Lengo kuu la Bima ya Afya kwa Wote inayopendekezwa ni kwa Serikali kukusanya mapato zaidi

Tangu tupate uhuru, serikali ya Tanzania haijawahi kuwa na nia njema kwa wananchi wake; kisiasa, kiuchumi, wala kiafya.

Kodi tunazolipa hazitumiki kuinua hali ya maisha ya wananchi bali kuneemesha viongozi na ndugu zao. Kwa mfano; serikali kununua gari la Tshs 400m kwa ajili ya mkuu wa wilaya ni matumizi mabaya ya kodi zetu.

NHIF iliyopo sasa ipo taabani kifedha si kwa sababu watu hawachangii bali ufisadi!

Pamoja na serikali kuipigia promo Bima ya Afya kwa wote kwamba itakuwa mkombozi kwa afya ya wananchi, naiona vingine:

1. Watakaoiongoza ni watanzania wale wale walioipeleka NHIF ICU
2. Inalazimisha watu kujiunga nayo: Wastaafu, wenye magari, wanafunzi wa vyuo vikuu lengo likiwa kuongeza mapato na siyo kuwapa nafuu ya gharama za afya.
3. Sisi tuliopo Kibondo, Kigoma itatugharimu zaidi kupata huduma Muhimbili kuliko waliopo DSM.
4. Ni kutokana na sababu hizo ndiyo maana naiona Bima ya Afya kama muendelezo ule ule wa tozo kwa kujificha nyuma ya afya kwa wote.
Hiyo Bima bora iletewe wawekezaji tu binafsi siona kama ina tija yoyote
 
Na hiyo bima ya NHIF ikiwa lazima, ni nini hatima ya bima zingine nyingi zilizopo na ambazo ndio priority ya wengi?
 
Bima ya afya aitolewi na NHIF pekee tafuta bima nzuri kwaajiri yako na familia yako bima ni muhimu sana unaongea hayo nadhani ujawahi kuuguza
Bima inayoweza kutibu magonjwa mengi makubwa huwa ni gharama sana, kwa umaskini wa Hawa watanzania wengi hawaiwezi. Nchi ina waajiriwa mil 2 tu hii, usisahau hilo
 
Dada hicho ki thread chako kina tofauti ipi na unachoongea Sasa hivi?

Usipende kuropoka hovyo 👇

Dada zako ni chawa wenzako. Nikukumbushe tena mmeaswa kujibu Kwa hoja ambazo bahati mbaya hamna.

Hayupo anayepinga bima. Ila bima ya shuruti yenye malengo ya wazi ya kukusanya pesa ili kupata faida tena kutoka kwa walengwa wasio wagonjwa ni ukakasi mtupu.

Kwamba Kwa kujihakikishia kupata faida serikali itawalazimisha watu wote kukata bima.

Si ilazimishe watu wote wacheze tatu mzuka, Biko, karata tatu au upatu ili ipate faida?

Kwamba yenyewe kuwekeza kutokea kwenye kodi zetu aah aah. Hawataki kuwajibika ila kulamba asali.

In short ni wa nini hawa?
 
Bima ya afya aitolewi na NHIF pekee tafuta bima nzuri kwaajiri yako na familia yako bima ni muhimu sana unaongea hayo nadhani ujawahi kuuguza
Mstaafu hana chaguo la bima ya afya. Serikali itakata michango ya bima ya afya kwenye pension yake juu kwa juu apende asipende hata.. akihamia burundi
 
Na hiyo bima ya NHIF ikiwa lazima, ni nini hatima ya bima zingine nyingi zilizopo na ambazo ndio priority ya wengi?
Nia ya Serikali ni kuwaondoa hao bima binafsi ili abaki peke yake. Implications: kukusanya mipesa mingi ya kufisadi.
 
Tangu tupate uhuru, serikali ya Tanzania haijawahi kuwa na nia njema kwa wananchi wake; kisiasa, kiuchumi, wala kiafya.

