DolphinT
JF-Expert Member
- Mar 9, 2016
- 2,014
- 2,979
Ndugu mwanabodi haya sio majibu sahihi ya hoja iliyoko mezani!Kwani huyo mlimbikeni kayaona Leo mpaka ajifanye kushaangaa, kama sio kejeli na ulimbukeni usio na maana? Anawasanifu wenzake wanakaa kwenyemagofu, bila hata kuwachangia ata mfuko Mumoja wa simenti hizo so kejerii?? Haya yeye tukifuatilia ndugu zake wote WA damu wanaishi kwenye magorofa?
Mtu anauekuamsha usingizini unamwitaje limbukeni?
Kukueleza ukweli kuwa unakaa kwenye magofu inabidi ukae kwenye makazi Bora unamwita Limbukeni? Angesema mtu wa CCM ungeunga mkono bila Shaka yoyote na ungesema serikali Ni sikivu na imeona matatizo ya watu wake!
Lema hawezi kuwachangia mifuko ya cement amewachangia mawazo, waiambie serikali iwe na Sera nzuri ya viwanda na biashara ili gharama ya vifaa vya ujenzi ishuke au iwe himilivu!
Serikali ije na sera Bora ya nyumba na makazi kwa.kujenga nyumba za gharama nafuu na kuziuza kwa wananchi kwa cash au mkopo kupitia shirika la nyumba!
Serikali ije na sera Bora ya kilimo, viwanda na biashara ili sekta hizo ziajiri watu wengi zaidi ili wawe na kipato Cha kuwa na makazi Bora badala ya kukaa kwenye Nyumba za nyasi, miti, matope na Tembe kama sungura au wadudu!
Umepita muheza wewe au Kabuki ukaona Aina za nyumba wanazokaa wagosi wenzetu?
Hakuna mahala Lema ametamka kuwa ndugu zake wote wa damu wanakaa kwenye magorofa! Huo Ni uwongo umeandika ! Na nyumba iliniwe nyumba Bora sio lazima iwe ya ghorofa au hukusoma sayansi kimu na maarifa ya jamii!
Kama humpendi Lema Basi chukua alichokuambia! Tunapotoka tunapata exposure na lazima tuje na mawazo mapya kuwaamsha waliolala! Nchi hii Ni tajiri tatizo Ni Sera mbovu za chama chako na serikali yako!
Kwani serikali haijui.ifanye Nini saruji na mabati viweze kununulika na wananchi? Au kwakua viongozi Wana hisa kwenye hivyo viwanda na ushirila na wamiliki wanamini kwamba cement inajengea barabara, zahanati na madaraka tu? Amka nguchiro mmoja wewe