Lema atua Tanga Mjini, ashangaa na kulia baada ya kukuta Watu bado wanaishi kwenye Magofu zama hizi!

Lema atua Tanga Mjini, ashangaa na kulia baada ya kukuta Watu bado wanaishi kwenye Magofu zama hizi!

Kwani huyo mlimbikeni kayaona Leo mpaka ajifanye kushaangaa, kama sio kejeli na ulimbukeni usio na maana? Anawasanifu wenzake wanakaa kwenyemagofu, bila hata kuwachangia ata mfuko Mumoja wa simenti hizo so kejerii?? Haya yeye tukifuatilia ndugu zake wote WA damu wanaishi kwenye magorofa?
Ndugu mwanabodi haya sio majibu sahihi ya hoja iliyoko mezani!

Mtu anauekuamsha usingizini unamwitaje limbukeni?
Kukueleza ukweli kuwa unakaa kwenye magofu inabidi ukae kwenye makazi Bora unamwita Limbukeni? Angesema mtu wa CCM ungeunga mkono bila Shaka yoyote na ungesema serikali Ni sikivu na imeona matatizo ya watu wake!

Lema hawezi kuwachangia mifuko ya cement amewachangia mawazo, waiambie serikali iwe na Sera nzuri ya viwanda na biashara ili gharama ya vifaa vya ujenzi ishuke au iwe himilivu!

Serikali ije na sera Bora ya nyumba na makazi kwa.kujenga nyumba za gharama nafuu na kuziuza kwa wananchi kwa cash au mkopo kupitia shirika la nyumba!

Serikali ije na sera Bora ya kilimo, viwanda na biashara ili sekta hizo ziajiri watu wengi zaidi ili wawe na kipato Cha kuwa na makazi Bora badala ya kukaa kwenye Nyumba za nyasi, miti, matope na Tembe kama sungura au wadudu!

Umepita muheza wewe au Kabuki ukaona Aina za nyumba wanazokaa wagosi wenzetu?

Hakuna mahala Lema ametamka kuwa ndugu zake wote wa damu wanakaa kwenye magorofa! Huo Ni uwongo umeandika ! Na nyumba iliniwe nyumba Bora sio lazima iwe ya ghorofa au hukusoma sayansi kimu na maarifa ya jamii!

Kama humpendi Lema Basi chukua alichokuambia! Tunapotoka tunapata exposure na lazima tuje na mawazo mapya kuwaamsha waliolala! Nchi hii Ni tajiri tatizo Ni Sera mbovu za chama chako na serikali yako!

Kwani serikali haijui.ifanye Nini saruji na mabati viweze kununulika na wananchi? Au kwakua viongozi Wana hisa kwenye hivyo viwanda na ushirila na wamiliki wanamini kwamba cement inajengea barabara, zahanati na madaraka tu? Amka nguchiro mmoja wewe
 
..nguvu inayotumika kupotosha hotuba za Lema au kumkashifu ni ushahidi kwamba Ccm hawana majibu ya hoja zake.

..Kuna tatizo la umasikini nchini. Kitu anachofanya Lema ni kuwaelimisha wananchi waukatae umasikini.

..Jambo lingine anawaelekeza wananchi kwamba utawala mbaya wa Ccm ndio chanzo cha umasikini hapa nchini.

..Ccm wanaogopa kwamba wamachinga, bodaboda, mama ntilie, wakiamini anachokisema Lema, chama chao hakitakuwepo ktk maeneo yote ya mijini.
Observation nzuri.

Hatahivyo, zaidi ya hapo sisi wananche tuwe na mioyo ya ujasiri tukatae hila zote na propaganda za serikali ya ccm lakini pia wanasiasa wote hasioonyesha kutuamsha tutoke kwenye umasikini huu mbaya.

Watu wetu bado wanakabiliwa na umasikini uliokithiri.

Vijana hawana sehemu zakulala wanaishi stoo, walio panga kodi inawapiga chenga, na kwasababu vijana wengi hawana kazi kwahiyo wengi wanakosa lishe bora na hii inaathiri pakubwa akili za vijana.

CCM wamewapiga spell watanzania.

Mwananchi yeyote anayewashtua watanzania waone ubaya wa umasikini na wafanye maamuzi yakutoka kwenye hali mbaya walizonazo basi mwananchi huyu ni shujaa.

Binafsi nadhani kuna maeneo matatu tuhitaji kufanyia kazi.

1. Haja yakuweka msisitizo kuwafunza watu wetu elimu ya uraia ili wafahamu sera zipi za serikali ni mbaya kwao na kuzikataa lakini pia elimu iwapatie ujasiri wakutosita kufanya maamuzi pale sera, sheria au mapendekezo ya kiserikali/kisiasa yanapokuwa hayana faida kwao, hasa kiuchumi.

