Lema: Narudi Tanzania

Lema: Narudi Tanzania

‘’Tanzania ni nchi inayoheshimu utawala wa sheria.’’alisema msemaji wa serikali Dokta Hassan Abbas.
Eeenh Heee,
Msemaji wa serikali Comical Abbas!

Huyo akikwambia jambo lolote ni muhimu ukatafute ukweli juu ya jambo hilo mahali kwingine.

Hivi anayo PhD ya uongo na mipasho? Kuna vyuo vinavyotoa taaluma hiyo?
 
Godbless Lema asema anafikiria kurudi nyumbani Tanzania
Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambaye alikimbilia ughaibuni kwa madai ya wasiwasi wa usalama wake mara baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020 anafikiria kurudi nchini Tanzania.

Baada ya kifo cha Rais Magufuli Lema anatarajia kuona uongozi wa Rais Samia ukirekebisha na kutafuta maridhiano ya taifa zima.

‘’Nataka kurudi nyumbani hata leo, nyumbani ni nyumbani tu, wakati nakimbia nyumbani nilishuhudia uzoefu mbaya mimi na familia yangu’’, alisema

Lema ameeleza kuwa mabadiliko ya mifumo ya kiutawala ikiwemo viongozi watakaojali haki ni sura itakayorejesha imani ya kwamba sasa maisha yako salama.

‘’Nitarudi nyumbani mapema sana kuendelea na mapambano. Uwepo wetu huku hauna maana ya kwamba tumekuja kula bata, hakuna maisha yoyote, mtu anaweza akakimbia nyumbani kwao ambako amejijenga vizuri.’’alisisitiza

Hata hivyo Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ilitupilia mbali madai hayo ya upinzani na kusema hayo ni maigizo ya upinzani.

‘’Tanzania ni nchi inayoheshimu utawala wa sheria.’’alisema msemaji wa serikali Dokta Hassan Abbas.

Samia Suluhu Hassan ameapishwa leo jijini Dar es salaam kuongoza awamu ya sita ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kifo cha mtangulizi wake John Pombe Magufuli.




https://t.co/4ZC5OwVwiq https://t.co/j2CDmIdCg9
Kama ukirudi fanya na biashara halali na kulipa kodi yetu la sivyo baki hukohuko kwenu.
 
Hivi mbona Bobi Wine huwa haondoki nchini kwake? au yeye hana tishio kama hawa wananzengo..
 
Lema! aliyetangulia ni magufuli na hakuwa na shida na wewe,hapa ni nyumbani rudi ukiendeleza yaleyale wananchi tupo tusiotaka maziombwe nchi lzm isogee.
 
Lema you are long done friend. Wewe una mawazo mgando sana yaani unaamini kuna mtu anakuwaza ndani ya chadema? au serikalini au CCM? you are wrong my ndugu. Fungua duka la spea hapo toronto kwani kuna shida
 
Back
Top Bottom