Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

[emoji28][emoji28]nimecheka kama mazuri.wanasheria wa huyu mwamba wali fail wapi
 
Utoto ulikuwa unamsumbua, they were and are still young to hold such positions. Kama ingelikuwa siyo kuwatesa/kuwa na kuwaibia watu, I would pardon him due to his young age!
Young age!??? Come-one!! Miaka 35 unashindwaje kuongoza wilaya? Young age ndo inampeleka kwenda kulazimisha kwa kutumia silaha? Tatizo ni moja: Mfumo uliotumika kumuweka kwa hiyo nafasi, pamoja na kutoact timely pale ilipoonekana anatenda masuala ambayo siyo mazuri sana na hakuchukuliwa hatua--- Kama mfumo ulikosea wakati wa vetting, basi alitakiwa kubadilishwa mapema kabisa---Hakuna factor ya young age kabisa hapo!!!
 
Hukumu ya kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya inasomwa muda huu katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Akisoma maelezo ya awali Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Odira Amworo amesema kati ya mashahidi 11 wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi wao, ambapo ushahidi wa watu 9 umeonekana una mashiko na ushahidi wa watu wawili umetupwa.

Hakimu Amworo amesema kuwa mahakama imejiridhisha kuwa siku ya tukio February 9 mwaka 2021 washtakiwa wote watatu walikua dukani kwa Saad na wote walishiriki kufanya unyang'anyi wa kutumia silaha, kabla ya kumpiga Saad na kumsabanishia majeraha, wakitaka wapewe TZS 100M au mfanyabiashara huyo apewe kesi ya uhujumu uchumi.

Hakimu anasema kwa mujibu wa kifungu cha 201 cha sheria ya makosa ya adhabu, mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kutumia silaha kunyang'anya mali ya mtu mwingine, adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela pamoja na viboko 12 au miaka 30 bila viboko.

Baada ya kusema hayo Sabaya alianguka na kudaiwa kuzimia, hali iliyofanya Hakimu kuahirisha kusoma hukumu hiyo kwa dakika 5. Baadae Sabaya alizinduka na hukumu ikaendelea kusomwa.

Kabla hajataja adhabu, Hakimu amewapa washtakiwa nafasi kujitetea kwa mara ya mwisho, ambapo Sabaya ameomba apunguziwe adhabu kwa sababu anaye mchumba ambaye ameshamtolea mahari na hivyo akihukumiwa miaka mingi atashindwa kumuoa.

Hukumu inaendelea kusomwa. Letz keep waiting.!View attachment 1975366
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Kosa la unyanganyi na kutumia silaha miaka 30 huyu kijana kuna kosa alimfanyia mama nadhani ndio maana ameadhibiwa kiasi hicho sio bure kabisaa.....Ila mama na yeye afahamu yeye mtu wa dini....
 
Sijapenda hukumu hii maana wasiwe wanajenga ngao ya kumfunga Mbowe na baadaye wam- pardon Sabaya na kumsamehe na kumpa cheo!
Mwanaccm Sabaya ameshitakiwa kwa makosa ya kweli , Mbowe kesi yake ni ya uongo
 
Mama mwaka 2025 anaondoka hapo alipo sio Rais sio chochote....
 
Ila mama hapa amecheza vibaya sana maana anataka aonekana yeye mtu mzuri aje kusema kesho kwamba jamaa aachiwe....timeshajuwa huo mchezo tayari anatafuta ufahari wa kijinga tu
 
Aliyekuwa Dc wa Hai Ole Sabaya baada ya kuhukumiwa amewatoa wasiwasi wafuasi wake kwa kuwapa kauli ya kiroho , Amesema hivi , Nanukuu , MSIJALI MAANA MUNGU YUKO KAZINI , Mwisho wa kunukuu .

Chanzo : Mwananchi

Nachukua nafasi hii mimi binafsi kuipa pole sana familia ya Ole Sabaya kwa shida iliyotokea kutokana na hukumu aliyopewa kijana wao .
Lipo jambo la kujifunza. Kwa viongozi, mnaweza kuwamiza sana viongozi kwa chini kutekeleza kazi majukumu yao. Kwa viongozi wa chini, fanya yaliyo katika majukumu yako
 
Back
Top Bottom