Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Binafsi sijafurahishwa na kauli za mtukufu JPM dhidi ya wabunge wa CCM walio kwenda kumtembelea lema kipindi yupo Kisongo. Mtukufu JPM amewaita wabunge hao 'wasaliti'. Hii ni kauli ya kulipasua taifa.

Lakini tujiulize je hii ndio mara ya kwanza kwa Mtukufu kuongea wazi wazi kauli za chuki dhidi ya wapinzani? La hasha, nakumbuka mwaka 2016 septemba Rais JPM akiwahutubia wananchi wa Zanzibar alitamka wazi wazi kuwa Anamshangaa sana Rais wa ZNZ anasaini makaratasi ya mtu aliyekataa kumpa mkono siku ya mazishi ya Jumbe, na kusema kwake isingekua rahisi hivyo.

Kwa kutizama kauli hizi unaweza ukajiuliza je Rais anafikiria nini kichwani kuhusu watu walio na Kabila au Dini tofauti na yake?

Kwa sasa tunaweza tukaona ni kauli za kisiasa na kupita tu, lakini naamini ipo siku Mtukufu anaweza kusema jambo juu ya Wasukuma dhidi ya makabila mengine au wakristo dhidi ya dini zingine, Jambo ambalo litadumu katika vichwa vyetu Milele yote na kuvuruga Maana ya Utanzania wetu.

Inasikitisha Rais anaposhindwa kutambua kua yeye kama Mtanzania Namba moja hapaswi kututizama wananchi wake katika mizania ya U Ccm na U pinzani, Raisi anapaswa kuelewa/kukumbushwa kuwa Kabla ya U ccm au U pinzani wetu sisi ni WATANZANIA, kabla ya kumtizama lema kama mwana chadema unapaswa kumtizama kama mtanzania.
Unapoomba kuombewa na wananchi huwa husema naomba wana Ccm mniombee, bali huwa unaomba watanzania wote

Mtukufu JPM unapaswa kuzitafakari sana kauli zako kabla hujalitenganisha Taifa.

Mapenzi ya Chama yasizidi mapenzi ya Taifa.

Nadhani gazeti la Mwananchi wanatakiwa kuthibitisha walicho andika katika hii habari.
 
Maneno ya Baba wa Taifa.

Kazi ya uongozi ni kujenga watu wawe kitu kimoja. Kazi ya uongozi si kutenga watu waliokuwa na umoja wawe mbali mbali. Na hasa mahali ambapo bado hamjakomaa bado mpo katika jitihada za kujenga wakianza viongozi wa namna hiyo na tukawakubalia tutagawanyika.

Lakini baadhi ya Watanzania wanadhani Lema na Tundu Lissu na CHADEMA ndio wachochezi. Wanashindwa kuona kauli zote hizi kuwa zina hatari kubwa kwa taifa letu. Tuache unafiki na ushabiki, yamkini tutapona. Ama sivyo tutageuka Taifa la kijinga sana kwa hayo yatakayojiri muda si mrefu
 
Kutokana na hofu kubwa tuliyonayo watanzania, basi hata JF haikupona sababu tunapo paza sauti zetu kulalamika juu ya jambo flani, matokea yake uzi huo ama unafutwa ama unaunganishwa na uzi mwingine hata kama nia ya mleta mada inatofautiana na mada iliyopita.

Lengo langu leo ni kuanzisha mjadala kuhusu kauli za Rais ambazo zinatugawa ktk misingi ya itikadi za vyama. Rais anataka hata wabunge wa CCM wasishirikiane hata ktk matatizo. Mbunge wa chama kimoja akiwekwa mahabusu, basi mbunge wa chama kingine asiende kumpa pole.

Je huu siyo uchochezi? Je tufanyeje basi?
 
Kwani yeye ni Dini gani. Nachelea kusema dini yake imemlea katika mafundisho ya chuki, visasi na jazba.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu mie sidhani kama ana dini huyu. Haiwezekani mtu mwenye dini na kusikiliza mawaidha ya upendo miongoni mwa wanadamu yanayotolewa na mapadri na yaliyomo kwenye biblia anaweza kuwa na chuki za kutisha, roho mbaya na visasi vya kutisha kiasi hiki. Kwenda kanisani ni unafiki tu wa kutuzuga Watanzania.

Kwani yeye ni Dini gani. Nachelea kusema dini yake imemlea katika mafundisho ya chuki, visasi na jazba.
 
Hakuna uarafiki hapo nyote wawili mkishika vipaza,ni ma mc wazuri wa kuhubiri chuki!
 
Sidhani Kama sizonje Hana ubinadamu kiasi hicho,ila hajiamin yeye Na serikali yake hivyo Kila mkusanyiko anahisi unamjadili Na kumkosoa..

Mh.lema huku mtaani hali Ni mbaya maana wananchi wanakamatwa hovyohovyo kisa kuijadili serikali..!

No democracy, no peace , tunaishi Kama tuko ukimbizini
 
Kwa nionavyo mm naona viongoz wetu wanakosa karama ya uongoz kabisa, hawajiamn na nafasi zao walizonazo,

Sahivi kumekuwa na wanaccm na wapinzani wakat uchaguz umeisha 2015 na sasa ss ni watanzania je tukiishi kwa itkad ya vyama tunaelekea wapi?

