PreGE2025 Lema: Simba na Yanga zinanikera, namuomba Mungu aziondoe mara moja

PreGE2025 Lema: Simba na Yanga zinanikera, namuomba Mungu aziondoe mara moja

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mbona malalamiko yalikuwa ni mengi ya kwamba aliua upinzani kupitia nguvu na wala si demokrasia!, vilevile amekuwa akishutumiwa juu ya matukio ya upotevu wa wanasiasa wa mlengo pinzani!, wewe wafikiria nini..?
Hayo ni maoni tu kama yalivyo yangu.
 
Magufuli alibadilisha siasa za Tanzania. Tutake tusitake.

Alifanikiwa kubadilisha mitazamo ya watu wengi saana. Na kufubaa kwa upinzani ni matokeo ya Kukubalika kwa Magufuli.

Huu ni mtizamo wangu.....
Upinzani umefubaa wapi bablai? Kama upunzani umefubaa kwanini ccm inatumia nguvu kubwa kuwanyamazisha?

Najua unajua ccm haina appeal yoyote kwa raia na ndio maana wanajaribu kutumia mbinu zote chafu kunyamazisha upinzani. Hizo kampeni za mama kila kitu mama ni zakumfanya aonekane anakubalika lakini in reality hamna tena mvuto. Wana force tu.

Nakushangaa ukisema upinzani umefubaa. Ungetakiwa kusema upinzani umekuwa repressed.
 
Upinzani umefubaa.....
Binafsi naona mnajicha nyuma ya police brutality na CCM tu.

Miaka ya 2010-2016 CCM ilikuwepo na police ilikuwepo. Viwanja vilijaa mashabiki wa upinzani waliokuwa tayari kufia chama. Sitaki kuamini police waliowaua kina Mwangosi lakini bado watu wakaingia barabarani ndiyo hii polisi ya Leo.

Angalia mikutano ya Lema ya Arusha ya enzi zile na yasasa anayosimama juu ya meza anajiongelesha mwenyewe tu.
 
Ukitaka kutawala wa raha lqzima ubuni kitu kitakacho waondolea kufikiri na badala yake wachekelee na kuona mambo sawa.

Hata kwenye familia baba katili mfanye mkeo na watoto wako madondocha utaishi kwa raha mno - hawatauliza chochote utakachosema ndicho hicho hicho.
Wanyime elimu watoto ili how na why siziwepo kisha mkeo mfungulie ngenge ili ashinde huko sokoni. Utaishi kwa raha.
Hawa ndiyo CCM, vijana wamegeuka boda, chawa, kubet, mishangazi na kubet ma mioira mabinti nao kutafuta mijibaba ya kuwalea

Siku zinasonga!!
 
Upinzani umefubaa.....
Binafsi naona mnajicha nyuma ya police brutality na CCM tu.

Miaka ya 2010-2016 CCM ilikuwepo na police ilikuwepo. Viwanja vilijaa mashabiki wa upinzani waliokuwa tayari kufia chama. Sitaki kuamini police waliowaua kina Mwangosi lakini bado watu wakaingia barabarani ndiyo hii polisi ya Leo.

Angalia mikutano ya Lema ya Arusha ya enzi zile na yasasa anayosimama juu ya meza anajiongelesha mwenyewe tu.
Acha unazi mzee.
 
Mfanyakazi mwenyewe ndio mimi hapa .
Tutakutana ofisini ndugu yangu haina shida 😌 . Nashukuru kujua ID

Ukweli mchungu Ila hizi timu zinawafanya Watanzania kuzidi kuwa wajinga

Hakuna tofauti ya mtanzania mwenye degree na ambaye hajui kusoma

Kuna siku nilikuwa nabishana jamaa mmoja namwambia hizi timu CCM anazitumia kutawala bila usumbufu!!

90% ya mashabiki wa hizi timu ni wajinga

Juzi tena Kuna mfanyakazi wangu anaomba ruhusa kwa mkuu wake eti akaangalie mechi ya Simba na almasry nilicheka Sana yaani uondoke kazini muda wa kazi kisa kwenda kwenye mpira?

Huu ukweli Lema kaongea hizi timu zingefutika au kuacha kubebwa soka la Tanzania lingeenda mbali Sana!!

Uchawa wote uanzia kwenye hizi timu
Kama ni shabiki kindakindaki basi kazi yenyewe aliifanya shingo upande na kile tusi la k-nyok- aliwapiga kimoyomoyo kwa kila dakika ya mechi yaani mara 90
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ameendelea kusema kiwa wakazi wa Dar es Salaam wamekuwa nyuma katika harakati za kudai mabadiliko na badala yake wanayapa kipaumbele mambo yasiyokuwa na maana ikiwemo ushabiki wa mpira wa miguu hususan kwa timu za Simba na Yanga.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Alianza na bodaboda
 
Wakwepa kodi wengi pia wamejificha katika kufadhili mpira.
 
