Katika Mkutano huo wa Hadhara jijini Arusha Gobless Lema amedokeza kuwa wapo baadhi ya Viongozi wa Serikali wanamtulana Rais Samia. Akifafanua jambo hilo Lema anasema:
"Natoa maelekezo kwa Viongozi wa Kanda na Makatibu Rais Samia yupo Arusha apewe Kadi ya CHADEMA. Anatukanwa na wakina Mwigulu, Kina January, Majaliwa, Ummy Mwalimu, Mawaziri wote wanamtukana Rais jamani.
"Anaenda wapi yule Mama wa watu, wanamtukanaje Mimi Sijui lakini wanamtukana."
Nimesikia hayo majina na nasubiri kusikia kama watamkamata Lema au watamtaka atoe ushahidi ingawa kawa mjanja kwa kutaja wachache akimanisha mawaziri wote.
Mmmhhhh...!!! Hili nalo ni kuangalia kwa jicho la ndani zaidi, usikute ni kumchonganisha Mkuu wa nchi na wasaidizi wake wa karibu, sio jambo la kukurupuka, vyombo vipo vifanye kazi yake