Natoa mchango kupitia experience yangu binafsi (ndoa ya DC, watoto dini ya baba, Muslims)
Shida kubwa ya hii ndoa ni watu wanaowazunguka (binafsi baba mkwe wangu na robo tatu ya ndugu zake hawakushiriki chochote kilichofuata baada ya mahari, send off hakuja wala harusi hakuja, ingawa harusi ilikua ndogo tu wageni hawakufika 150)
Kilichosaidia mimi binafsi nilikubali watoto wafate kwa baba ila mimi nisiguswe kwa chochote, siwezi kuwa (Muslim, msabato wala mkatoliki)
Nilichojifunza, Muslims wana inferiority complex sana hata awe na shule, mwenzangu kabla ya ndoa nilikua naona kabisa yupo radhi tufanye sogea tukae kuliko kufunga kwa DC na sio kuachana,
Ila mimi niliweka msimamo either kwa DC au kila mtu apambane na hali yake.
Kwetu niliwekwa vikao sababu ukoo mzima hakuna ndoa ya DC, kuna ndoa za kikristo na chache za kiisilamu(less than 3) ambazo ndugu zangu wamebadili, nilikua tu muwazi sitoweza na kama hawapo tayari kuniaga kwa send off basi ntaolewa tu kwa DC bila sherehe muhimu mahari wamechukua
Kilichotubea sisi hatujakutana ukubwani sana, tumekutana umri ambao tushajitambua potential ya kila mmoja na tushaona namna gani tunaweza kubuild empire pamoja, so hasara za kuachana zilikua kubwa kuliko za kuendelea
Binafsi sijutii maamuzi yangu, mwenzangu siwezi kuusemea moyo, ila kama anajuta itakua ni roho ya kibinafsi sababu kiimani mimi ndo nimepoteza sana kuliko yeye
mtihani mkubwa ni kwamba, watoto wanavyozidi kukua wanakua attracted more to christianity sijui kwanini ila imetokea tu sababu huwa nawaona especially mkubwa kwasababu nikiwa nakula live sermons youtube anavutiwa sana na anapenda kuuliza maswali
KEY POINT YA MSINGI: SISI HATUKUWEKA WAZI KAMA KUNA UWEZEKANO WA KUTOFUNGA NDOA YA KIISILAMU KABLA YA MAHARI, MPAKA MILA ZINAFANYIKA KILA MTU ALIASSUME NTABADILI DINI (NA KUNA NDUGU ZANGU WALIUMIA SANA SABABU KIUKWELI KWETU MUSLIMS HAWAPENDWI ILA HAKUNA MCHUMBA WA HIYO DINI ALOWEKEWA NGUMU KUOA KAMA BINTI AMEKUBALI)
Kijana kama haujaingia kwenye huu mtego hakikisha wote mna akili timamu, mkubaliane watoto wanamfata nani otherwise VITA NI KUBWA ITAWASHINDA, MTAPOTEZEANA MUDA NA MBAYA ZAIDI WATOTO WATAHANGAIKA