Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
KUNA ZOEZI LA KUHAKIKI WANACHAMA HAI, NI UTARATIBU WA KAWAIDA KWA HESABU YA HARAKA HARAKA WANA CCM TUMEFIKIA 12.5 MILIONI.Leo asubuhi Mjumbe wa nyumba 10 amekuja kwangu kutaka kuniorodhesha kama nina kadi ya CCM. Mimi nikamuuliza nani kakutuma uorodheshe watu? Unawaorodhesha kwa sababu gani? Yeye kanijibu kuwa ametumwa na Katibu wa CCM kata kuorodhesha watu na kadi zao.
Jibu nililompa ni kuwa mimi sina chama na ni raia mwema hapa mtaani. Nikakataa kuorodheshwa na akaondoka. Nauliza kuna tatizo gani? Mbona CCM inaorodhesha watu karibu na uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Jambo hili linatakiwa likemewe kwa nguvu zote.
