Leo dola moja ni sawa na 2290. Kweli uchumi unakuwa

Leo dola moja ni sawa na 2290. Kweli uchumi unakuwa

Katika mambo yanayokera,kutia hasira na kutia kinyaa ndo haya

Tanzania asilimia kubwa ya bidhaa tuna-import nje (kununua nje ya nchi) sasa hili swala la dola kupanda dhidi ya shilingi kunazidisha mfumuko wa bei hapa nchini

Hili jambo linapigiwa kelele mno lakini serikali yetu inayojidai ni sikivu hili wamelikalia kimya Bot nao kimya?

Miaka mitatu dola kupanda dhidi ya shilingi kutoka 1500 hadi leo karibia 2300 ni jambo la kutisha sana hii ni fedheha mno na inaonyesha uchumi wa nchi umedorora

Kwa hii hali mtawaweka wapi vijana wengi walojiajiri kwenye kununua bidhaa nje? (Importers)

Mtawaweka wapi wananchi kutokana na mfumuko wa bei?

Kwanini tusiruhusu free exports watu wauze nje free bila makato ili walau shilingi ipate thamani na mfumuko wa bei uondoke na wananchi wafurahie unafuu wa bidhaa kwa bei ya chini?View attachment 925952
Unreliable source. Aja kuleta ujinga stupiddity
 
Exchange rate sahihi ni za commercial Bank

CRDB = 2,344
NMB = 2,322

Bank kuu bado wanalazimisha rate isomeke 2,290
Jamani[emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] kama ni hivi we are dying
 
Exchange rate sahihi ni za commercial Bank

CRDB = 2,344
NMB = 2,322

Bank kuu bado wanalazimisha rate isomeke 2,290
Tunaofanya transctions kwenda nje na kupokea hela kutoka nje tunakuelewa kwa hii rate yako... Every time nikibuy us dollars exchange kuwa inakaribia 2400...
 
una uhakika? mi nipo nmb now.. jifunze kutofautisha buying and selling unavyosoma rate
Halafu let me tell me tell u one thing... hizo exchange rate mnazotuandikia huwa zinakuwa different kabisa while mtu akifanya transaction mfano kama mfano kama buy/sell=2260/2300 wakati wa kufanya transction expect sell kuwa higher kuliko hiyo iliyoko hapo na buy kuwa low kuliko hiyo iliyoko hapo... huo ndo uchuro wa banks za kibongo...
 
rate sahihi ni ile ya bureau de change ambayo unaweza ukaifanya hela yako ikiwa $ kwaajili ya matumizi ya ndani au ya nje.
FB_IMG_1541699367214.jpg
 
Unreliable source. Aja kuleta ujinga stupiddity
Are you gone mad? Kuna kitu au data zimepikwa hapa?kwani dola dhidi ya shilling haijapanda? Stupidity imekujaa wewe usiyeelewa chochote dunia hii
 
Hivi Tanzania au benki zetu zinaruhusu ufungue akaunti ya fedha za kigeni hata kama huna chanzo cha mapato ya hiyo fedha za kigeni? Hawatauliza hii akaunti ya dola unayofungua pesa za kuhifadhi chanzo chake utakuwa unakitoa wapi? Mfano ukisema unafanya kazi, je unalipwa kwa dola? naomba kufahamu kuhusu hili....
Hakuna maswali yoyote Mkuu. Utaratibu au namna ya kufungua hiyo dollar Acc, ni sawa tu na jinsi ulivyofungua hiyo Acc ya kawaida...

#Kazi ni kwako
 
Nyie tafuteni hel bwna. Ukiwa na mpunga wa kutosha hzi exchange rate si issue sana. Siku zote tzs unashuka thamani tangu wakati wa mwalimu J.K Nyerere mpaka J.Kikwete. Kikwete wakati anaingia madarakani alikuta exchange rate ya approximately 1usd= 900 tzs na ameondoka madarakani exchange rate ikiwa almost 1usd = 2000 tzs. lakini mlikaa kimya kwa vile mianya ya upigaji ilikuwa imejaa tele.
 
Ukiingi kwenye tovuti ya benki kuu na ofisi ya taifa ya takwimu, unakutana na ripoti kadha wa kadha wanazoziandaa kuhusu uchumi wa nchi. Kuna tovuti nilikuta wameandika TZS currency depreciation against US dollar ni 2.4%.

Siko mtaalamu sana wa mambo ya uchumi ila hii ratio ina maana kuwa shilingi iko imara kulinganisha na dola ya kimarekani ambapo mwanzo ratio ilikuwa 7%. Sasa turudi kwenye uhalisia, shilingi dhidi ya dola ya kimarekani inaimarika au inazidi kuzorota???

K' Matata.
Jukwaa lako ni kule MMU ndio panaendana na wewe, huku utaishia kuaibika.
 
Are you gone mad? Kuna kitu au data zimepikwa hapa?kwani dola dhidi ya shilling haijapanda? Stupidity imekujaa wewe usiyeelewa chochote dunia hii
Usihangaike kujibu machizi ya ccm
 
  • Thanks
Reactions: etb
Bank zote za kibongo zinafanya hyo huduma?.. Pili mpk uweke kwnye fixed account ama hta accnt ya kawaida tuu?
Mkuu CRDB wanafanya na ni acc ya dola inaweza kuwa ya kawaida tu sio fixed acc tena makato madogo sana
.
BancABC pia ipo tena hawa unatakiwa ufanye deposit ya $50 tu hakuna makato ya kila mwezi. Unaenda kufungua acc siku hiyo hiyo unapata VISA Debit Card na baada ya masaa machache unaweza kufanya manunuzi popote duniani kwa VISA.

Zipo bank zingine kibao hapa nchini wana huduma ya acc ya fedha za kigeni kama dola au Euro bila mashariti mengi. Mimi nimekupa muongozo kwa hizo mbili ambazo nina uzoefu nazo wa kuzitumia.
 
Tunza fedha katika account maalum iwe kwa USD na sio TZS.
Ili utakapo kuwa unatoa hiyo fedha utapewa kwa rate ya wakati huo.
Account ya dola ni gharama sana kuifungua na kuiendesha, mi ningemshauri anunuwe dola kutunza nyumbani kwake
 
Nchi nyingine account ni moja tu. Ila unaweza kuweka dola na ukachukua dola, na currency nyingine zozote. Ukitumiwa pesa kwa dola automatically zinaingia kwenye account ya dola. Ila bongo unatakiwa kuwa na akaunti lukuki kama line za simu.
 
Account ya dola ni gharama sana kuifungua na kuiendesha,
Kuna benki zingine hakuna ghalama yeyote ya kuiendesha.
Iko hivi, chukulia mfano umeweka US $50 kwenye account yako, Baada ya muda mfano mwaka mmoja, kiasi utacho toa ni hiyo hiyo US $50
- Hakikisha unapata taaarifa za account na vigezo/ masharti kwa benki tofauti tofauti.
- Hakikisha unapata taarifa ya kutosha kuhusua aina ya account katika benki husika unayotaka kufungua.
- Benki zingine ni kweli kuna makato kwa kila mwezi na kila unapo toa fedha yako.
mi ningemshauri anunuwe dola kutunza nyumbani kwake
Hapana
Sikubaliani na hii hoja.
 
Back
Top Bottom