Lengo la dini ni nini?

mi nadhani lengo la dini ni kumpandikiza mtu woga na wasiwasi kwa kumwambia vitu vya kutisha ili watu wachache watawale dunia. angalia ukweli kuhusu siku ya hukumu, uwepo wa shetani na dhambi utagudua walioleta ayo haikua bahati mbaya ila ni mpango mkakati wa kumtawala mwanadamu mwenye macho aone na mwenye kusikia asikie
 
Kiranga uko wapi? Au ulisharudi kundini.
 
Last edited by a moderator:
Mtoa mada hauna tofauti na mimi. Nami nimezaliwa kwenye familia ya washika dini. Toka utoto hadi miaka 20 nafunzwa maswala ya dini. Lkn nimekuwa mtu mzima sasa, huwa najiuliza baada ya kufa kuna kuishi tena baada ya hapo? je roho yangu itaenda wapi? mbona nikilala usingizi sijielewi iweje nikifa nivae mwili mpya?
 

Ni msiba mkubwa kwa mwanadamu kutojua umuhimu wa dini.Dini ina kusudio la msingi kwa wanadamu.Mwenyezi Mungu hakutuumba tu na kutuacha twende hovyo kama mbuzi wasio na mchungaji.Akatupa na dini ili uwe mfumo/muongozo wa maisha yetu ili kufikia lengo lililokusudiwa.Sasa mwanadamu akiacha dini,ajue AMESHAPOTEA.Ni mada ndefu,nitaiweka hapa ili tutoane katika kiza kinene.
 

Hakika ni msiba mkubwa.Kwenye meseji yako nimegundua mambo matatu,kwanza hujui kama Mungu yupo au la,pili huamini kama mwanadamu kaumbwa na Mungu na hujui dhumuni lake la kutuumba.Ni maafa makubwa.Tatizo lako ni elimu ya dini huna.Naandaa mada za kuwaondoa kwenye ujinga huu hapa hapa Jamii Inteligence.
 
Na mimi nawaza tuuu...
Nilisha wahi fikiria kama wewe na majibu sikupata, lakini nilipo muuliza moja ya walimu wa dini ya kikristo kuhusu uwepo wa Mungu na uwezo wake pamoja na contradiction zake Alinijibu kwa swali JE UNAAMINI SHETANI YUPO?? (Akawaweka Sub question je unaamini Uchawi upo?? na Je UCHAWI ni ushetani au laa??
 


Hakuna jipya utakalo kuja nalo zaidi ya zile hadithi na ngano za kale za watu wa mashariki ya kati i,e wayahudi na waarabu...ambazo watu walishazishtukia kitambo.

Utaanza ku-quote vifungu vya biblia au quran ukifikiri hivyo vitabu vimeshishwa na mungu...kumbe ni wahuni tu wameviandika kwa utashi wao wa utamaduni na mazingira yao.

Anyway-lets wait and see.
 
kwani kuna ubaya gani wewe mwenyewe ukanieleza maana ya hilo neno? mimi sipo hapa ku-act kama najua kila kitu... mimi nakuruhusu unaweza kuendelea na kunielewesha unachoisi sikielewi.

ni kweli kabsa Deni, tupo hapa kueleweshana ,si kubishana.
IELEWEKE KWA WOTE.
 

Ndugu yangu IGWE,lengo langu ni kuleta hoja kwa mujibu wa quran na sio kumlazimisha mtu kuamini.Tujibidiishe kuutafuta ukweli,haya mambo yako wazi dana,tatizo hatusomi au tumeacha dini.
 
Aisee umelijibu hili swali muhimu vizur sana.. Truly Great thinker
 
Achana na dini pamoja na hilo limungu ambalo halipo,Jitambue mwenyew bac , Mbingu IPO within yourselves , Jesus is not the way to Heaven but yourself is the way to heaven thru self determination!! mwenzako mie Nitakapokufa tu naenda MAMBOSASA CITY ambayo ipo kule kwetu mbinguni na majengo yote ya kule ni meupe yote na nyasi za kijani kibichi mud a wote ,Kama mtafika kule heaven nawakaribisha sana MAMBOSASA CITY .Iliopo upande wa mashariki ya makao makuu ya Mbinguni!!!!
 
Mi naona wengi mnajibu swala la dini sana, wakati mtoa mada haelewi hata, kama kuna MUNGU... Mi nafikiri aeleweshwe kwanza uwepo wa MUNGU na uumbaji wake na kwanini alimuumba Lucifer(shetani) na bado akatuma mitume wake... akiyaelewa hayo hata dini hatalazimishwa atanyoosha njia kuitafuta dini ya kweli.
Nb. Dini sio tu kwenda kanisani au msikitini,
 
Dini ni jamii ya watu wenye shauli moja,imani moja,mlengo mmoja.kwangu mimi naichukulia dini kama sehemu ya kuwa wamoja na kutafuta kustarabiana tu kwa hofu ya siku moja kuna hukumu kwa mkosaji,ni vyema kuendelea hvyo coz inatuweka kua na amani,lakini ukweli ni kwamba kama mwanadamu yeyote mwenye ako na akili anajua nini ni dhambi na nini ni utakatifu,haihitaji dini kuogopeshana,hata mimi hua napata ukakasi kuambiwa nikizini na kupata raha ile ile aloiweka MUNGU eti kuna siku atanichoma moto mkali sifi wala sizimii na nitasikia maumivu hayo bila kikomo maisha yote,huu ni uongo uliopigiwa mstali.kweli yamkini yupo MUNGU ila waliokuja kusambaza dini pia walipitisha na uongo kadhaa ili watu wawe na hofu na wawe wapole.niishie hapa
 
Uwezi elewa radha ya tunda lililo ktk kinywa changu
sawa sawa leo unajaji uwepo wa MUNGU lakini tambua walikuwepo wengi waliokwisha kuuliza jambo hilo je unataka kutambua jibu walilopata....
kwa asilimia kubwa akili ya mwanadamu ndiyo umponza jaribu kutafuta mtu ambaye unamwamini anakuzidi hekima na maarfa muulze kuhusu uwepo wa MUNGU.
 
Hivi kwanini NASA hawakutengeneza chombo cha kugundua Mungu yuko wapi ??!!!.. kazi kuchunguza masayari .. si watengeneze chombo watutafutie huyu Mkuu kakaa kipande IPI...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…