Lema atua Tanga Mjini, ashangaa na kulia baada ya kukuta Watu bado wanaishi kwenye Magofu zama hizi!

Tuseme ni mpumbavu au mjinga ?
 
Lema ameshangaa kabisa kuona vijumba? Hahaha, noma sana huyu kamanda, aende Canada miaka kumi akirudi atakuwa anarudisha kichwa nyuma kunyoosha nywele zake.
 
Lema yuko sahihi,sema wahuni hawataki wananchi waamushwe kwenyeusingizi mzito ambao umewasababishia umasikini wa kutupwa,kutokana na sera mbovu za serikali ya ccm.
Umesema vyema sana.

Watanzania sisi tunahitaji kuamshwa toka kwenye usingizi mzito tuliolala.

Watu wetu wamepigwa na umaskini kiasi kwamba hawafahamu tena namna yakutoka.

Imefika sehemy kuishi kwenye nyumba duni na kukosa hata chakula wananchi wanaona ni sawa tu, Mungu ndiyo kawapangia hivyo. Inasikitisha sana.

Acha Lema awaamshe.
 
Mshamba katika ubora wake yaani mlevi huyu ndo awe kiongozi [emoji23][emoji23][emoji23]labda kwa wavuta bhangi
Uongozi unapewa na watu na hilo kwa Lema sio jambo la ajabu anapewa anytime akigombea kwani mfano tumeuona majuzi aliporudi.
Ni kwa vile nyie msie mpenda lolote asemalo mna crash kupinga ukweli, lakini wapenda ukweli wanamkubali hoja zake
 
Hivi na mm siku nikienda kanada na kurudiii nitakuja na ulimbukeni namna hiii??
Hivi kuishi kwenye magofu ya waarabu hadi leo sio umasikini? Mlitaka awakejeli na kuwaambia magofu hayo ni fahari kwa Tanga?
Mnatia kinyaa kwa ujinga wa aina hii
 
Lema ingekuwa amezaliwa huko alikotoka halafu iwe ndo mara yake ya kwanza kufika Tanzania angetuua kwa presha kwa haya Mambo aliyoyakuta, yaani Lema wakutuona sisi tunaishi kama wadudu kweli.........!
nmecheka sana [emoji23][emoji23][emoji23] Yani nikiwaza ulivyoongea kwa uchungu
et wadudu
 

..nguvu inayotumika kupotosha hotuba za Lema au kumkashifu ni ushahidi kwamba Ccm hawana majibu ya hoja zake.

..Kuna tatizo la umasikini nchini. Kitu anachofanya Lema ni kuwaelimisha wananchi waukatae umasikini.

..Jambo lingine anawaelekeza wananchi kwamba utawala mbaya wa Ccm ndio chanzo cha umasikini hapa nchini.

..Ccm wanaogopa kwamba wamachinga, bodaboda, mama ntilie, wakiamini anachokisema Lema, chama chao hakitakuwepo ktk maeneo yote ya mijini.
 
Kweli kama unaongelea moyoni basi unge-"appreciate" mambo positive aliyokuwa afafanya JPM, mie naona hapo unaleta unafiki, huku unasema haya baadaye unasema mtu aliyekuwa anajitahidi kujenga uchumi mzuri hafai
 
Ila watu wa Tanga siyo maskini' kiviiile, hayo magofu mostly ni culture tu asiwachukulie poa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…