TABASAMU LA OLE SEBAYA LINA SIRI NZITO.
Anaandika, Robert Heriel
Ni kweli Ole Sebaya ni miongoni mwa Viongozi waliokuwa wakifanya kazi Kwa namna ya kipumbavu Sana, Hakuwa pekeake, walikuwa wa Aina yake kadha wa kadha, hao walijifanya miungu watu. Maneno yaliyowatoka midomoni yalikuwa kama wendawazimu. Sitaki kuwataja Ila wanajifahamu wenyewe na wengi walipata nafasi ya kusoma baadhi ya maandiko yangu. Wapo waliojirekebisha lakini wapo waliokaidi. Hata hivyo ndivyo maisha yatakavyo hivyo, wengine waangamie na wengine waokoke.
Mbali na udhaifu wa Ole Sebaya katika misukosuko yake tangu imkute lakini Jambo moja ninaweza kumsifu; nalo ni TABASAMU.
Ole Sebaya pamoja na uhuni wako ambao wengine tuliutambua Kwa ishara za lugha uongeapo kipindi ukiwa Mkuu wa wilaya, siwezi kuwa Mnafiki nikanyamaza kukunyima sifa hii, TABASAMU hata kwenye nyakati ngumu.
TABASAMU la OLE Sebaya linanifundisha mambo kadhaa, na linanifanya nimsifu Kwa ushujaa huo. Unajua kutabasamu wakati WA taabu sio mchezo.
Kila nilipomuona Ole Sebaya akishuka kwenye karandinga la mahabusu alishuka akiwa anatabasamu.
Jambo hili niliwahi fundishwa zamani Sana nikiwa mtoto mdogo kuwa;
Mbinu moja wapo ya kukabiliana na nyakati ngumu ni KUTABASAMU.
Mbinu hii nimeishuhudia mara mbili, na Ole Sebaya anakuwa mtu wa tatu kumuona akiwa anatabasamu hata akiwa katika Mazingira magumu.
Sina Shaka kuwa Ole Sebaya ni Mhalifu, katika hilo sina Shaka kwani alishajuonyesha tangu alipopewa Cheo cha ukuu wa wilaya. Ingawaje wapo wengine ambao bila Shaka muda huu wanaomba miungu yao kuwa upepo wa Sebaya usiwageukia na wao.
TABASAMU la Sebaya linaweza kuwa na maana Kati ya zifuatazo;
1. Matumaini.
Ole Sebaya anatabasamu huenda anamaana kuwa anayopitia ni majaribu tuu, yote yatapita
2. Majuto
Ole Sebaya anatabasamu Kama mtu anayejuta, anayejidharau kuwa alikuwa mjinga na Mpumbavu, n.k
3. HAKUWA PEKEAKE.
Ole Sebaya huenda anatabasamu Kwa sababu anashangaa kageuka Mbuzi WA kafara, waliofanya Kama yeye huenda walikuwa wengi lakini anaona yeye ndiye kaangukiwa na kitu kizito.
4. MAPENZI YA MCHUMBA WAKE YAMEMPONZA.
TABASAMU la OLE linasema mambo mengi.
Yale ya ngoswe kipenzi cha uzembe yanaweza kuwa yamemkuta Bwana Sebaya.
Huenda zile hela za unyang'anyi alikuwa anazipeleka Kwa mchumba wake huyo ambaye ndiye aliiomba mahakama imfikirie kwani anamchumba amemtolea mahari.
Sebaya huenda anatabasamu Kwa kujicheka kuona mchumba wake kasababisha kajiingiza katika matatizo.
Huenda anatabasamu kila akikumbuka akiombwa pesa ndefu na mchumba wake, huku Mshahara wa ukuu wa wilaya akiona ni mdogo. Hayo yote ni assumption tuu.
Ila Siri za TABASAMU la OLE Sebaya anazijua yeye mwenyewe.
Ole Sebaya mbali na kuwa sikupendezwa na tabia zako mbofu na nilitarajia matokeo haya kwako lakini nisiwe muongo kuwa nilikuona jasiri kila nilipoona unatabasamu.
Nitaenda kumtembelea Ole Sebaya kisha nitamuuliza TABASAMU lake lilikuwa na maana gani?
Ipendeze Ukate Rufaa alafu ujipange kwenye kujitetea bhana. Masuala ya kitoto ya kuleta Uchumba kwenye ishu nzito zinazokukabili uachane nazo.
Mimi nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam