Lengo mojawapo la bajeti ya mwaka huu ni kusomesha kwa wingi Wataalamu Fani na Ujuzi Adimu/Maalum, wazazi shaurini watoto vizuri shahada za kusomea

Kalaghabaho na ujuaji wako

Nimekushambulia kwenye baadhi ya nyuzi naona unajitutumua ili ionekane kuna mjadala fulani serious kuhusu bajeti, japo si vibaya ufanyavyo maana ndio wajibu wenu kama wanaccm. Huyo uliyemjibu kwa kejeli amesema jambo la kweli. Ni nadra sana mambo mengi yanayojadiliwa kwenye bajeti zetu kuwa na cosistance, haswa yenye muelekeo huo. Wangalau ambapo serikali inawakamua walipa kodi, hapo ndio hawayumbiyumbi. Hayo ni mengine ni kutake risk, nothing serious. Tuna uzoefu wa kutosha kwenye mambo hayo.
 
Kuna kozi inabidi zifutwe hapa TZ
Hapana Kuna watu wanazihitaji wao Kama wao mfano Kuna digrii ya uchoraji na Sanaa za maigizo huwa hazikosi wanafunzi hata mwaka mmoja na wanajilipia wao wanajua watazifanyia Nini .
 
Sema wewe Mimi hopes hazijafa nimeona fursa kibao ndani bajeti hiyo bajeti mipesa yote hiyo Kama wewe huoni fursa kwenye hiyo bajeti wewe hata Mungu hawezi elewa akusaidiaje
Mzee

No one is discussing this shit

Ukitaka kujua watu dont pay attention to this nonsense,check uzi za budget ya serikali ya kuanzia 2015 kurudi nyuma uone takwimu za uchangiaji uone!

Do not even compare!

Watu milioni 60 kama citizenry of this banana republic tayari walishajitoa na hizi maneno ambazo ni hela personal za mtu mfukoni maana hakuna accountability ya aina yeyote!

The government machinery and systems have been hijacked and destroyed singlehandedly na mtu mmoja!

Hakuna government essentially!

Yaani watu wapige rubber stamp kwenye budget halafu baada ya kutumia hakuna kuhoji even kuone hesabu za ukaguzi!

This is crime!
 
YEHODAYA,

Usome kwa mwaka mmoja? Shida ya bajeti zenu hazina projection ya miaka mingi. mwaka huu wako hapa mwaka mwingine wako kuleee. huoni utajikuta shule kila mwaka?
Waulize waliokimbilia kusoma petroleum engineering wako wapi leo, kamwe usisome kwa kufuata sera za CCM kwakua siku zote hua hazina dira wala mwelekeo.
No comment! Over.
 
Budget ya serikali ni budget ya serikali sio yako!
Hapa ndio nimekuelewa vizuri kuwa wewe Ni maskini wa kutupwa kazi ya bajeti ya serikali Ni kumwaga pesa kwa watu kupitia huduma mbali mbali inazohitaji iwe mafuta ya magari yake muuza mafuta utapata pesa,iwe miradi ya ujenzi ya serikali unajua tenda za vifaa vya ujenzi pesa hiyo,iwe ujenzi wa maabara unajua pesa ya ku supply vifaa vya maabara hiyo nk
Ukisikia bajeti za shule za bweni mapesa kadhaa unajua tenda ya chakula Cha watoto wa shule za bweni hiyo

Wewe maskini wa kutupwa hata ungekuwa na kibiashara Cha kueleweka ungejua role ya bajeti kukupa pesa wewe nadhani wewe utakuwa machinga au mfagia ofisi ya chadema

Wewe maskini bajeti ya serikali Ni yako unachotakiwa ujipange kwenda kuchukua hiyo pesa kwa kuangalia kwenye bajeti Kuna fursa gani na ujipangaje
 
mkuu ww inaonekana hauko Tanzania hii yetu utakuwa sehemu nyingine, pesa hizi zinatoka kwenye mfuko wa mtu mmoja nchi hii. kwani ni mara ngapi bajeti hata pesa zilizopangwa hazifiki katika idara husika ? kwa mataifa mengine yenye utawala bora ni sawa ila si hapa kwetu. " asomaye na afahamu"
 
MKUU umeongea ukweli mtupu. Kwa Kiasi kikubwa watanzania walio wengi hawajui kufuatilia Fursa ziko wapi.

