Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,322
- 3,648
Katika zama hizi za kutekwa,kuuawa na kupotea kwa watu,Godbless Lema anasema tuwe watu wa amani sababu dawa ya muovu ni kuwa mtu wa amani kama Zito Kabwe alivyo mtu wa amani kwa Serikali ya sasa ambayo ilisababisha mauaji ya Oktoba 29,2025.Godbless Lema anasema wananchi waanzishe nguvu ya Umma kwa amani ila yeye hawezi kuwa sehemu ya hiyo nguvu ya Umma sababu yeye ni kiongozi wa Chadema akiwa sehemu ya nguvu ya Umma basi Chadema itafutwa,Gobless Lema anasema familia yake mke na watoto wake sasa ni raia wa Canada,na Canada ni sehemu nzuri ya kuishi maana kuna watu wema sana.Godbless Lema amesema tusiwasikilize kina Mange Kimambi na Maria Sarungi,hao ni wanaharakati wapotoshaji,amegusia tena,yeye Godbless Lema alipotaka kurudi Tanzania aliongea na Jakaya akasema Magufuli amekufa naomba nirudi Tanzania,alifurahi sana Mama alivyokuwa Rais,amesema watu wakimsema sana atang'atuka Chadema aende akafanye biashara zake kama Freeman Mbowe.Ahsante.