Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Miaka 30 jela? JPM huko alipo atakuwa anaumia sana vijana wake kutendewa hivi
Aliwazaa yeye?wakati wao wanawatendea watu wengine ilikuwa haki tu eti?hujawahi kutana na sabaya kwenye kumi na nane zake alipokuwa madarakani
 
Mbowe ni 30+ hahaha aisee ni nouma. Waliokuwa wanashangilia ya Sabaya sasa tusubiri tena ya Mbowe
Mle hqmna kesi...PGO yenyewe tu imewaumbua..

Unapataje legal right wakati hukufuata utaratibu wa ukamataji na haki ya uliyemkamata.

Sheria naanzia pale police anapokwambia upo chini ya ulinzi kwa kutumia PGO na si anavyoona yeye inafaa
 
Mbowe anafungwa tuombe tu Mungu na tuendelee kuwepo

Hukumu ya sabaya hii 30 na bado ana kesi nyingine je akiukumiwa Tena 30 maana yake 60 hapa Kuna harufu ya siasa .

Aliokuwa akifaya nao Kazi wamemzunguka na kumtosa!!

Ila nawashauri msije kujaribu kumfunga Mbowe kitanuka street wajeda lazima watakinukisha tu!!
 
Sidhani. Hakuna kesi ya maana dhidi yake.
Wasiwasi wangu ni kulazimisha tu ili basi wamfunge, Had it been that we have an independent judiciary, I would be taking my cold beer waiting for a celebration day!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Wamemuhurumia anapewa chumba chake Jela.
Mahita yule rafiki yake waliokuwa wakishirikiana kuwabambikia kesi chadema kuwapiga watu yupo njiani kumfanyia Mipango akajifiche msumbiji mpaka kifungo kimalizike arejee
 
Kufuatia kuhukumiwa miaka 30 jela aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake, kama taifa tumeachiwa mafundisho kadhaa..

1. Katiba Mpya - inahitajika kuondoa umungu mtu uliotamalaki nchini toka kwa viongozi wa CCM, tusiendelee kuishi kwa kutegemea fadhila za Rais aliyeko madarakani, badala yake sheria ndio iwe kiongozi wetu.

2. Kulindana - hii nayo ingetokea endapo marehemu Magufuli angeluwa bado yuko hai, siamini kama Sabaya angeshtakiwa na mwishowe kuhukumiwa.

3. Cheo ni dhamana - hasa kwa vijana, wasivimbe vichwa wanapopewa madaraka kwa kisingizio cha kulindwa na wakubwa, kwani hawajui kesho yao itakuwaje endapo mkubwa atakapofariki.

4. Mahakama ziachwe zifanye kazi zake kwa uhuru, zisiingiliwe na yeyote, makosa ya Sabaya yalikuwa dhahiri na yalionekana mpaka kwenye camera za CCTV, hivyo hukumu iliyotoka ni ya haki kulingana na kosa aliloshtakiwa nalo na adhabu aliyopewa.

5. Wapambe kukimbia - hawa huwa karibu na kiongozi anayeenda kinyume na tatatibu za majukumu yake kwa kumjaza maneno ya uongo ajione ana support ya kutosha, lakini mara baada ya kutiwa hatiani na kuhukumiwa, hawa jamaa hupotea kama upepo na kumuacha mhusika peke yake bila msaada.

Ni wakati sasa kwa watanzania kuamka na kudai Katiba Mpya itakayoleta usawa kwenye jamii yetu, itakayoweka misingi ya majukumu na mipaka ya utekelezaji wa majukumu hayo kisheria, ili kuzuia uwepo wa watu wa aina ya Sabaya huko mbele ya safari ambao huamua kuwaumiza watanzania wenzao kwa maslahi yao binafsi na ya chama chao CCM.
 
Wote mnaofurahia msiombe siku moja ukaenda mahakamani na ujua kabisa ukweli huna kosa ila ukaenda na maji ...

Duniani hakuna mahakama ni upumbavu mtupu hakuna cha mahakama wala nini ni ujinga + ujinga ...

Sibirini ya Mbowe ndio mtajua hamjui
Sasa mnalalamika nini kuna mtu alimtuma akavamie maduka ya watu? Si alisema makamu Dr. Mpango anayajua hayo maagizo mbona kamkana. Wacheni upumbavu mnapopewa madaraka muachage ulimbukeni.
 
hahahahaha tulikuwa tunadai haki kwa Sabaya...ndio hiyo haki Sabaya kaipata.....wengine wanadai haki kwa Mbowe pia. Sabaya anakwenda kutoa ushahidi dhidi ya Mbowe kumtishia maisha, kumbuka alitishiwa maisha akiwa kiongozi wa umma na akitekeleza majukumu ya umma....Ndio maana kuna wakati tunapaswa kutokuwa mashabiki wa siasa baadala yake tuishi kwa uhalisia bila kuangalia upande...

Unaweza kutupiwa ndoano halafu ukaimeza nzima nzima ukaimeza...
kutupiwa ndoano kwa.miaka 30 we jamaaa ni aje
 
Back
Top Bottom