Wanataka mpaka washikwe mkono na Serikali na kupelekwa mpaka Fursa zilizopo. Wengi ni walalamishi na wenye kushabikia vitu wasivyovijua.

Kama unataka kufanikiwa ni lazima uwe mdadisi sana wa mambo yanayofanywa na serikali. Pia kutafuta Taharifa za Fursa mbali mbali zilizopo na kuzichangamkia.

Sasa kama hutaki wewe shabikiatu chadema wakujaze maneno uvimbe na kuichukia Serikali ya chama cha Mapinduzi kumbe tatizo ni ujinga Wako wakuto kutafuta taharifa za Fursa na ukafanikiwa.
 
Blah blah blah blah

Nina hela kiasi kwamba sihitaji serikali iwe mteja wangu kwa chochote!

Siiuzi serikali chochote,I dont need uteja wao!

Hakuna hela ya bure,wakija kununua chochote kwenye kampuni yako ni mteja kama mteja mwingine yeyote na unawapa huduma,hawakupi hela bure na wala hutoi huduma bure....Give and take,hakuna msaada!

Blah blah blah blah!
 
YEHODAYA,

Usome kwa mwaka mmoja? Shida ya bajeti zenu hazina projection ya miaka mingi. mwaka huu wako hapa mwaka mwingine wako kuleee. huoni utajikuta shule kila mwaka?
Mkuu naomba kuunga mkono hoja yako kwa kutoa mfano halisi kipindi cha 2014/15 Petroleum and Gas was a talk if the town kwa wanafunzi wa kidato cha 6,kupelekea vijana wengi hasa vipanga kujagua kusomea kozi hizo....guess what 4 years later watu hawa wanalitambua vizuri joto la jiwe
 
mleta mada halijui taifa hili vizuri. watu wanaidai serikali kwa kazi walizofanya nazo miaka mitano nyuma sijui anaongea nn. jamaa anaona tumekaa kimya anatuona wajinga sana.
 
Fani hizo ni zipi bwashee?
 
Alamsiki,
Nitakurupuka hapa na sijasoma bajeti. Hili lieleweke.

Bajeti, kwa uelewa wangu ina malengo mengi, mengine yapoyapo tu na mingi inaleta fursa kama hoja za wakuu humu.

Bandiko hili halikubandikwa kuchambua bajeti wala kuonyesha mapungufu ya bajeti kama wengine wenu humu mlivyodandia...bandiko hili lina nia na limeelekezwa kwa "Wazazi" kama njia ya kuwa taarifu na kushauri.

Bandiko hili lina taarifa na ushauri kwa wazazi Watanzania, Wananchi na wanafunzi kwa ujumla kuhusu fursa zitakazotokea na "Lengo..." katika fani "Adimu" na "Maalum" kwenye bajeti kwa mfano, mikopo yenye riba nafuu n.k au hata kulipiwa na serikali au ajira za moja kwa moja baada ya masomo, na huu ni mfano tu, kwani hapo juu nimesema, sijasoma bajeti, na kushauri tu usome au usikilize kwa yatayojiri kuhusu fursa hizo.

Alikumhali, kuna genge la watu potofu, la watu wenye kujaza ujinga, la watu wajinga kwa kutambua na hata kutotambua ujinga wao, wanatamba,wanashambulia na kudhalilisha pamoja na kujenga taharuki. Niwasii, wacheni, mnajijua.

Moja ya sehemu nitayoshauri ni "Cyber Security"

Wazazi changieni katika maono ya Vijana wetu wa kesho pamoja na kuzingatia umuhimu wa uzalendo kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Shehena hii itatusaidia katika uchumi na medani kwa Taifa na ushindani Kimataifa.

Aluta Continua
 
,
Moja ya sehemu nitayoshauri ni "Cyber Security"
Uko sahihi cyber security Ni eneo adimu na dunia nzima mashirika binafsi na serikali nyingi wanawataka Sana

Vita ,udukuzi nk uko kwenye cyber wars .

Vijana na wazazi wenye watoto waelekeze uelekeo huo hizo Ni moja ya skill adimu Sasa hivi ulimwenguni

Degree za Cyber security sasa hivi Ni hot cake
Ushauri mzuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…