Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Mnaposhangilia pia mjiandae hizi kesi zote zipo chini ya TISS Hawa mahakimu hukumu wanaandikiwa.

Ni sawa sababya kufungwa lakini majonzi yatakuwa makubwa Sana kwa Mbowe Kama wafuasi wa chadema hawataingia barabarani.

Inawezekana Mbowe hatutamuona Tena mpaka 2026 Tena kwa dharau ataachiwa kwa msamaha wa Rais.
Hakuna wa kuingia road siunaona leo wala hakuna cha mabango wala nini na.shughuli imefanyikia kwenye ngome yake

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Haki emetendeka, hii iwe fundisho Kwa majambazi wengine.
bashite ameponea chupuchupu
Ashukuru Mungu, Ruge hayupo! Ule uvamizi alioufanya pale Cloud, sio wa kuuachia hivi hivi. Ushahidi uliochunguzwa na ile tume iliyoundwa na Nape, itumike!
 
Pamoja na mabaya yake lakn hukumu imekua kali sana mawakili wa utetezi wame prove failure jela si jambo la kufurahia kwa mtu kamwe
 
Nasomeka vizuri tu, sema wewe ndo ndo uelewi, mimi nilitaka kujua miaka alohukumiwa ili nipate jibu ninachokiwaza.siasa ni mchezo mchafu
Rugemalira hakuhukumiwa kifungo kama Sabaya, kesi ya Ruge DPP aliifuta.
 
Acha kutoa hukumu kwa kuwaza miujiza brother. Mahakama inafuata sheria siyo mihemko ya kiccm
Ndio maana yake!

Na lazima ifuate sheria hata kwa kesi ya gaidi kama ilivyofanya kwa sabaya!

Hakika mahakama zetu ziko huru sana
 
Nasema hivi,Mungu wa haki huwa yupo.Kama kuna watu bado wana hulka za kuumiza wengine watavuna wanachopanda.
 
TABASAMU LA OLE SEBAYA LINA SIRI NZITO.

Anaandika, Robert Heriel

Ni kweli Ole Sebaya ni miongoni mwa Viongozi waliokuwa wakifanya kazi Kwa namna ya kipumbavu Sana, Hakuwa pekeake, walikuwa wa Aina yake kadha wa kadha, hao walijifanya miungu watu. Maneno yaliyowatoka midomoni yalikuwa kama wendawazimu. Sitaki kuwataja Ila wanajifahamu wenyewe na wengi walipata nafasi ya kusoma baadhi ya maandiko yangu. Wapo waliojirekebisha lakini wapo waliokaidi. Hata hivyo ndivyo maisha yatakavyo hivyo, wengine waangamie na wengine waokoke.

Mbali na udhaifu wa Ole Sebaya katika misukosuko yake tangu imkute lakini Jambo moja ninaweza kumsifu; nalo ni TABASAMU.

Ole Sebaya pamoja na uhuni wako ambao wengine tuliutambua Kwa ishara za lugha uongeapo kipindi ukiwa Mkuu wa wilaya, siwezi kuwa Mnafiki nikanyamaza kukunyima sifa hii, TABASAMU hata kwenye nyakati ngumu.


TABASAMU la OLE Sebaya linanifundisha mambo kadhaa, na linanifanya nimsifu Kwa ushujaa huo. Unajua kutabasamu wakati WA taabu sio mchezo.

Kila nilipomuona Ole Sebaya akishuka kwenye karandinga la mahabusu alishuka akiwa anatabasamu.
Jambo hili niliwahi fundishwa zamani Sana nikiwa mtoto mdogo kuwa;

Mbinu moja wapo ya kukabiliana na nyakati ngumu ni KUTABASAMU.
Mbinu hii nimeishuhudia mara mbili, na Ole Sebaya anakuwa mtu wa tatu kumuona akiwa anatabasamu hata akiwa katika Mazingira magumu.

Sina Shaka kuwa Ole Sebaya ni Mhalifu, katika hilo sina Shaka kwani alishajuonyesha tangu alipopewa Cheo cha ukuu wa wilaya. Ingawaje wapo wengine ambao bila Shaka muda huu wanaomba miungu yao kuwa upepo wa Sebaya usiwageukia na wao.

TABASAMU la Sebaya linaweza kuwa na maana Kati ya zifuatazo;
1. Matumaini.
Ole Sebaya anatabasamu huenda anamaana kuwa anayopitia ni majaribu tuu, yote yatapita

2. Majuto
Ole Sebaya anatabasamu Kama mtu anayejuta, anayejidharau kuwa alikuwa mjinga na Mpumbavu, n.k

3. HAKUWA PEKEAKE.
Ole Sebaya huenda anatabasamu Kwa sababu anashangaa kageuka Mbuzi WA kafara, waliofanya Kama yeye huenda walikuwa wengi lakini anaona yeye ndiye kaangukiwa na kitu kizito.

