Lema ana malengo gani na CHADEMA? Matendo yake yanatia wasiwasi

Lema ana malengo gani na CHADEMA? Matendo yake yanatia wasiwasi

Lema ajitetea.

Kutoka ukurasa wake wa X.
============
Nimeona matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Mama Samia, hasa niliponukuu salamu za pole za Mwenyekiti Lissu kutoka gerezani.

Kwa sisi jamii tunaodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, hili linapaswa kutufikirisha. Kutofautiana kwa hoja hakuhitaji matusi, dhihaka wala chuki.Lissu amekaa gerezani takribani mwaka mmoja na miezi sita, akikabiliwa na kesi ambayo sisi tunaamini ni ya kisiasa na isiyo na haki.

Anafahamu yaliyompata na serikali iliyomweka mahabusu. Lakini alipofahamishwa kuhusu msiba wa mume wa Mama Samia, akiwa mbele ya mahakama, alitoa salamu zake za pole kwa wafiwa mara mbili.Huu si unyonge. Hii ni hekima, utu na ukomavu wa kiwango cha juu.

Na si mara ya kwanza. Aliwahi pia kumtetea Sabaya katika kesi yake Moshi. Wengi tulishangaa, nami nilishangaa. Lakini nilipomuuliza baadaye, nilielewa kwamba kwake haki haichagui upande.

Hilo ndilo fundisho kubwa tunalopaswa kulibeba. Tunaweza kupinga serikali, kudai haki na kupigania demokrasia bila kujenga harakati zetu juu ya chuki na kisasi.

Lakini kama tunasema tunampenda Lissu, basi pale anaposema ana pumzi ya kuvumilia mateso na kukaa gerezani, sisi tunapaswa kuchukua kauli hiyo kama mwito wa ujasiri, si ruhusa ya kukaa kimya.

Kama tunaamini kesi hii si ya haki, basi viongozi tunanapaswa kuwaongoza wananchi katika hatua za amani, kisheria na kidemokrasia za kudai haki, pengine kwa njia ya maandamano. Sio kwenye keyboard tu na microphone.

Demokrasia inahitaji wananchi wanaothubutu kusimama kwa kile wanachoamini. Na kama siku moja tutapata nafasi ya kuongoza nchi hii, tusije tukarudia makosa tunayoyapinga leo. Lazima tutawala kwa haki, utu na dhamira njema.

Mimi nitasimama kwenye upendo, utu na haki siku zote ktk kazi hii. Anyway , hekima ya Lissu kutoa pole kwa Mama Samia was a top-class thinking. Inaonyesha kwamba hata unapoteseka, unaweza kuchagua utu, hata unapopinga, unaweza kukataa kisasi.

Wakati mwingine Mungu hataki umshinde adui yako kwa chuki, bali kwa upendo, hekima na maisha yenye ushuhuda kwamba uovu wake haukukushinda.

Mimi niko tayari kusimama kwa amani na kwa ujasiri. Katika hatua ya kupigania uhuru wa Lissu kuwa nje ya kuta za gereza na sio kusema ana pumzi ya kukaa jela hata maisha.

Tuna watu wengi sana Chama hiki , pumzi yetu itoke mtandaoni , fikeni tu hata mahakamani kwa sasa na huku viongozi wakuu watusaidie kutafakari jambo muhimu la haki , sheria na amani.

“You don’t have to hate those who hurt you. Sometimes the greatest revenge is to rise above them with peace, dignity, and success.”Thank you !!
6:00 AM · Sep 14, 2026
 
Tnakubali kabisa Lissu ni msomi, na akili sana
Lakini sio mwanasiasa, ndio maana huwa anaongea kwa kufokafoka, maana yake anashindwa kutofautisha kuwa mwanasiasa na kujua nini cha kuongea kwa wakati muafaka unaoendana na muda.
Kusema kukinukisha, tutazuia uchaguzi usifanyike na kutambua tutaumizwa ni dhahiri alichosema kilitafsiriwa moja kwa moja na wananchi kuwa ni kuwasha moto.
Na kweli moto uliwashwa na watu waliumia
Sasa mpaka hapo tayari kuna Circumstantial evidence
Hakika. Hata mahakamani unaona kabisa Ile discipline Kwa ajili ya majaji haipo. Unaweza kuwa na Hali kabisa lakini zile kebehi wakiwa mahakamani atajikuta kesi inaishia mahakama ya rufani(rufaa)
 
