Lema umeamua kuwasaidia CCM kwenye propaganda ya kukigawa chama?

Wewe sasa umenielewa vzr sana. Nilitamani niandike kwa urefu lkn mm ni mvivu wa kuandika.

Kwa sasa Chadema Iko sehemu nzuri sana wananchi wanaikubali na kuiunga mkono vibaya mnooo....! Wasiruhusu kabisa kuwapa CCM propaganda za kuwapa unafuu. Huu uzushi kama Chadema wasipoupa usurious utakipa chama msuko suko mkubwa sana. Maana inavyooneka serikali ya Samia imeshatenga fedha za kutosha kuhakikisha inamung'oa Heche kupitia hiyo project.
Kama Chadema wakishindwa kumlinda Heche basi nachokifikria kinaenda kutimia
 
Njia Bora ya kumlinda ni kuunda tume huru ifanye uchunguzi huru na majibu yatoke hadharani
 
Gentleman with nonsense mayhem,
lengo haikua ni kumpa mchango huo mwenyekiti. Kwakua mchango ulie ulikua ni wa kiwango kikubwa sana cha pesa, na lema na sugu walifanya kazi kubwa sana kuwaomba rafiki zao hao kuichangia chadema, waliona ni heshima kuwakutanisha wachangiaji hao na heche for recognitions. Na hivyo ndivyo wachangiaji wengi wa mamilioni ya pesa huichangia chadema.

Sasa kwamfano wewe unachangia buku tu nani akupeleke kwa heche kwa mfano? Wakati huna hata rafiki unaeweza kushawishi nae achangie buku?

Halafu gentleman,
mimi nina muamini Mungu pekee na sio huo ushirikina unaoeleza ๐Ÿ’
 
Jenga Chama wewe..hayo yalishaisha..Ukweli ni ule alioutoa Mnyika kwamba Pesa hazijaliwa.

Madam Brenda majuzi ametoa wito kwa Mwenye kujua zaidi na awape ushahidi na watachukua hatua.
 
Matumaini ya Samia sasa hivi yapo kwenye hilo Baraza la CHADEMA, kupata mwanya wa kukivuruga chama; na hiki ndiyo kitakachokuwa kipimo muhimu cha kujuwa utayari wa CHADEMA kushika madaraka.

Ni wazi, kwa sasa John Heche ndicho kizingiti wanachotafuta kuking'oa kuisambaratisha CHADEMA.
 
Jenga Chama wewe..hayo yalishaisha..Ukweli ni ule alioutoa Mnyika kwamba Pesa hazijaliwa.

Madam Brenda majuzi ametoa wito kwa Mwenye kujua zaidi na awape ushahidi na watachukua hatua.
Tofauti yangu na wewe ni huo mstari wa kwanza,...."hayo yalishaisha...".
Kama zilikuwa ni mbinu zilizotengenezwa nje, na Lema kazipokea na kuziingiza ndani ya chama; umejuwaje kuwa "hayo yalishaisha" Lema kakwambia hivyo; kasema popote hata huko ndani ya chama kwamba aliingia kwenye mtego wa wabaya wao, na anaomba yaishe?
Au anasubiri Baraza ili akiwashe zaidi?
 
NI IMANI YA WATANZANIA WOTE YA KWAMBA CHADEMA NI CHAMA SAFI,IKIMAANISHA HAKUNA RUSHWA,UFISADI WALA WIZI,NDIYO MAANA KINAPATA NGUVU YA KUNYOOSHEA WENGINE KIDOLE,KWA DHANA HIYO HIYO ILI KUBAKI KATIKA UKAMILIFU WAKE,NA ENDAPO IKATOKEA TUHUMA,ILI KULINDA USAFI WA CHAMA NI VYEMA,ANAYETUHUMIWA KUKAA KANDO KWA MUDA ILI CHAMA KIFANYE KAZI YAKE YA KIUCHUNGUZI,KATIKA KUDUMISHA HESHIMA YA CHAMA,BASI HECHE KAA PEMBENI ILI KUTUNZA HESHIMA YA CHAMA,HOFU YAKO IPO WAPI HATA BAADA YA UCHUNGUZI NA WEWE UKIJIAMINI NI MTU SAFIII!...
USAFI WAKO NDANI YA CHAMA NI LAZIMA UTAKUREJESHEA MAMLAKA YAKO,AU UNAKOSA IMANI YA KUJIAMAINI KUHUSU USAFI WAKO NDANI YA CHAMA?
 
Usitishike naye ..Lema ni Mwanachama tu kama sisi wengine na ndiyo utambulisho Mkuu wa Mwanachadema,vyeo ni mgawanyo tu wa kazi ili chama kisonge..
Amini kabisa CHADEMA hii inauhakika wa kusonga mbele bila Heche au Lema,na wengineo.
Kuibua tuhuma kisha zikathibitika siyo za kweli ni jambo la kujenga na halipaswi kuchukuliwa kama ni kosa na haipo mantiki ya kuanza kumzonga mtoa taarifa.Pengine ipo siku atakuja na tuhuma za ukweli na akakisaidia chama.
Yaliisha ilipothibitishwa na mmoja wa signatories kwamba zipo...Labda na wewe kama unajua hazimo au zimeoungua ..Fanya tu kama Lema,ibua tuhuma na wape ushahidi Wahusika waweze kufuatilia.Duru zinaarifu hata Lema mwenyewe alisema anasikika...
 
Mimi ninakuelewa wewe kwa haya unayozungumza hapa; lakini sijui kama wewe ndiye Lema mwenyewe.
Na ungekuwa ndiye yeye, ningekushauri usawazishe haya yote huko huko ndani ya chama, tena kwa nguvu zaidi bila hata ya chembe ya 'doubt'.

Hili swala la kusema CHADEMA ni wanachama na siyo viongozi, pia lina kasoro yake. Tumeona ilipofikia CCM sasa bila ya kuwa na viongozi wasiokuwa imara.

CCM kilikuwa chama imara sana, chenye wanachama tuliodhani wanatambua umuhimu wa kuwa huru na kulinda heshima ya taifa hili.
Sasa niambie kama CCM hiyo ndiyo hii tuliyonayo sasa..

Tatizo na hatari inayokikabili CHADEMA sasa hivi; pamoja na kuwa na wanachama wanaotambua hatari zinazowakabili ni kwamba chama hakijapewa nafasi ya kutulia tokea kilipochukua maamuzi ya kubadili uongozi na kuwa na mwelekeo mpya.
CHADEMA kinazongwa na baadhi ya waliomo ndani, hata kama ni wachache, ambao hawajaachana na hisia zilizotokana na msuguano uliopita. Kundi hili linashirikiana/linatumiwa na hao hao waliotaka uongozi wa zamani ubakie madarakani.

Lema anatakiwa ndiye awe mstari wa mbele kuondoa sintofahamu hiyo aliyoiingiza yeye ndani ya chama. Akinyamazia tu, hiyo ni ishara hasi.
 
..mwambie Lema na sugu hizo ndio gharama za recognition..ukilalamika kiwango cha ujinga kinakuwa juu zaidi, bora unyamaze liwe funzo kwako..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