We can chew gum and walk.

Mbona Uingereza wana ushabiki wa mpira mpaka football hooliganism, na bado kwenye kuwekana sawa serikalini wanawekana sawa vizuri tu?

Lema alitakiwa kujua kujipenyeza kwenye kitu kinachopendwa na watu na kukitumia kwa faida ya ajenda yake. Si kutaka kubomoa ushabiki wa mpira ambao una mizizi mirefu kuanzia kabla hata ya uhuru.

Nyerere hakuwa mpenzi wa mpira, michezo pekee aliyocheza ni darts, bao na pool. Lakini alielewa umuhimu wa kutumia klabu za michezo kwenye harakati za TANU.

Na hapo ndipo CCM inapovishinda hivi vyama vya upinzani.

Kwenye vitabu vya Shivji na wenzake kuna sehemu wameandika jinsi Nyerere alivyopewa ushauri na washauri wake wa siasa kwamba maduka yote yataifishwe, hata maduka madogo ya Uswahilini. Huo ulikuwa ushauri wa wasomi wa uchumi. Lakini Nyerere akautafakari ushauri huo, akaona apate mawazo zaidi. Akamtafuta Mzee mmoja wa Yanga aliyekuwa CCM anaitwa Tabu Mangala. Nyerere akamuuliza Mzee Tabu Mangala, vipi, tutaifishe maduka ya watu ya Uswahilini? Mzee Tabu Mangala akasema chonde chonde Baba usifanye hivyo, hao wasomi hawajui tunavyoishi Uswahilini, sisi ndio tunajua.

Hapo utaona klabu ya Yanga ilitumika kama sehemu ya CCM na serikali kupata habari za chini kabisa jwa wananchi. Na Nyerere alijuwa na washauri wake rasmi wa uchuni, lakini pia alitumia wazee wa CCM waliokuwa kwenye hizi klabu kujua wananchi wanataka nini. Mwishowe Nyerere aliuacha ushauri wa washauri wake wasomi, akaufuata ushauri wa Mzee Tabu Mangala.

You are not supposed to alienate the people you are fighting for.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ameendelea kusema kiwa wakazi wa Dar es Salaam wamekuwa nyuma katika harakati za kudai mabadiliko na badala yake wanayapa kipaumbele mambo yasiyokuwa na maana ikiwemo ushabiki wa mpira wa miguu hususan kwa timu za Simba na Yanga.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Huyu mwizi wa magari naye akamatwe haraka, pumbavu sana huyu.
 
Tafuteni namna ya kuwashawishi watu sio mnakuwa na mood swings kama mnamimba.

Kulala kwa hadhira ni uzembe wa fanani. Miaka ya nyuma Arusha tulikuwa tayari kufa kwa ajili ya chadema leo hii hayo mapenzi yamepotea....jitathminini
Uko sahihi kabisa kuanza kulalamikia sababu ni mpira ndo maana watu hawataki mabadiliko ni upumbavu na kukubali wamefeli kushawishi watu. huko misri kuna team kali sana za mpira kama zamalek lakin watu wakiamua kukiwasha wanakiwasha.Nchi zingine nyingi tu kama uingereza watu wana wazim na soka ila wakiamua kuingia mtaani wanaingia.Lazima akina Lema wakubali watu bado hawana imani nao so wanachagua kuishi kwa amani kuliko kuwa nyuma ya wachumia tumbo.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ameendelea kusema kiwa wakazi wa Dar es Salaam wamekuwa nyuma katika harakati za kudai mabadiliko na badala yake wanayapa kipaumbele mambo yasiyokuwa na maana ikiwemo ushabiki wa mpira wa miguu hususan kwa timu za Simba na Yanga.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Haw watu wa UPINZANI wapo katika makundi makuu matano
1. MANABII. Hawa watu wa maonyo. Wanaonya kuhusu hatari inayomkabili mtu, kiongozi, serikali, na na utwala. Mifano ya watu Hawa ni Lema, Lissu, . Hawa huwa wanaongea ukweli wa mambo yalivyo bila kujali watu wangapi wanalioenda au hawalioendi Hilo jambo! Mfano mzuri hili la Lema kusema hapendi mpira na Simba na Yanga . Tunajua Namna gani mpira unapendwa na watanzania.
 
Back
Top Bottom