Ujue Lisu yupo pale alipofikia kutokana na kauli zake. Nachomaanisha ukiwa upinzani lazima uongee Kwa uangalifu sana maana wako most wanted.
Lissu hayupo pale kwa sababu ya kauli zake yupo pale kwa sababu ya msimamo wake, hapendi kuonewa wala kuonea ni muumini wa haki, yeye ni tofauti na sampuli za akina Mbowe au Zitto vinginevyo angekuwa uraiani siku nyingi.
 
Tnakubali kabisa Lissu ni msomi, na akili sana
Lakini sio mwanasiasa, ndio maana huwa anaongea kwa kufokafoka, maana yake anashindwa kutofautisha kuwa mwanasiasa na kujua nini cha kuongea kwa wakati muafaka unaoendana na muda.
Kusema kukinukisha, tutazuia uchaguzi usifanyike na kutambua tutaumizwa ni dhahiri alichosema kilitafsiriwa moja kwa moja na wananchi kuwa ni kuwasha moto.
Na kweli moto uliwashwa na watu waliumia
Sasa mpaka hapo tayari kuna Circumstantial evidence
Ona takataka hii, Lisu alishtakiwa lini na uchaguzi ulikuwa lini?
 
20260914_082135.jpg
 
Tatizo la vyama vya upinzani, ni kuwepo mapandikizi mengi sana ya CCM na ni kazi ngumu sana kuyamaliza...
Kila siku wanafika bei na kila siku wananunuliwa wengine hiyo haitakuja kuisha.
Waswahili wanamsemo wao njaa haimpendezi mtu .
 
huyu ameahidiwa kurudishwa kwenye nafasi yake , game ni kwamba TL wamkute na hatia ,apoteze sifa, huyu bwana na kundi lingine ndani lirudi kwenye maridhiano, zile safari za kizimkazi na kule kwenye uzinduzi ni sehemu hiyo ya deal
 
Tatizo la Lema na Chadema kwa ujumla ni kila mtu kuwa msemaji wa mambo ya chama kitu ambacho CCM wamefanikiwa kuzima.

Lema kila siku yuko social media, kila issue anajibu ndio maana lazima utaongea hata yasiyotakiwa. Kama suala la Lissu kutoa pole limepostiwa na Brenda inatosha yeye ana repost basi.

Law 4: Always say less than necessary!!
Lakini Mbowe aliwahi kiyasema haya yote kipindi cha uchaguzi na akashambuliwa sana, licha ya mapungufu yake.

Party politics za Africa zinahitaji Mtu mmoja mwenye nguvu sana na anayeweza kucontrol makundi yote. Raila aliweza hilo na alikuwa kingmaker akitaka maridhiano yanatokea akitaka kuingia serikalini anaingia akitaka maandamano kinanuka, na yeye ndio alikuwa kila kitu. Hii style ya Chadema sio salama sana; kila mtu anataka kusema - na hakuna mwenye uwezo wa kucontrol hilo kwa sasa. Mbowe aliweza sana kuicontrol Chadema na viongozi wake. Not now

So, Chadema wazoee kuwa hizi ni siasa mpya lakini zina risk yake.
 
huyu ameahidiwa kurudishwa kwenye nafasi yake , game ni kwamba TL wamkute na hatia ,apoteze sifa, huyu bwana na kundi lingine ndani lirudi kwenye maridhiano, zile safari za kizimkazi na kule kwenye uzinduzi ni sehemu hiyo ya deal
Sidhani, hata Lissu akikutwa na hatia Mbowe hawezi kuwa Mkiti.
 
Kwani Lema ni msemaji wa chama? Mbona amekuwa kiherehere hivi🙆‍♂️
Anafanya haya kwa maslahi ya nani?
 
"Nimeona matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Mama Samia".

Lema huu sio mwandiko wako ni mwandiko wa CCM.
 
Mi binafsi huwa simwelewi kabisa, watu tunapigania katiba Chadema kinapigania katiba yeye anapingana na chama.

HVFgFSiXgAALwGz.jpg
 
Back
Top Bottom