2. Teknolojia. Mambo mengi Tanzania yanakwama kwasababu teknolojia ipo chini sana. Kuanzia kuregister business au hata mambo madogo kufanay money transaction kutoka nje ya nchi. Tukumbatie teknolojia tupunguze process ndefu zisizo nafaida.

3. Elimu na ujuzi. Uliza hapo mtaani kwako vijana wangapi wana ujuzi wakufanya kazi fulani kwa uhakika na kulipwa pesa? Jibu ni hamna au wachache sana.

Shida hapo ni aina ya elimu.

Elimu ya Tz bado dhaifu sana. Vijana wetu hawawezi kushindana na vijana wa nchi nyingine.

Wapo dhaifu kwenye bongo zao kwasababu wamelishwa chakula/elimu dhaifu.

Shida kubwa.
 
Lema ingekuwa amezaliwa huko alikotoka halafu iwe ndo mara yake ya kwanza kufika Tanzania angetuua kwa presha kwa haya Mambo aliyoyakuta, yaani Lema wakutuona sisi tunaishi kama wadudu kweli.........!
Nimecheka sana,huyu Mmachame noma sana safari hii kazingua.
 
nmecheka sana [emoji23][emoji23][emoji23] Yani nikiwaza ulivyoongea kwa uchungu
et wadudu
Lema hajatutendea haki Mkuu[emoji1787][emoji1787],

Lema huyu tumeishi nae miaka mingi hapa, kaenda Canada miaka miwili tu amerudi na mafurushi ya masimango.....!

Ni kweli tunaishi maisha mangumu lakini akilia sisi anatuumiza badala ya kutusaidia kama anaweza.
 
Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Godbless Lema ambaye wengine hupendelea kumwita Nabii ametua jijini Tanga na kushikwa na mshangao mkuu.

Lema amesema haamini macho yake kushuhudia Watu wanaishi kwenye Magofu yaliyojengwa na waarabu nyakati za utumwa.

Lema amewataka wakazi wa Tanga kuukimbia umasikini kwa kujikomboa Kifikra kwanza kisha wakumbatie Kilimo cha kisasa.

Lema yuko kwenye ziara ya Mikutano ya nchi nzima akiwa na Viongozi mbalimbali wa Chadema.

Mungu ni Mwema wakati Wote!

FrypEqxX0AQnlpg
Kwani kwao Moshi au Canada hawapo
 
Huyu jamaa kweli amepungukiwa kichwani serikali gani inayomjengea mwananchi nyumba toka lini Serikali inachofanya ni kuhakikisha mzunguko wa pesa unapatikana mtaani ili wannachi wajishuhurishe na waboreshe maisha yao wenyewe na kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Suluhu amefanikisha hilo aache upotoshaji wananchi wasije wakahisi ni jukumu la Serikali kuwajengea nyumba
 
Elimu

Elimu

Elimu ndogo afu hana exposure
Ukweli usemwe tu.
Mji wa Tanga pamoja na Bandari na kupakana na nchi Jirani Kenya kwenda Mombasa. Ni aibu mno pamoja Juzi wamedai kutia Meli ya Kimarekani na abiria.
Nini kilichopo Kati ya Serikali Viongozi, wabunge na Wakuu wa Wilaya Tanga??
Magofu yapo ni kweli kabisa.
Bado tunataka liende Bomba la mafuta! Kweli.
Si tuanze kulitengeneza Jiji liwe na sura! Ama kweli.
 
Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Godbless Lema ambaye wengine hupendelea kumwita Nabii ametua jijini Tanga na kushikwa na mshangao mkuu.

Lema amesema haamini macho yake kushuhudia Watu wanaishi kwenye Magofu yaliyojengwa na waarabu nyakati za utumwa.

Lema amewataka wakazi wa Tanga kuukimbia umasikini kwa kujikomboa Kifikra kwanza kisha wakumbatie Kilimo cha kisasa.

Lema yuko kwenye ziara ya Mikutano ya nchi nzima akiwa na Viongozi mbalimbali wa Chadema.

Mungu ni Mwema wakati Wote!

FrypEqxX0AQnlpg
Juzi nilikuwa nasoma BBC, Kuna Kijiji huko Uingereza wanakijiji wanahangaika kumpata daktari wa kufanya kazi kituo cha afya.

Wanakijiji ni maskini bora sie wa Tanga.

Nilishangaa sana.
 
Lema ingekuwa amezaliwa huko alikotoka halafu iwe ndo mara yake ya kwanza kufika Tanzania angetuua kwa presha kwa haya Mambo aliyoyakuta, yaani Lema wakutuona sisi tunaishi kama wadudu kweli.........!

Wee jamaa umenichekesha haswa!! Yaani Lema leo anatuona sisi tunaishi kama wadudu wakati maisha yake amekulia kwenye magofu haya haya!!

Siasa ni usanii mtupu, siasa sasa imekuwa comedy🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom