Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Yeah hasikiki sana akisisitiza hilo. Sasa hivi tutaanza kwenda wenyewe kwa viongozi wa dini kuombewa kama dogo Bashite.[emoji13]
Mleta mada ameleta Jambo la msingi lijadiliwe kwa manufaa ya wengi, Wazandiki Kama wewe na wenzako mnakuja na UZANDIKI wenu kama kawaida. Anzisheni Uzi ili mjadili yenu huko mkuu.
 
Naona kuna ukweli maana kadri siku zinavyoenda jamaa ndiyo anazidi kuwa na chuki za kutisha sana, pamoja na kicheko chake cha kinafiki anapokuwa hadharani.
Aige mfano kwa lowassa yule ndo mwanasiasa anaejua siasa
 
Akisha jibu ile kesi ya ndoto, then nitatoa maoni yangu kama kuna mtu anakutakia kifo afu we umpende tuu eti utaenda peponi!!
 
Naona mapito ya Lema yanaendelea kumuimarisha na kumjaza hekima siku hadi siku
 
Tunakoelekea sasa ni kubaya sana, ni wakati wa maraisi wastaafu na viongozi wa dini kusema 'kitu'
 
Mheshimiwa Lema ameongea maneno katika vitabu vyote vya dini watu wameamrishwa kuishi kwa wema hata na wasio kupenda, japo father mjengo yeye hataki watu waishi kwa umoja kama muasisi wa taifa alivyokuwa kuwa anahubiri. Kinachoonekana yeye anachukulia kama upinzani ni uadui anasahau kama nje haiwezi kwenda bila ya upinzani, maana kama hutaki kukoselewa basi wewe unajipa sifa za mungu, ndiye ambaye hakosei peke yake.
Mungu ibariki tanzania na utulinde na watawala madhalimu.
 
Mna wakati mgumu sana upinzani safari hii msipo simama pamoja na kuweka tofauti zenu pembeni sijui hali itakuwaje
Be specific upinzani upi unaomaanisha huoni hata wewe ni mpinzani kwa mada iliyopo mezani, ndani ya kanisa la anglikani kuna upinzani(Mokiwa Vs cheme...), CCM kuna upinzani (Bashe, Msukuma, ... Vs Mwenyekiti) na nyingine nyingi, Sasa wewe unamanisha Upinzani upi?
 
Ndio mana tuliaamini lema aliwekwa mahabusu kwa amr ya rais
 
Anapenda kukaa kisongo kuliko kukaa jimboni kuwahudumia wananchi. Na mwisho wa siku anatafuta kura za huruma alipwe kwa ajili ya kukaa kisongo kuliko kura za asante kwa kazi njema ya maendeleo jimboni. Waarusha badilikeni.
 
Na upinzani munawajibu wa kuhubiri haya uliyoyasema kwa wanachama wa wapenzi wenu, Chadema mna wanachama na wapenzi wenye chuki kwa serikali na dola kwaujumla. Kila mmoja anamuhitaji wenzake kwa njia moja au nyingine.

Dodoma hivi majuzi wamempiga mpita njia kwakua alikua ktk gari ya chama nani kiongozi wa upinzani hapakua na sababu yoyote ile zaidi ya kujipitia pale, je ni wanachama wangapi wamedhuriwa na hawa wapinzani hata useme chadema ina wanachama wenye chuki na serikali na dola? sijakuelewa samahani nifungue macho ili tujue hawa wapinzani ni maditecta na magaidi tu.
 
Anapenda kukaa kisongo kuliko kukaa jimboni kuwahudumia wananchi. Na mwisho wa siku anatafuta kura za huruma alipwe kwa ajili ya kukaa kisongo kuliko kura za asante kwa kazi njema ya maendeleo jimboni. Waarusha badilikeni.

Tujuze aliomba au alituma maombi wapi ili aende kisongo? alafu ilikuaje majaji wakaona hakuna sababu ya lema kushikiliwa pale pasipo dhamana?
 
Mhe Lema tunakuombea upite salama katika majaribu yote haya na tunamwombea sana sizonje mwenyezi Mungu amjaze busara. Hana busara. Mhe Lema ninyi tunawaamini kama kambi na viongozi wa upinzani kuongoza harakati za kudai TUME HURU YA UCHAGUZI. Tusahau mambo ya KATIBA MPYA YA WANANCHI - hiyo ni ndoto ya mchana katika enzi za usizonje. Lakini madai ya tume huru ya uchaguzi ni jambo linalowezekana - hata tukishindwa lakini tutakuwa tumeitangazia jumuiya ya kimataifa wapi hili taifa lilipo na linaelekea wapi. Ni lazima tupige kelele na viongozi ndio nyie. Tusipopata tume huru ya uchaguzi kabla ya 2020, basi tuombe kutokuwepo uchaguzi - tumwache sizonje na ccm yake watawale milele.
 
Asante Simba wa Yudah
 
Excellent! Lakini rais pia alikwenda hospitali kumtembelea Sumaye wakati amelazwa kule. Je nao ni usaliti kwa chama chake? Kana kwamba kama hiyo haitoshi alikutana pia na Lowassa kwenye Jubilei ya miaka 50 ya ndoa ya Mkapa na mkewe na wakasalimiana na kunong'ona kidogo. Je huo nao ni usaliti kwa chama chake? Rais pia amekuwa anakwenda kusali katika madhehebu tofauti na dhehebu lake. Je huo na ni usaliti kwa dhehebu lake?! Ni kwanini rais anahubiri chuki badala ya utangamano? Kwanini tusiamini kuwa yeye ni rais wa ajabu kwa haya anayoyasema? Kama ni usaliti basi yeye ndio atakuwa msaliti namba moja kwa chama chake kuliko hao wabunge. Tatizo lake anaona kibanzi kwenye macho ya wenzake wakati yakwake yote mawili yana boriti
 
Alihitaji faraja.....!! Wewe ulikwenda kufarijiana?
ilikua sio lazima kila mtu aende na thread aiuliziii mauzurio soma uelewe. imesema kwa alie na nafasi na kama huelewi nenda kachukue cheti chako kolomije kilaza wewe siku nyingine usikurupuke kujibu usichoelewa
 
Lema Sasa jikite kwenye maendeleo, ninaamini watu hawataendelea kukuchagua kwa jina lako tu.
 

Wala nisiende mbali, chuki sio kupigana makonde tuu, chuki ipo hata kwenye matamshi ya mtu. Lema aliposema utapata baraka kwa Mungu ukimzomea Lowassa. Wewe kwa mtazamoa wako yale maneno yalikuwa ni chuki, kejeli, utovu wa nidhamu au labda kwa mtazamo wa upinzani ule ulikuwa ni ujasiri? kauli nyingi za upinzani zimejazwa chuki ambazo ukiwauliza ni za nini, wanakosa majibu. Hivi, mtu mwenye akili timamu anaweza kusimama hadharani ukasema nimeota mtu fulani atakufa?, unaweza kutumia kauli hiyo kwa mtoto aliye mzaa? au unaweza kuwaambia wanafamilia nimeota baba yetu atakufa? kama sio chuki ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…