Lengo kuu la Bima ya Afya kwa Wote inayopendekezwa ni kwa Serikali kukusanya mapato zaidi

Hiyo Bima bora iletewe wawekezaji tu binafsi siona kama ina tija yoyote
 
Na hiyo bima ya NHIF ikiwa lazima, ni nini hatima ya bima zingine nyingi zilizopo na ambazo ndio priority ya wengi?
 
Bima ya afya aitolewi na NHIF pekee tafuta bima nzuri kwaajiri yako na familia yako bima ni muhimu sana unaongea hayo nadhani ujawahi kuuguza
Bima inayoweza kutibu magonjwa mengi makubwa huwa ni gharama sana, kwa umaskini wa Hawa watanzania wengi hawaiwezi. Nchi ina waajiriwa mil 2 tu hii, usisahau hilo
 
Dada hicho ki thread chako kina tofauti ipi na unachoongea Sasa hivi?

Usipende kuropoka hovyo πŸ‘‡

Dada zako ni chawa wenzako. Nikukumbushe tena mmeaswa kujibu Kwa hoja ambazo bahati mbaya hamna.

Hayupo anayepinga bima. Ila bima ya shuruti yenye malengo ya wazi ya kukusanya pesa ili kupata faida tena kutoka kwa walengwa wasio wagonjwa ni ukakasi mtupu.

Kwamba Kwa kujihakikishia kupata faida serikali itawalazimisha watu wote kukata bima.

Si ilazimishe watu wote wacheze tatu mzuka, Biko, karata tatu au upatu ili ipate faida?

Kwamba yenyewe kuwekeza kutokea kwenye kodi zetu aah aah. Hawataki kuwajibika ila kulamba asali.

In short ni wa nini hawa?
 
Bima ya afya aitolewi na NHIF pekee tafuta bima nzuri kwaajiri yako na familia yako bima ni muhimu sana unaongea hayo nadhani ujawahi kuuguza
Mstaafu hana chaguo la bima ya afya. Serikali itakata michango ya bima ya afya kwenye pension yake juu kwa juu apende asipende hata.. akihamia burundi
 
Na hiyo bima ya NHIF ikiwa lazima, ni nini hatima ya bima zingine nyingi zilizopo na ambazo ndio priority ya wengi?
Nia ya Serikali ni kuwaondoa hao bima binafsi ili abaki peke yake. Implications: kukusanya mipesa mingi ya kufisadi.
 
Hebu nipe ufafanuzi na ushahidi ya kuwa NHIF imefilisika, pili hebu nielezee wewe bima ya afya kwa wote unavyojua imeelezewa itatolewa kwa mfumo gani. Kama huwezi kujibu hayo maswali basi wewe ni mtu usiyejua unachotaka kututaarifu bwana mkubwa. Watanzania kwa story za vijiweni, nawakubali.
 
Chief nakweli bado huna elimu. Haki ya Mungu, hujawahi kuona watu vijijini wakiambiwa waende Muhimbili, Bugando au Benjamin mkapa kwamatibabu ya kibingwa. Utalia. Ugonjwa usikiage tu kwa wenzako nakama hujawahi ishi mikoani karibu uone. Cancer, kisukari na magonjwa ya moyo yamewafikia wazee wetu wengi na vijana wengi walio kijijini nakujitibu hawajui waanzie wapi. Boss, ngoja tuangaliane tu mengine mpaka yakukute tu
 
Na hiyo bima ya NHIF ikiwa lazima, ni nini hatima ya bima zingine nyingi zilizopo na ambazo ndio priority ya wengi?
Ndio maana mnaambiwa msome hiyo bima ya afya kwa wote itaoperate vipi. Nanikakwambia NHIF ndiyo msimamizi wa bima ya afya kwa wote!!
 
Nia ya Serikali ni kuwaondoa hao bima binafsi ili abaki peke yake. Implications: kukusanya mipesa mingi ya kufisadi.
Bima ya afya kwa wote sio NHIF, ndio maana nakwambia idadavue sera ya bima afya kwa wote ndio nitajua kuwa unaelewa unachokisema. Tuache ushabiki tutaaibika sana.
 
Magufuli alijenga hospitali zipi ww πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ acha ndoto za mchana huduma zinazotolewa kwenye hizo hospitali ni useless kabisa
 

Umesoma vizuri kuelewa tunachoongelea lakini ndugu?

Tofautisha bima na malengo ya wazi ya bima hii kama ambavyo bila aibu tunaambiwa.

https://www.jamiiforums.com/threads...a-serikali-msitake-faida-tu-wekezeni.2052039/

Hatupingi bima bali tunapinga bima iliyojilekeza kwenye faida tu ya mwenye nayo.

Kuhusiana na kubwabwaja kuhusiana na elimu za watu:

"Kushandinishana elimu labda kama kila mtu aweke CV yake hapa tuone."

Usishangae kukuta usiyeelimika au mwenye elimu duni zaidi ni wewe ndugu.

Zaidi sana sijui hilo linakuja je hapa.
 
Ndio nikakuuliza umesoma sera ya bima ya afya kwawote inavyooperate. Acha ushabiki boss. Naunajua nini maana ya bima ya afya??? Unajua hayo malengo yamekadiliwa kutokana na takwimu gani chief au umekariri kila kitu ni wizi. Yaani mtanzania anaweza kuwa hajui bases ya kitu lakini akakipinga au kukisema bila kujuaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚. Yaani hujui malengo uliyoyasikia hukujaribu kuuliza kwanini waliyaweka malengo hayo bali unakimbilia kupinga. Unajua hii bima ya afya hapa Tanzania ni rafiki sana nahaiendi kibiashara. Unajua operation cost chief inayotumika per month acha per year kulipa zahanati, vituo vya afya na hospitali kila mwezi na bima. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ chief, ninachokwambia tu acha propaganda utaumia sana. Pili kama wewe ni mwerevu nenda kasome concept ya cost sharing kwaupanda wa health sector ni moja ya nguzo ya hiyo sekta. Isome vizuri ndiyo utajua maana ya bima. Acha propaganda
 

1. Unaelewa tofauti ya bima hii na malengo ya bima hii kama nilivyokutafadhalisha mara kadhaa hapo awali?

2. Tunaweza kujielekeza kwenye tatizo halisi kwa lengo la kujadiliana kistaarabu badala ya kuruka ruka huku na kule na kuitana majina ya ajabu ajabu hali hatujuani?

Labda tuanzie hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…