Hii nchi iwe yawanaccm na wengne ni maadui? Nani analeta haya yaliyokataliwa na MWL Nyerere? Uongozi sio kaz ndogo maana kile unachokisema,kuwaza kina impact 100% kwa umma hivyo viongoz chungeni kauli zenu Tanzania ni nchi yenye amani na hatuna udin,uchama nk,

Fanyen kaz ya kutuunganisha watanzania na sio kutugawa,kwani mnapotugawa mnahatalisha amani na umoja wetu, viongoz tumieni hekima nasio ubabe,chuki,Visasi,kiburi nk,
 
Dah inakatisha sana tamaa.
Mtu ambaye kila siku anasisitiza watu wamuombee halafu anaonyesha ubaguzi dhahiri,sijui ni mtu wa aina gani.
Labda anataka tumuombee ili awe na roho mbaya
 
Dah inakatisha sana tamaa.
Mtu ambaye kila siku anasisitiza watu wamuombee halafu anaonyesha ubaguzi dhahiri,sijui ni mtu wa aina gani.
Labda anataka tumuombee ili awe na roho mbaya
Siku hizi mbona ameacha[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ameacha kusisitiza watu kumuombea?
Yeah hasikiki sana akisisitiza hilo. Sasa hivi tutaanza kwenda wenyewe kwa viongozi wa dini kuombewa kama dogo Bashite.[emoji13]
 
Halafu kuna wapuuzi kibao hadi viongozi wa dini wamo katika hao wapuuzi wanatuambia ni chaguo la Mungu!!
 
Kwa nionavyo mm naona viongoz wetu wanakosa karama ya uongoz kabisa, hawajiamn na nafasi zao walizonazo,

Sahivi kumekuwa na wanaccm na wapinzani wakat uchaguz umeisha 2015 na sasa ss ni watanzania je tukiishi kwa itkad ya vyama tunaelekea wapi?

Hii nchi iwe yawanaccm na wengne ni maadui? Nani analeta haya yaliyokataliwa na MWL Nyerere? Uongozi sio kaz ndogo maana kile unachokisema,kuwaza kina impact 100% kwa umma hivyo viongoz chungeni kauli zenu Tanzania ni nchi yenye amani na hatuna udin,uchama nk,

Fanyen kaz ya kutuunganisha watanzania na sio kutugawa,kwani mnapotugawa mnahatalisha amani na umoja wetu, viongoz tumieni hekima nasio ubabe,chuki,Visasi,kiburi nk,
That's another fake thread from a fake member for the fake intention
 
Nilishasema na nitasema.. kukosekana kwa busara kwa mkulu.. kutasababisha makundi na udui kati ya wananchi. Hii inahatarisha umoja..wa nchi yetu
 
Ndio maana mfalme Suleiman aliomba Mwenyezi Mungu ampe hekima.
 
......
......ukiongea na LEMA unaongea na Watanzania

Ndio maana yake na ni vyema kila mtu alifahamu hilo. Nchi hii imepiganiwa,kulindwa na kutunzwa mpaka kufika hapa tulipo ambapo mtoto wa masikini anaweza kuwa mbunge kwa kupigiwa kura tu kwenye boksi lakini bado watu wanaweza kukashifu na kubeza juhudi hizo
 
Mimi ni mwananchi huru nikiwa na maana sijajiunga na chama cha siasa ila nafuatilia sana mwenendo wa vyama na siasa zake. Kiukweli kauli aliyoitoa m/Kiti wa CCM Taifa ya kuimarisha uhasama na chuki dhidi ya wanachama wa vyama vinavyopingana na serikali imenishangaza sana kwa kuwa pamoja na nafasi yake ya uanachama yeye pia ni RAIS wa wananchi wote wa Tanzania yetu ambapo ana jukumu la kutuunganisha wote kama Taifa bila kujali itikadi za kisiasa kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu. Sijui kwa nini Rais wetu anaonyesha chuki waziwazi kwa wananchi jambo ambalo wote wenye busara na utu hawawezi kushangilia jambo hilo. Je, ina maana awamu hii tunaongozwa na Rais asiyekuwa na dini? Na kama anayo je ni dini na mungu yupi anayeagiza watu kuimarisha uadui na chuki kati ya mtu na mtu? Mimi ninavyojua hata kama ni timu ya mpira haiwezi kuonekana ubora wake endapo hakuna timu pinzani halafu waonyeshe ufundi wao wa kucheza. Vivyo hivyo siasa..chama tawala hakiwezi kutuonyesha ubora wa utendaji wake na hakitaweza kuwa na juhudi za ziada kwa kuwatumikia wananchi bila kuwepo uponzani tena wenye nguvu. Pia kwa KIONGOZI bora atakuwa anawatumia wapinzani wake kuboresha utendaji wake pale wanakopakosoa na si kukasirika na kuwaona ni adui zake..WAPINZANI NI KIOO CHA KUJIANGALIA KWA WATAWALA. Mbona hata Rais wetu mstaafu juzijuzi tu alisema wazi kuwa upinzani wa kisiasa si uadui? Na hilo alimwambia mbunge wa Chalinze (CCM) pale alipomwona akisalimiana na kuongea na KIONGOZI mmojawapo wa upinzani. Je Raid wetu Magufuli anataka kutuaminikisha kuwa Mh. Kikwete naye na huyo mbunge wa Chalinze ni wasaliti wa CCM? Au tuamini kuwa raid wetu ni mnafiki pale anapomsifia 'MZEE KIKWETE?' Rais ameshatufanya tumwangaliye kwa jicho la tatu
 
Back
Top Bottom