Binafsi sijafurahishwa na kauli za mtukufu JPM dhidi ya wabunge wa CCM walio kwenda kumtembelea lema kipindi yupo Kisongo. Mtukufu JPM amewaita wabunge hao 'wasaliti'. Hii ni kauli ya kulipasua taifa.
Lakini tujiulize je hii ndio mara ya kwanza kwa Mtukufu kuongea wazi wazi kauli za chuki dhidi ya wapinzani? La hasha, nakumbuka mwaka 2016 septemba Rais JPM akiwahutubia wananchi wa Zanzibar alitamka wazi wazi kuwa Anamshangaa sana Rais wa ZNZ anasaini makaratasi ya mtu aliyekataa kumpa mkono siku ya mazishi ya Jumbe, na kusema kwake isingekua rahisi hivyo.
Kwa kutizama kauli hizi unaweza ukajiuliza je Rais anafikiria nini kichwani kuhusu watu walio na Kabila au Dini tofauti na yake?
Kwa sasa tunaweza tukaona ni kauli za kisiasa na kupita tu, lakini naamini ipo siku Mtukufu anaweza kusema jambo juu ya Wasukuma dhidi ya makabila mengine au wakristo dhidi ya dini zingine, Jambo ambalo litadumu katika vichwa vyetu Milele yote na kuvuruga Maana ya Utanzania wetu.
Inasikitisha Rais anaposhindwa kutambua kua yeye kama Mtanzania Namba moja hapaswi kututizama wananchi wake katika mizania ya U Ccm na U pinzani, Raisi anapaswa kuelewa/kukumbushwa kuwa Kabla ya U ccm au U pinzani wetu sisi ni WATANZANIA, kabla ya kumtizama lema kama mwana chadema unapaswa kumtizama kama mtanzania.
Unapoomba kuombewa na wananchi huwa husema naomba wana Ccm mniombee, bali huwa unaomba watanzania wote
Mtukufu JPM unapaswa kuzitafakari sana kauli zako kabla hujalitenganisha Taifa.
Mapenzi ya Chama yasizidi mapenzi ya Taifa.
Nadhani gazeti la Mwananchi wanatakiwa kuthibitisha walicho andika katika hii habari.