4. MAPENZI YA MCHUMBA WAKE YAMEMPONZA.
TABASAMU la OLE linasema mambo mengi.
Yale ya ngoswe kipenzi cha uzembe yanaweza kuwa yamemkuta Bwana Sebaya.
Huenda zile hela za unyang'anyi alikuwa anazipeleka Kwa mchumba wake huyo ambaye ndiye aliiomba mahakama imfikirie kwani anamchumba amemtolea mahari.

Sebaya huenda anatabasamu Kwa kujicheka kuona mchumba wake kasababisha kajiingiza katika matatizo.
Huenda anatabasamu kila akikumbuka akiombwa pesa ndefu na mchumba wake, huku Mshahara wa ukuu wa wilaya akiona ni mdogo. Hayo yote ni assumption tuu.

Ila Siri za TABASAMU la OLE Sebaya anazijua yeye mwenyewe.

Ole Sebaya mbali na kuwa sikupendezwa na tabia zako mbofu na nilitarajia matokeo haya kwako lakini nisiwe muongo kuwa nilikuona jasiri kila nilipoona unatabasamu.

Nitaenda kumtembelea Ole Sebaya kisha nitamuuliza TABASAMU lake lilikuwa na maana gani?

Ipendeze Ukate Rufaa alafu ujipange kwenye kujitetea bhana. Masuala ya kitoto ya kuleta Uchumba kwenye ishu nzito zinazokukabili uachane nazo.

Mimi nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Au anatabasamu kutokana na upungufu wa akili. Licha ya ujambazi alikuwa anamdharau sana bosi Mama Anna Mghwira hadi mahakamani akaropoka kuwa aliapishwa na mtu asiyemfahamu!!! Huyu ni chizi.
Anaulizwa una bastola anajibu sin ila nina kachuma tu kanaitwa Glock 17.
 
"TABASAMU", imekuwa "TABASAMU", robo tatu ya andiko zima, 'what the heck is that'!

Hapa kuna mtu aliyekuwa tayari kutoa roho za watu, leo hii tunahadithiwa juu ya tabasamu lake? Hakuna habari ya kumzungumzia huyu mtu na wengine wa aina yake ambao tunapaswa kuwaepuka kila iwezekanavyo kuweka watu wa aina hiyo kwenye uongozi wa nchi?

Hakuna mafunzo yoyote tunayoweza kuyafafanua tukitumia mifano ya hawa watu ili jamii ielewe hatari zinazoambatana na kutokuwa waangalifu kwenye kutafuta viongozi wa nchi yetu?
 
Au anatabasamu kutokana na upungufu wa akili. Licha ya ujambazi alikuwa anamdharau sana bosi Mama Anna Mghwira hadi mahakamani akaropoka kuwa aliapishwa na mtu asiyemfahamu!!! Huyu ni chizi.
Anaulizwa una bastola anajibu sin ila nina kachuma tu kanaitwa Glock 17.
Ofcoz tabasamu lake ni tatizo lake la kisaikolojia
 
Nafurahi sana mtu akini-tag inaonyesha ni kiasi gani ujumbe wangu unavowafikia huko kunako.
Tuna mpango wa kumpa miaka ya mvua bwana wenu mbowe na mnabahati wale mume zenu wengine wamekimbia nchi wakamuacha boya ambaye sasa hv anauona moto huko huku vibinti vikibishana huko Twita
Bora Mbowe ana miaka 60 sasa Sabaya miaka 35 no mke,no watoto so sad.Mbowe ana mke,watoto na wajukuu he has nothing to loose kama Sabaya anaelia na kwenda kuoa.Ila maharani akate rufaa mahakama itatenda haki na Mungu wetu hajalala.
 
Au anatabasamu kutokana na upungufu wa akili. Licha ya ujambazi alikuwa anamdharau sana bosi Mama Anna Mghwira hadi mahakamani akaropoka kuwa aliapishwa na mtu asiyemfahamu!!! Huyu ni chizi.
Anaulizwa una bastola anajibu sin ila nina kachuma tu kanaitwa Glock 17.


😄😄😄😄

Ole Sebaya hajui kuendana na Muktadha, huenda alijua yupo ndotoni, sasa akawa analeta masikhara
 
Back
Top Bottom