Lema ana malengo gani na CHADEMA? Matendo yake yanatia wasiwasi

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Sio mara ya kwanza Lema kutiliwa wasiwasi na wanachama wa Chadema.

Kipindi cha Uchaguzi wa Mkiti kanda ya Kaskazin alisusa akakimbia Canada, hata wakati wa Uchaguzi wa Mkiti taifa uliomuondoa Mbowe alionekana kumuunga Lissu kwa shingo upande hakuwa na option nyingine.

Kwenye kikao cha Kamati Kuu Kigoma alisema anataka Heche Makamu Mkiti apishe kikao ili wajadili pesa za Tone Tone.

Baadae mtandaoni akaandika, iwapo maazimio ya Kamati Kuu yataenda kinyume atalazimika kujitetea mwenyewe.

Jana Lema kasema Heche huwa anafanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, DGIS.

Hivi lengo la Lema kwa chama ni nini haswa, kukisambaratisha, kuonyesha umma Heche hafai au kuonyesha bila yeye hakuna chama.

====
Lema ajitetea.

Kutoka ukurasa wake wa X.
============
Nimeona matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Mama Samia, hasa niliponukuu salamu za pole za Mwenyekiti Lissu kutoka gerezani.

Kwa sisi jamii tunaodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, hili linapaswa kutufikirisha. Kutofautiana kwa hoja hakuhitaji matusi, dhihaka wala chuki.Lissu amekaa gerezani takribani mwaka mmoja na miezi sita, akikabiliwa na kesi ambayo sisi tunaamini ni ya kisiasa na isiyo na haki.

Anafahamu yaliyompata na serikali iliyomweka mahabusu. Lakini alipofahamishwa kuhusu msiba wa mume wa Mama Samia, akiwa mbele ya mahakama, alitoa salamu zake za pole kwa wafiwa mara mbili.Huu si unyonge. Hii ni hekima, utu na ukomavu wa kiwango cha juu.

Na si mara ya kwanza. Aliwahi pia kumtetea Sabaya katika kesi yake Moshi. Wengi tulishangaa, nami nilishangaa. Lakini nilipomuuliza baadaye, nilielewa kwamba kwake haki haichagui upande.

Hilo ndilo fundisho kubwa tunalopaswa kulibeba. Tunaweza kupinga serikali, kudai haki na kupigania demokrasia bila kujenga harakati zetu juu ya chuki na kisasi.

Lakini kama tunasema tunampenda Lissu, basi pale anaposema ana pumzi ya kuvumilia mateso na kukaa gerezani, sisi tunapaswa kuchukua kauli hiyo kama mwito wa ujasiri, si ruhusa ya kukaa kimya.

Kama tunaamini kesi hii si ya haki, basi viongozi tunanapaswa kuwaongoza wananchi katika hatua za amani, kisheria na kidemokrasia za kudai haki, pengine kwa njia ya maandamano. Sio kwenye keyboard tu na microphone.

Demokrasia inahitaji wananchi wanaothubutu kusimama kwa kile wanachoamini. Na kama siku moja tutapata nafasi ya kuongoza nchi hii, tusije tukarudia makosa tunayoyapinga leo. Lazima tutawala kwa haki, utu na dhamira njema.

Mimi nitasimama kwenye upendo, utu na haki siku zote ktk kazi hii. Anyway , hekima ya Lissu kutoa pole kwa Mama Samia was a top-class thinking. Inaonyesha kwamba hata unapoteseka, unaweza kuchagua utu, hata unapopinga, unaweza kukataa kisasi.

Wakati mwingine Mungu hataki umshinde adui yako kwa chuki, bali kwa upendo, hekima na maisha yenye ushuhuda kwamba uovu wake haukukushinda.

Mimi niko tayari kusimama kwa amani na kwa ujasiri. Katika hatua ya kupigania uhuru wa Lissu kuwa nje ya kuta za gereza na sio kusema ana pumzi ya kukaa jela hata maisha.

Tuna watu wengi sana Chama hiki , pumzi yetu itoke mtandaoni , fikeni tu hata mahakamani kwa sasa na huku viongozi wakuu watusaidie kutafakari jambo muhimu la haki , sheria na amani.

β€œYou don’t have to hate those who hurt you. Sometimes the greatest revenge is to rise above them with peace, dignity, and success.”Thank you !!
6:00 AM Β· Sep 14, 2026

====
Majibu ya Lema: πŸ‘‡πŸ½


View: https://www.instagram.com/p/DdQH6YTiumo/
 
hiyo ni ngori kabisa gentleman
 
sasa lema si anasema wazi?

Acha amwage mboga.
 
sasa lema si anasema wazi?

Acha amwage mboga.
Yes,
heche alipokea pesa za tone tone kupitia akaunti yake binafsi, ambazo hakuziwasilisha kwenye chama,

so,
kwa heshma lema akaomba heche atoke kwenye kikao husika cha kamati kuu Kigoma, ili hatimae viongozi wajadili hali hiyo, ila katibu mkuu akamkingia kifua heche. Na ndio maana kutoka hapo michango ya tone tone ya ikiwa ni pamoja na ile milioni 334 ikasuasua na hatimae kukwama kabisa.

So,
heche anabaki kuongeza tuhuma tu dhidi yake mwenyewe.

1. Ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi.

2. Usaliti dhidi ya mwenyekiti wake na chadema kwa ujumla πŸ’
 
Yaani mtu unaleta maada then unakuja kujichangia kwa id tofauti ili uonekane unawachangiaj
 
Chadema ni chama cha Kaskazini, na malengo yake makuu ni uchumi na kukipasha joto CCM isilale usingizi wa pono katika kuwahudumia wananchi. Yaani kulikuwa na win-win kati ya chadema na CCM, hata Nyerere alikipenda chadema kuliko vyama vingine vya upinzani kwa sera zake.

Baada ya wahuni akina Heche kumpora Mbowe chama, sasa hivi ni Heche na Lissu tu m wanaokifaidi chama kiuchumi na kujulikana.

Lazima chama kirudi kwa wenyewe wa kaskazini na waKKKT kiendelee na malengo yake. Maana Mzee Mtei, Mbowe na Makani hawezi kuanzisha chama ambacho kinaweza kutumika kuichoma moto nchi yote kabisa kama hivi:
https://www.facebook.com/
View: https://www.facebook.com/watch/?v=988605313638635
 
Tatizo la Lema na Chadema kwa ujumla ni kila mtu kuwa msemaji wa mambo ya chama kitu ambacho CCM wamefanikiwa kuzima.

Lema kila siku yuko social media, kila issue anajibu ndio maana lazima utaongea hata yasiyotakiwa. Kama suala la Lissu kutoa pole limepostiwa na Brenda inatosha yeye ana repost basi.

Law 4: Always say less than necessary!!
 
Na bahati mbaya baadhi ya mapandikizi ni watu ambao wanachama na wapenzi wa hivi vyama vya upinzani wamewaamini kwa muda mrefu, lakini nyuma ya pazia Watu hao ni hatari sana.....
Sahihi mkuu.. Tuna safari ndefu
 
Siku zote ukitaka kuua hakikisha unawachonganisha wagombane wenyewe Kwa wenyewe. Hata Lisu kutoa zile kauli za kukinukisha ilikuwa ni kosa kubwa sana hata kama ilikuwa sio Nia kamili lazima wajuwe kuwa wawe makini sana na nini wanaongea maana ni watu wanaowindwa sana wakosee hata Kwa maneno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…