☑️Good!. Sina tatizo na wewe kuwa kiongozi wa kiroho...
☑️Sasa mbona u miongoni mwao washabikiao mauaji ndugu
Rabbon kiongozi wa kiroho? Unaongoza roho gani kwani? Au umesahau umeandika nini huko juu?
☑️How? Kama kiongozi wa dini/kiroho unapendekeza vitokomezweje? Kwa njia ya kuwaua mashoga?
☑️Nakushauri kitu kimoja tu wewe kiongozi wa kiroho. Wafundishwe watu kumjua na kumheshimu Mungu kanisani kwako..!
☑️Acha ushabiki usio na msingi wa NENO la MUNGU..!!
☑️Wewe kama kiongozi wa kiroho, huwezi kutumia njia hiyo unless uniambie ni kina nani kwenye Biblia walitumia njia hiyo kuishinda dhambi na uovu...
Waefeso 6: 11 - 12
"....Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho...."
☑️Kabla ulikuwa unaeleza vizuri sana lakini ghafla ukapoteza maboya ukaanza kuhamadisha vita vya damu na nyama..!
☑️Ndugu
Rabbon, adui yako sio SHOGA wala MSAGAJI. Adui zako ni hao kwenye bold ink kwenye mistari hiyo ya Biblia. Pingana na hao. Don't fight the wrong enemy..
☑️Biblia inasema hivi kuhusu silaha za kutumia kupigana vita hiyo;
Efeso 6: 13 - 18
".....
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;..."
☑️Katika silaha zote zulizoorodhoshwa hapo juu hakuna Silaha ya maandamano..!!
☑️Wewe kama kiongozi wa kiroho kama ulivyojiita, hii ndiyo njia sahihi ya kushughulikia uovu..?
☑️It doesn't matter at all..
☑️Kuishiwa uvumilivu Haina maana utumie njia yoyote kushughulikia ambacho kinakufanya uishiwe uvumilivu. Vinginevyo hata wewe utajikuta ukitenda makosa yaliyokukoseshea uvumilivu...!!
☑️Wewe kama kiongozi wa kiroho waambie watu kutumia njia sahihi kupambana na uovu wowote...!!
☑️Ndiyo endelea nao...
☑️Wafundishwe watu huko kanisani/msikitini kwako kutumia njia sahihi kupambana na adui kama ambavyo mtume Paulo kaziweka wazi hapo juu kwa Waefeso...
☑️Mkikosea tu nyie viongozi wa kiroho kuwaelekeza na kufundisha watu mtakuwa mnapigana na adui asiye sahihi, Kwa njia zisizo sahihi na hivyo mtashindwa tu...!!
☑️Kumbe nyie viongozi wa kiroho mnatetea nini? Matetea sheria za jino Kwa jino siyo..?
☑️Godbless Lema na CHADEMA wamefanya ya upande wao. Fanya na wewe palipopungua...!!
☑️Na Mimi ni hayo tu japo ni mengi...!!