Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Ingieni mtaani kama walivyofanya Waarabu na Arab spring yao.

Au mnaogopa virungu?

Oh wait...UKUTA ulimomonyoka😀
 
Ni bahati nzuri Katiba yetu kwa asilimia kubwa mambo ya msingi yamezungumzwa ikiwemo unalosema la uhuru wa kufanya siasa. Lkn viongozi wengi wa Kiafrika wakiwemo wa Tanzania wamekuwa wakikandamiza vyama vya upinzani kwa kutumia dola, pia mihimili mingine haina uhuru wao binafsi kufanya maamuzi.
 
Lendila ndugu yangu pole sana, sie labda hatuna hata hiyo katiba yenyewe kwani haiwezekani I we inavunjwa kiasi hiki mie nikikuwa sijui kama katiba tunayo na imeandikwa hivyo,Duu.
 
Nashangaa Lema na wewe umegeuka kuwa mtu wa kulia lia kama msichana sikunhizi.Wakati zamani ulikuwa kamanda.Kuna vijana wa kazi wapo wengi tu mtaani wameshajikatia tamaa wakipewa maelekezo wanapiga kazi.Sasa badala ya kuwatafuta unalialia tu
 
Leo naona umeanza na salamu siyo matusi tena na kejeli zile....hakika selo haijawahi mwacha mtu salama. Umekuwa mtiifu kweli.
 
Huo ndio ukweli, kwa Tanzania ukiwa mpinzani serikali ya CCM wanakuona wewe ni zaidi ya shetani. Watakuchukia, watakusema vibaya, watakupa kibano na hata pengine kukudhuru kabisa.

Kuwa mpinzani kwa nchi kama ya tanzania ni kuhatarisha maisha yako na kuyaweka katika risk kubwa ya kuyapoteza.

Ni vema kujifanya mjinga ili siku zipite, vinginevyo uingie katika siasa za kipinzani huku ukiwa umesha wajengea misingi ya maisha wategemezi wako kama watoto na wazazi. Vinginevyo unaweza kuwaacha watoto wako pasipo kuwajengea misingi ya kimasha

Wanaccm wanavyomwona mpinzani wanatamani wakuchome moto kabisa upotee mbali huko
 
Ukweli kabisa hata mimi ukinipinga hovyo bila hoja nakuona Zimwi.
 
Ujifanye mjinga siku zipite halafu matatizo aje kurithi mtoto wako, wajukuu zako na kizazi kijacjo siyo? Miafrika bhana! We unafikriia urefu wa pua yako tu! Si afadhali basi ungesema turudi kwenye system ya chama kimoja kulio kusema tkae wajinga?
 
Mawazo ya kihuni yanakera,kama haya ya kulazimishana kuingia msituni.
Ukimsoma Lema vizuri ktk uzi huu anamshauri Rais kufuata taratibu za Urais kama taasisi. Ili awe kiongozi na si mtawala mwenye hofu na nafasi yake . Ukiwa kiongozi raha lakini mtawala ni hofu.

NAAMINI UTANIELEWA
 
Ukimsoma Lema vizuri ktk uzi huu anamshauri Rais kufuata taratibu za Urais kama taasisi. Ili awe kiongozi na si mtawala mwenye hofu na nafasi yake . Ukiwa kiongozi raha lakini mtawala ni hofu.

NAAMINI UTANIELEWA
Mimi nilikuwa naujibu uzi mwingine kabisa nadhani umeunganishwa na huo wa Lems.
 
Nimepata taarifa mh.Halima mdee kakamatwa na dhamana kanyimwa Leo hii! Huku ni kumchonganisha Rais na wananchi .

Sio wote wanaofurahi huu ukandamizwaji dhidi ya wapinzani kwa makosa ya kusingiziwa kama uchochezi na kisha kukosa dhamani

Tangu nakua na kupata akili nimeona fair play katika uwanja wa kisiasa nchini.

Lakini kwa hili watanzania tuseme inatosha wanatuharibia nchi hawa.

Juzi sugu Leo mdee!

Kwa pamoja tuseme sasa inatosha na tuchukue hatua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angeona anachonganishwa angekemea
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natoa tu angalizo kwamba siasa siyo uadui.

Siasa ni sayansi.

Watanzania tuvumiliane wapinzani siyo malaika wala CCM siyo malaika mkuu vyama vyote ni vya wanadamu.

Mungu wa mbinguni awabariki.

Maendeleo hayana vyama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…