Lema: Vijana wa CHEDEMA wanyimwa dhamana Singida kisa kuimba nyimbo ya Taifa na bendera ya chama

dosama

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Posts
912
Reaction score
957
Nilikwenda Singida kuwasalimu KM BAVICHA Nusrat/ Mwenezi Twaha Mwaipaya, sikuweza kuwaona wanashitakiwa kwa kosa la kuimba wimbo wa Taifa huku wakiwa wameshika bendera ya Chama.

Wote wamenyimwa dhamana, kwani hati ya kiapo cha DPP inasema wao kukaa kwao nje ni hatari kwa usalama. Mahakama inapaswa kulinda haki za Binadamu kwa dhati, kwani ni chombo cha maamuzi ya haki, hofu yoyote juu yake ni mwelekeo mbaya kwa Nchi.

Wanaoteswa wakikata tamaa, mnaotesa mtakuwa kwenye hali mbaya sana. Mateso yakizidi kifo kinapoteza thamani.

Twendeni mpaka mwanzo wa bahari.
 
Swali, wanakosa au hawana kosa?,je walikusudia kufanya kosa au ni bahati mbaya ?,je kukosa dhamana ni salama kwao ?,kosa linadhhaminika ?
 
Swali wanakosa au hawana kosa?
Tupe maoni yako scenario, umeiona hapo kama wimbo wa Taifa unaimbwa hata kwenye viwanja nvya mpira kwaajili ya michezo je hawa wametenda lipi baya dhidi ya nchi yao ?
 
Tukimtanguliza mungu mbereeeeeee,MNIOMBEEEEEEEEEEEEEEEE.
 
Swali, wanakosa au hawana kosa?,je walikusudia kufanya kosa au ni bahati mbaya ?,je kukosa dhamana ni salama kwao ?,kosa linadhhaminika ?
Kuwanyima dhamana ni kuwakomoa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…