Kodi tunazolipa hazitumiki kuinua hali ya maisha ya wananchi bali kuneemesha viongozi na ndugu zao. Kwa mfano; serikali kununua gari la Tshs 400m kwa ajili ya mkuu wa wilaya ni matumizi mabaya ya kodi zetu.

NHIF iliyopo sasa ipo taabani kifedha si kwa sababu watu hawachangii bali ufisadi!

Pamoja na serikali kuipigia promo Bima ya Afya kwa wote kwamba itakuwa mkombozi kwa afya ya wananchi, naiona vingine:

1. Watakaoiongoza ni watanzania wale wale walioipeleka NHIF ICU
2. Inalazimisha watu kujiunga nayo: Wastaafu, wenye magari, wanafunzi wa vyuo vikuu lengo likiwa kuongeza mapato na siyo kuwapa nafuu ya gharama za afya.
3. Sisi tuliopo Kibondo, Kigoma itatugharimu zaidi kupata huduma Muhimbili kuliko waliopo DSM.
4. Ni kutokana na sababu hizo ndiyo maana naiona Bima ya Afya kama muendelezo ule ule wa tozo kwa kujificha nyuma ya afya kwa wote.
Hebu nipe ufafanuzi na ushahidi ya kuwa NHIF imefilisika, pili hebu nielezee wewe bima ya afya kwa wote unavyojua imeelezewa itatolewa kwa mfumo gani. Kama huwezi kujibu hayo maswali basi wewe ni mtu usiyejua unachotaka kututaarifu bwana mkubwa. Watanzania kwa story za vijiweni, nawakubali.
 
Biashara ya bima hufanywa Kwa kumshawishi mteja (kumtongoza). Jiunge nasi Kuna faida kadhaa. Kwenye process faida hupatikana.

Biashara hii haifanywi Kwa kuwaambia watu jiungeni nami ili wachache nitawafidia nyingine zote ni faida yangu.

Hata nguvu ya Biko hawasemi zawadi ni sehemu ya michango yenu wenyewe.

Walamba asali mmetumbua hadi sasa mmejisahau. Mnataka hadi kulazimisha watu kujiunga hata na upatu ili mpate faida. Huoni hapa tulipo ni kama tunataka kulazimishana kucheza Biko kiaina?

Hivi tozo na kodi zetu hazina cha kufanya na ustawi wetu ila wenu?

Angalizo: mstufanye kuwa hatuna elimu ati kuwa wenye elimu ni nyie tu.
Chief nakweli bado huna elimu. Haki ya Mungu, hujawahi kuona watu vijijini wakiambiwa waende Muhimbili, Bugando au Benjamin mkapa kwamatibabu ya kibingwa. Utalia. Ugonjwa usikiage tu kwa wenzako nakama hujawahi ishi mikoani karibu uone. Cancer, kisukari na magonjwa ya moyo yamewafikia wazee wetu wengi na vijana wengi walio kijijini nakujitibu hawajui waanzie wapi. Boss, ngoja tuangaliane tu mengine mpaka yakukute tu
 
Na hiyo bima ya NHIF ikiwa lazima, ni nini hatima ya bima zingine nyingi zilizopo na ambazo ndio priority ya wengi?
Ndio maana mnaambiwa msome hiyo bima ya afya kwa wote itaoperate vipi. Nanikakwambia NHIF ndiyo msimamizi wa bima ya afya kwa wote!!
 
Nia ya Serikali ni kuwaondoa hao bima binafsi ili abaki peke yake. Implications: kukusanya mipesa mingi ya kufisadi.
Bima ya afya kwa wote sio NHIF, ndio maana nakwambia idadavue sera ya bima afya kwa wote ndio nitajua kuwa unaelewa unachokisema. Tuache ushabiki tutaaibika sana.
 
Unachoongea kuhusu ufisadi ni kweli ni tatizo katika mfuko wa NHIF. Lakini bima ya afya inayosimamiwa na serikali ni nzuri na ni muhimu. Makampuni ya binfasi yanakamua zaidi. Serikali ilifanya jambo jema sana kuanzisha NHIF.

