Pre GE2025 Lema afunguka baada ushindi wa Tundu Lissu Uchaguzi CHADEMA, Mbowe ni kaka yangu ila Lissu ni bora zaidi wakati huu

Pre GE2025 Lema afunguka baada ushindi wa Tundu Lissu Uchaguzi CHADEMA, Mbowe ni kaka yangu ila Lissu ni bora zaidi wakati huu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Godbless Lema avunja ukimya baada ya ushindi wa Tundu Lissu Uchaguzi CHADEMA adai yeye kwenda kinyume na Mwenyekti Freeman Mbowe ilikuwa ngumu sana.

"Nitendo gumu la kisiasa, katika matendo magumu ya kisiasa nimeshawahi kuyafanya hili ni namba moja katika maisha yangu, Mbowe ni kaka yangu, ni ndugu yangu kabisa lakini niliamini kwamba Lissu anaweza kuwa kiongozi bora kwa wakati huu..."

"Umekuwa uchaguzi wa kidemokrasia na kila mtu ameona mchakato ambao ulikuwa mubashara kupitia vyombo mbalimbali niseme tu tumeshinda kwa haki na tunakwenda kuanza kazi mara moja"

Mhe. Lema umefanya kazi kubwa na sasa unaweza kurejea rasmi Arusha kuchukua jimbo. Umefanya kazi kubwa kutenganisha ukanda na Utaifa. Umesimama na kuhakikisha mwenye haki anapewa haki yake.

Siasa za Tanzania zitakukumbuka kwa mambo mengi. Mshauri vyema bosi wako mpya kwa malengo ya kupanga safu inayounganisha chama na kuvuka salama katika misukosuko ya kisiasa.
 
Ndio njia pekee ya kuwa chama serious kujitofautisha na CCM kama CDM itaendelea kuchagua watu bora na siyo kuangalia kabila la mhusika, undugu, urafiki. Lema ni mfano wa kuigwa hata na CCM.
 
"Nitendo gumu la kisiasa, katika matendo magumu ya kisiasa nimeshawahi kuyafanya hili ni namba moja katika maisha yangu, Mbowe ni kaka yangu, ni ndugu yangu kabisa lakini niliamini kwamba Lissu anaweza kuwa kiongozi bora kwa wakati huu..."

"Umekuwa uchaguzi wa kidemokrasia na kila mtu ameona mchakato ambao ulikuwa mubashara kupitia vyombo mbalimbali niseme tu tumeshinda kwa haki na tunakwenda kuanza kazi mara moja"
Hongera Godbless Lema.Umetanguliza utaifa kwanza badala ya ukanda na ukabila.Historia itakukumbuka.
 
Hongera Godbless Lema.Umetanguliza utaifa kwanza badala ya ukanda na ukabila.Historia itakukumbuka.
Hata mimi sikuamini. Nilidhani ni strategy ya Mbowe kumfanya adui wa mchongo ili amsaidie kwenye kuhesabu kura. Hongera yake.
 
Sasa midomo na masimango viachwe. Ibaki kufanya kazi za chama kuendelea kurushiana manebo hasa kwa viongozi sio sawa. Lema keshafanya kazi yake akae kimya vinginevyo nikuendelea kutengeneza yasiyotakiwa kutengenezwa
 
Back
Top Bottom