Alamsiki,
Nitakurupuka hapa na sijasoma bajeti. Hili lieleweke.
Bajeti, kwa uelewa wangu ina malengo mengi, mengine yapoyapo tu na mingi inaleta fursa kama hoja za wakuu humu.
Bandiko hili halikubandikwa kuchambua bajeti wala kuonyesha mapungufu ya bajeti kama wengine wenu humu mlivyodandia...bandiko hili lina nia na limeelekezwa kwa "Wazazi" kama njia ya kuwa taarifu na kushauri.
Bandiko hili lina taarifa na ushauri kwa wazazi Watanzania, Wananchi na wanafunzi kwa ujumla kuhusu fursa zitakazotokea na "Lengo..." katika fani "Adimu" na "Maalum" kwenye bajeti kwa mfano, mikopo yenye riba nafuu n.k au hata kulipiwa na serikali au ajira za moja kwa moja baada ya masomo, na huu ni mfano tu, kwani hapo juu nimesema, sijasoma bajeti, na kushauri tu usome au usikilize kwa yatayojiri kuhusu fursa hizo.
Alikumhali, kuna genge la watu potofu, la watu wenye kujaza ujinga, la watu wajinga kwa kutambua na hata kutotambua ujinga wao, wanatamba,wanashambulia na kudhalilisha pamoja na kujenga taharuki. Niwasii, wacheni, mnajijua.
Moja ya sehemu nitayoshauri ni "Cyber Security"
Wazazi changieni katika maono ya Vijana wetu wa kesho pamoja na kuzingatia umuhimu wa uzalendo kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Shehena hii itatusaidia katika uchumi na medani kwa Taifa na ushindani Kimataifa.
Aluta Continua