Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Kubalansi wote Kuachiwa imeshindikana hivyo balansi inayofanyika sasa ni Wote kwenda Jela ili Jumuiya ya Kimataifa ione kuna Haki na hakuna anayeonewa Tanzania.
Ni kweli kabisa sheria ichukue mkondo wake. Majaji na mahakimu wawe huru ku dispence justice kwa mujibu wa sheria bila kuingiliwa na mamlaka nyinginezo. Wawe firm and fair
 
Kesi ya kubumba ni kazi sana kumtia mtu hatiani...so far hata kama hujui sheria unaelewa hamna kitu mule.
Wale kina Kingai wamefanya uhuni.
 
Kufuatia kuhukumiwa miaka 30 jela aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake, kama taifa tumeachiwa mafundisho kadhaa..

1. Katiba Mpya - inahitajika kuondoa umungu mtu uliotamalaki nchini toka kwa viongozi wa CCM, tusiendelee kuishi kwa kutegemea fadhila za Rais aliyeko madarakani, badala yake sheria ndio iwe kiongozi wetu.

2. Kulindana - hii nayo ingetokea endapo marehemu Magufuli angeluwa bado yuko hai, siamini kama Sabaya angeshtakiwa na mwishowe kuhukumiwa.

3. Cheo ni dhamana - hasa kwa vijana, wasivimbe vichwa wanapopewa madaraka kwa kisingizio cha kulindwa na wakubwa, kwani hawajui kesho yao itakuwaje endapo mkubwa atakapofariki.

4. Mahakama ziachwe zifanye kazi zake kwa uhuru, zisiingiliwe na yeyote, makosa ya Sabaya yalikuwa dhahiri na yalionekana mpaka kwenye camera za CCTV, hivyo hukumu iliyotoka ni ya haki kulingana na kosa aliloshtakiwa nalo na adhabu aliyopewa.

5. Wapambe kukimbia - hawa huwa karibu na kiongozi anayeenda kinyume na tatatibu za majukumu yake kwa kumjaza maneno ya uongo ajione ana support ya kutosha, lakini mara baada ya kutiwa hatiani na kuhukumiwa, hawa jamaa hupotea kama upepo na kumuacha mhusika peke yake bila msaada.

Ni wakati sasa kwa watanzania kuamka na kudai Katiba Mpya itakayoleta usawa kwenye jamii yetu, itakayoweka misingi ya majukumu na mipaka ya utekelezaji wa majukumu hayo kisheria, ili kuzuia uwepo wa watu wa aina ya Sabaya huko mbele ya safari ambao huamua kuwaumiza watanzania wenzao kwa maslahi yao binafsi na ya chama chao CCM.
support! well narrated! Thanks!
 
Mnaposhangilia pia mjiandae hizi kesi zote zipo chini ya TISS Hawa mahakimu hukumu wanaandikiwa.

Ni sawa sababya kufungwa lakini majonzi yatakuwa makubwa Sana kwa Mbowe Kama wafuasi wa chadema hawataingia barabarani.

Inawezekana Mbowe hatutamuona Tena mpaka 2026 Tena kwa dharau ataachiwa kwa msamaha wa Rais.
Mbowe hawezi kufungwa kwasababu hakuna ushahidi wa kumfunga. Labda itumike siasa. Ole sabaya kavamia duka la watu na silaha na kachukua fedha na ushahidi upo wazi mlitaka waachiwe?
 
Imenikumbusha uoinzani walirejeshewa ushindi wa uchaguzi kwa wabunge wao mahakamani! Kilichofuatia, rufaa za chama dola nazo zikashinda, kuna mazingira yalitengenezwa watu wakaingia king.

Lakini sio mara zote mambo yataenda kama tunavyowaza, kwanini isiwe mahakama imeamua kufanya kazi yake kwa weledi bila kuingiliwa kwenye maamuzi yake ili wakandamizaji waliojitutumua wapate haki yao?

Subira yavuta heri
 
wote mnaofurahia msiombe siku moja ukaenda mahakamani na ujua kabisa ukweli huna kosa ila ukaenda na maji ...

duniani hakuna mahakama ni upumbavu mtupu hakuna cha mahakama wala nini ni ujinga + ujinga ...

sibirini ya Mbowe ndio mtajua hamjui
Kajambe mbele huko.au kama unamuonea huruma sana nenda kamsaidie. Au mlikua wote kwenye ujambazi nini
 
Ana wakati mgumu sana hili tukio limemkuta ghafla hakutegemea, alijua atalindwa na mamlaka mpaka mwisho wa safari kumbe hakuwa akilindwa na mamlaka bali alikuwa akilindwa na mtu mmoja ambae kwa sasa ni marehemu, amejikuta yuko peke yake mahakamani asijue la kujitetea ndio maana ameongea vitu vinavyoonekana vya ajabu.
 
Kubalansi wote Kuachiwa imeshindikana hivyo balansi inayofanyika sasa ni Wote kwenda Jela ili Jumuiya ya Kimataifa ione kuna Haki na hakuna anayeonewa Tanzania.
Acha ramli chonganishi Genta, kabla ya Sabaya yupo aliyevunja Green house, huyo ni spare, Huyo akavuka mipaka akaamua kuanza na wanaomsaidia aliyepachikwa Ugaidi, mwishowe baada ya mfungwa kuona au kuhisi ameishiwa nguvu usaidizi was wanaPGO ukaingilia kati wakiamini wanemazila Mbowe Kwa kumbambikia ugaidi na ndio uiuwa chadema na ndio kunfurahisha, au kumharibia mwenye mamlaka, mlicholenga mnajua wenyewe. Funzo msikariri mambo, hii Dunia niya Mola.
 
Duh kwamba mahakama inacheza na hisia sio facts
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hakuna ushahidi wa kumtia Mbowe hatiani. Mahakama haipaswi zifanye kazi zake kisiasa kwamba kwa kuwa huyu mhuni Sabaya kafungwa basi na Mbowe ni lazima afungwe.

Kubalansi wote Kuachiwa imeshindikana hivyo balansi inayofanyika sasa ni Wote kwenda Jela ili Jumuiya ya Kimataifa ione kuna Haki na hakuna anayeonewa Tanzania.
 
Back
Top Bottom