzania kupenda vivutio vyao na kuwekeza kwenye utalii wa ndani.

Tuanzishe historia. Tukutane juu ya paa la Afrika na tuandike jina la JamiiForums kwenye upepo wa milele.

Who’s in?
 
Habari,

Maoni yako yamesomwa.
 
Binafsi huwa naona ni ngumu sana ku mobilize watu humu kufanya jambo la wazi kama hilo kwasababu members wengi ni majini yani siyo verified members, hivyo kufanya jambo la wazi kuwa gumu.
 
Back
Top Bottom