Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Hukumu ya kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya inasomwa muda huu katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Akisoma maelezo ya awali Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Odira Amworo amesema kati ya mashahidi 11 wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi wao, ambapo ushahidi wa watu 9 umeonekana una mashiko na ushahidi wa watu wawili umetupwa.

Hakimu Amworo amesema kuwa mahakama imejiridhisha kuwa siku ya tukio February 9 mwaka 2021 washtakiwa wote watatu walikua dukani kwa Saad na wote walishiriki kufanya unyang'anyi wa kutumia silaha, kabla ya kumpiga Saad na kumsabanishia majeraha, wakitaka wapewe TZS 100M au mfanyabiashara huyo apewe kesi ya uhujumu uchumi.

Hakimu anasema kwa mujibu wa kifungu cha 201 cha sheria ya makosa ya adhabu, mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kutumia silaha kunyang'anya mali ya mtu mwingine, adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela pamoja na viboko 12 au miaka 30 bila viboko.

Baada ya kusema hayo Sabaya alianguka na kudaiwa kuzimia, hali iliyofanya Hakimu kuahirisha kusoma hukumu hiyo kwa dakika 5. Baadae Sabaya alizinduka na hukumu ikaendelea kusomwa.

Kabla hajataja adhabu, Hakimu amewapa washtakiwa nafasi kujitetea kwa mara ya mwisho, ambapo Sabaya ameomba apunguziwe adhabu kwa sababu anaye mchumba ambaye ameshamtolea mahari na hivyo akihukumiwa miaka mingi atashindwa kumuoa.

Hukumu inaendelea kusomwa. Letz keep waiting.!
FB_IMG_1634307998484.jpg
 
Mchezesha ngoma ndie aliemkamata manju,ngoma inaanza kusukwa, tukutane kesho siyo mbali sana na jana.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Confirmed kikwelikweli, kama hivyo ni habari njema Kwa wapenda haki wote, ila mbaya Kwa watenda uovu na wapenda kuona uovu ukitendeka. Binafsi ni furaha kwangu Kwa manyanyaso na uonevu uliotenda Kwa wale alioaminu wanatofautiana na itikadi yake ya kisiasa au Ile ya chama chake aliona hawastahili kupata haki yoyote Kwa matendo yake aliyoyafanya dhidi Yao
 
Hivi kuwa na mchumba uliyemlipia mahari ndio utetezi wa Ujambazi wake?[emoji28],yeye wakati anabaka wanawake wa watu huo muda si asingetumia kumuoa huyo mchumba?
 
Sabaya amehukumiwa miaka 30 jela
Mahakama ya hakimu mkazi Arusha imemuhukumu kwenda jela kwa miaka 30 aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai ole sabaya na wenzake kwa kosa la unyang'anyi kwa kutumia siraha
Not true! source of news?
 
"Mwenzako anaponyolewa, wewe tia maji"-Jiandae ndugu Mbowe
Hizi propaganda mmeanza kujiliwaza ili iweje, pambaneni na hali yenu, Sabaya ni shetani hilo halina ubishi, atubu gerezani, km mnataka kubalance mambo poleni.
 
Hivi si ana kesi nyingine tena Kilimanjaro? Tuna la KUJIFUNZA hapa katika uongozi.
 
Afadhali maana alijifanya task force ya mwendazake kumbe anafanya ujambazi
 
Back
Top Bottom