Kufuatia kuhukumiwa miaka 30 jela aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake, kama taifa tumeachiwa mafundisho kadhaa..
1. Katiba Mpya - inahitajika kuondoa umungu mtu uliotamalaki nchini toka kwa viongozi wa CCM, tusiendelee kuishi kwa kutegemea fadhila za Rais aliyeko madarakani, badala yake sheria ndio iwe kiongozi wetu.
2. Kulindana - hii nayo ingetokea endapo marehemu Magufuli angeluwa bado yuko hai, siamini kama Sabaya angeshtakiwa na mwishowe kuhukumiwa.
3. Cheo ni dhamana - hasa kwa vijana, wasivimbe vichwa wanapopewa madaraka kwa kisingizio cha kulindwa na wakubwa, kwani hawajui kesho yao itakuwaje endapo mkubwa atakapofariki.
4. Mahakama ziachwe zifanye kazi zake kwa uhuru, zisiingiliwe na yeyote, makosa ya Sabaya yalikuwa dhahiri na yalionekana mpaka kwenye camera za CCTV, hivyo hukumu iliyotoka ni ya haki kulingana na kosa aliloshtakiwa nalo na adhabu aliyopewa.
5. Wapambe kukimbia - hawa huwa karibu na kiongozi anayeenda kinyume na tatatibu za majukumu yake kwa kumjaza maneno ya uongo ajione ana support ya kutosha, lakini mara baada ya kutiwa hatiani na kuhukumiwa, hawa jamaa hupotea kama upepo na kumuacha mhusika peke yake bila msaada.
Ni wakati sasa kwa watanzania kuamka na kudai Katiba Mpya itakayoleta usawa kwenye jamii yetu, itakayoweka misingi ya majukumu na mipaka ya utekelezaji wa majukumu hayo kisheria, ili kuzuia uwepo wa watu wa aina ya Sabaya huko mbele ya safari ambao huamua kuwaumiza watanzania wenzao kwa maslahi yao binafsi na ya chama chao CCM.