Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Tusishangae akipewa kifungo kifupi sana au hata kifungo cha nje na faini juu. Hizi mahakama zetu sina imani nazo kwani maamuzi yake yana harufu za kisiasa.

Wanajukwaa poleni kwa kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Bila shaka baada ya Hukumu ya Lengai Ole Sabaya kuhairishwa tarehe 1/10/2021 ilipangwa kwamba itatolewa leo. Hivyo tuelekeze masikio yetu katika viunga vya mahakama.

=======

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo Oktoba Mosi, 2021 baada ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.

Agosti 24 mwaka huu, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walikamilisha kujitetea mahakamani hapo baada ya Jamhuri kukamilisha mashahidi 11 na vielelezo vinane.

Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Chanzo: Mwananchi
 
Shule ya kata matunda yake, I am sorry anyway!
Tusamehe mkuu sio makosa yetu ni CCM ndio inataka tuwe wajinga ili itutawale. Na imetupata tupo wengi kweli tuna Akili lakini akili zetu zenyewe hazina akili😂😂😂
Nyerere day tukiweka mauwa kwa kaburi la baba wa Taifa.👇🏾

832799A2-20C2-41BA-AD77-40BA4E326981.jpeg


059EC95A-B323-4EC6-8EAF-E04DA636BC50.jpeg
 
Back
Top Bottom