Tangu tupate uhuru, serikali ya Tanzania haijawahi kuwa na nia njema kwa wananchi wake; kisiasa, kiuchumi, wala kiafya.
Kodi tunazolipa hazitumiki kuinua hali ya maisha ya wananchi bali kuneemesha viongozi na ndugu zao. Kwa mfano; serikali kununua gari la Tshs 400m kwa ajili ya mkuu wa wilaya ni matumizi mabaya ya kodi zetu.
NHIF iliyopo sasa ipo taabani kifedha si kwa sababu watu hawachangii bali ufisadi!
Pamoja na serikali kuipigia promo Bima ya Afya kwa wote kwamba itakuwa mkombozi kwa afya ya wananchi, naiona vingine:
1. Watakaoiongoza ni watanzania wale wale walioipeleka NHIF ICU
2. Inalazimisha watu kujiunga nayo: Wastaafu, wenye magari, wanafunzi wa vyuo vikuu lengo likiwa kuongeza mapato na siyo kuwapa nafuu ya gharama za afya.
3. Sisi tuliopo Kibondo, Kigoma itatugharimu zaidi kupata huduma Muhimbili kuliko waliopo DSM.
4. Ni kutokana na sababu hizo ndiyo maana naiona Bima ya Afya kama muendelezo ule ule wa tozo kwa kujificha nyuma ya afya kwa wote.