Kwa hiyo ukiona afya ni jambo la muhimu kwako na uwezo wa kukata bima ya NHIF unao kata. Hakuna mfuko mwingine wa bima nchin Tanzania unaotoa thamani nzuri ya pesa zaidi ya NHIF.

Kutibiwa sio mpaka uende Muhimbili. Magufuli alishasambaza huduma maeneo mengi. Kuna hospitali nyingi za kisasa za Rufaa alijenga kwenye mikoa mbalimbali.
Magufuli alijenga hospitali zipi ww 😂😂😂😂😂 acha ndoto za mchana huduma zinazotolewa kwenye hizo hospitali ni useless kabisa
 
Chief nakweli bado huna elimu. Haki ya Mungu, hujawahi kuona watu vijijini wakiambiwa waende Muhimbili, Bugando au Benjamin mkapa kwamatibabu ya kibingwa. Utalia. Ugonjwa usikiage tu kwa wenzako nakama hujawahi ishi mikoani karibu uone. Cancer, kisukari na magonjwa ya moyo yamewafikia wazee wetu wengi na vijana wengi walio kijijini nakujitibu hawajui waanzie wapi. Boss, ngoja tuangaliane tu mengine mpaka yakukute tu

Umesoma vizuri kuelewa tunachoongelea lakini ndugu?

Tofautisha bima na malengo ya wazi ya bima hii kama ambavyo bila aibu tunaambiwa.

https://www.jamiiforums.com/threads...a-serikali-msitake-faida-tu-wekezeni.2052039/

Hatupingi bima bali tunapinga bima iliyojilekeza kwenye faida tu ya mwenye nayo.

Kuhusiana na kubwabwaja kuhusiana na elimu za watu:

"Kushandinishana elimu labda kama kila mtu aweke CV yake hapa tuone."

Usishangae kukuta usiyeelimika au mwenye elimu duni zaidi ni wewe ndugu.

Zaidi sana sijui hilo linakuja je hapa.
 
Umesoma vizuri kuelewa tunachoongelea lakini ndugu?

Tofautisha bima na malengo ya wazi ya bima hii kama ambavyo bila aibu tunaambiwa.

Hatupingi bima bali tunapinga bima iliyojilekeza kwenye faida tu ya mwenye nayo.

Kuhusiana na kubwabwaja kuhusiana na elimu za watu:

"Kushandinishana elimu labda kama kila mtu aweke CV yake hapa tuone."

Usishangae kukuta usiyeelimika au mwenye elimu duni zaidi ni wewe ndugu.

Zaidi sana sijui hilo linakuja je hapa.
Ndio nikakuuliza umesoma sera ya bima ya afya kwawote inavyooperate. Acha ushabiki boss. Naunajua nini maana ya bima ya afya??? Unajua hayo malengo yamekadiliwa kutokana na takwimu gani chief au umekariri kila kitu ni wizi. Yaani mtanzania anaweza kuwa hajui bases ya kitu lakini akakipinga au kukisema bila kujua😂😂😂. Yaani hujui malengo uliyoyasikia hukujaribu kuuliza kwanini waliyaweka malengo hayo bali unakimbilia kupinga. Unajua hii bima ya afya hapa Tanzania ni rafiki sana nahaiendi kibiashara. Unajua operation cost chief inayotumika per month acha per year kulipa zahanati, vituo vya afya na hospitali kila mwezi na bima. 😂😂😂😂 chief, ninachokwambia tu acha propaganda utaumia sana. Pili kama wewe ni mwerevu nenda kasome concept ya cost sharing kwaupanda wa health sector ni moja ya nguzo ya hiyo sekta. Isome vizuri ndiyo utajua maana ya bima. Acha propaganda
 
1. Unaelewa tofauti ya bima hii na malengo ya bima hii kama nilivyokutafadhalisha mara kadhaa hapo awali?

2. Tunaweza kujielekeza kwenye tatizo halisi kwa lengo la kujadiliana kistaarabu badala ya kuruka ruka huku na kule na kuitana majina ya ajabu ajabu hali hatujuani?

Labda tuanzie hapo?
 
Back
Top Bottom