Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Wale Mataga na Chawa wa ole Sasa hizi wanalia na kusaga meno.
Huyu hapa mmoja wapo
Screenshot_2021-10-15-17-01-00-066_com.facebook.katana.jpg
 
Amesukumwa ndani miaka 30 jela,hii iwe fundisho kwa malimbukeni wengine wa madaraka
 
Hukumu ya kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya inasomwa muda huu katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Akisoma maelezo ya awali Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Odira Amworo amesema kati ya mashahidi 11 wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi wao, ambapo ushahidi wa watu 9 umeonekana una mashiko na ushahidi wa watu wawili umetupwa.

Hakimu Amworo amesema kuwa mahakama imejiridhisha kuwa siku ya tukio February 9 mwaka 2021 washtakiwa wote watatu walikua dukani kwa Saad na wote walishiriki kufanya unyang'anyi wa kutumia silaha, kabla ya kumpiga Saad na kumsabanishia majeraha, wakitaka wapewe TZS 100M au mfanyabiashara huyo apewe kesi ya uhujumu uchumi.

Hakimu anasema kwa mujibu wa kifungu cha 201 cha sheria ya makosa ya adhabu, mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kutumia silaha kunyang'anya mali ya mtu mwingine, adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela pamoja na viboko 12 au miaka 30 bila viboko.

Baada ya kusema hayo Sabaya alianguka na kudaiwa kuzimia, hali iliyofanya Hakimu kuahirisha kusoma hukumu hiyo kwa dakika 5. Baadae Sabaya alizinduka na hukumu ikaendelea kusomwa.

Kabla hajataja adhabu, Hakimu amewapa washtakiwa nafasi kujitetea kwa mara ya mwisho, ambapo Sabaya ameomba apunguziwe adhabu kwa sababu anaye mchumba ambaye ameshamtolea mahari na hivyo akihukumiwa miaka mingi atashindwa kumuoa.

Hukumu inaendelea kusomwa. Letz keep waiting.!

Malisa

Wanajukwaa poleni kwa kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Bila shaka baada ya Hukumu ya Lengai Ole Sabaya kuhairishwa tarehe 1/10/2021 ilipangwa kwamba itatolewa leo. Hivyo tuelekeze masikio yetu katika viunga vya mahakama.

=======

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo Oktoba Mosi, 2021 baada ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.

Agosti 24 mwaka huu, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walikamilisha kujitetea mahakamani hapo baada ya Jamhuri kukamilisha mashahidi 11 na vielelezo vinane.

Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Chanzo: Mwananchi

UPDATE: SABAYA NA WENZAKE MIAKA 30 JELA

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ol
 
Hii taarifa imenivuruga. Maelezo na kichwa cha mada kama mvurugo hivi. Nilitaka kuona tu mtu ahukumiwa kunyongwa.
 
Sabaya alikosea aliposema oparesheni zake zilikubaliwa na wakubwa ( kina jiwe )

pole zake
 
Tushangilia hukumu hii, lakini pia ni maandalizi ya hukumu nyingine kwa mtu fulani na shahidi akiwa huyuhuyu....hapa tunaamini mahakama imetenda haki maana kwingine tutailaumu mahakama..
 
Hukumu inapitishwa wakati Mama yuko ziarani Arusha na Kilimanjaro?
Huenda akabadili upepo!
 
Back
Top Bottom