Leo dola moja ni sawa na 2290. Kweli uchumi unakuwa

Leo dola moja ni sawa na 2290. Kweli uchumi unakuwa

kwenda chini pia kingine si tuna import tuu unadhani uchumi wetu utakuwaje? kunahaja ya kuwa na uwiano hata ka hatutafika ila japo tuweze kutubutu
 
Exchange rate sahihi ni za commercial Bank

CRDB = 2,344
NMB = 2,322

Bank kuu bado wanalazimisha rate isomeke 2,290
Hizo rate ulizotaja ni kama wewe una Tshs na unataka "kununua" dollar. Kama una dollars na unataka kuchenji upate Tshs, rate za bank zitakuumiza mno - ni za kinyonyaji. So, rate "sahihi" zipo kwa bureau de changes.
 
Exchange rate sahihi ni za commercial Bank

CRDB = 2,344
NMB = 2,322

Bank kuu bado wanalazimisha rate isomeke 2,290
Commercial Bank hawana rate sahihi kwa sababu FOREX siyo kazi yao maana price zao ziko juu kwa sababu si kazi yao kubadilisha fedha mabank yana discourage kwa kuweka exchange rate za kuumiza. Bureau de change ama maduka ya kubadilishia fedha ndiyo yana Exchange rate sahihi.
 
Mnavyolaumu utadhani dolla kupanda imeanza jana..awamu zote hakujawahi kutokea dolla ikashuka. Walishindwa wale huyu atawezea wapi
 
Kuna vitu watu mnachanganya hapa rate sahihi ni zile ambazo BOT wanaziweka mabank na bureau wanafanya biashara hivo lengo ni kupata faida na ndiyo maana unakuta rate zao ziko juu kidogo kwa lengo la kutengeneza faida

hii ipo tofauti kidogo kwa bureau wao rate zao huwa za chini kulinganisha na mabank sababu ya competition iliyopo hivo wanashusha rate ili kuweza kupata wateja wakutosha

Na hizo rate ambazo ziko displayed kwenye board za mabank zio za kila mtu kuna customer ambao hupewa rate nzuri zaidi ambazo zinakaribia na za BOT sababu wao huuza au kununua kiasi kikubwa cha dollar

hizo rate za google zisiwatishe na kuja apa chafu taswira ya uchumi wetu

nawasilisha
 
Ndoto yangu ya kuagiza gari japan inazidi kuyeyuka.

Na ukifanikiwa kuajiza unakuja kupigwa kodi utafikiri wewe ni mtoto wa mama akambo!! Yaani full kukomeshwa huku bara. Jana nilikuwa naongea na mdau anasema Znz gari kama ist huku 12m wakati kwao unapata kwa 8.5m kuagiza mpaka unaitoa
 
Miamala niliyofanya leo rate ni
1usd = TZS 2,384.12

Kwenye hizi e_site
- ALIEXPRESS
- SUGARDENIM
- ACNE

Kwa amazon rate ni
1usd = 2,435
View attachment 926040
Leo AMAZON

1usd = TZS.2,445.3
1542337946500.png
 
Leo 18.11.2018 @08:45am

Paypal Rate

US $1 = TZS. 2,393.939393939394
 
Fungua dola account FNB
- Haina makato
- Kiasi utakachoweka, ndio utakachotoa
- Minimum kiasi cha kuweka ni kuanzia US $100

Account ya $ ni nzuri kuweka fedha ambayo huna matumizi nayo kwa muda.

Fika bank iliyokaribu nawe, ulizia uwepo wa $ account, uliza TOS zao.
Je katika iyo ya akaunt ya $ kwa Fnb,je naweza nikaifungulia Fixed Account dolla
 
Je katika iyo ya akaunt ya $ kwa Fnb,je naweza nikaifungulia Fixed Account dolla
Ndio waweza kufanya hivyo.
- Fedha yako itakuwa fixed, kama umeweka 1,000, mwisho wa siku utatoa kiasi hicho hicho $1,000
- Faida utakayoipata ni kutokana na kuporomoka kwa TZS
- Mfano uliweka rate ya $1 ikiwa 2,250 na ukitoa mfano (baada ya mwaka) rate ikawa ni $1 ni TZS 2,380
- Utaona hapo faida ni tofauti ya 2,380 - 2,250 = TZS.130 zidisha kwa $1,000
- Hitimisho: Nifaida kuhifadhi fedha kwa fedha ya kigeni USD na hii GBP
 
Ndio waweza kufanya hivyo.
- Fedha yako itakuwa fixed, kama umeweka 1,000, mwisho wa siku utatoa kiasi hicho hicho $1,000
- Faida utakayoipata ni kutokana na kuporomoka kwa TZS
- Mfano uliweka rate ya $1 ikiwa 2,250 na ukitoa mfano (baada ya mwaka) rate ikawa ni $1 ni TZS 2,380
- Utaona hapo faida ni tofauti ya 2,380 - 2,250 = TZS.130 zidisha kwa $1,000
- Hitimisho: Nifaida kuhifadhi fedha kwa fedha ya kigeni USD na hii GBP
Mfano nikiwa na milioni Mbili,nikataka niifanyie biashara ya kubadilisha shilingi kwenda dolla,kisha ikipanda niende kuibadilisha kurudi tsh je inawezekana
 
Mfano nikiwa na milioni Mbili,nikataka niifanyie biashara ya kubadilisha shilingi kwenda dolla,kisha ikipanda niende kuibadilisha kurudi tsh je inawezekana
Ndio. Inawezekana.
- Unapoweka au kutoa rate inayotumika ni ya wakati huo.
 
Wadau utalii wazungumzia BoT kufunga maduka ya kubadilisha fedha

By
Mtanzania Digital
-
November 22, 2018
0

113



Share














ELIYA MBONEA Na ABRAHAM GWANDU-ARUSHA
WAKATI maduka ya kubadilishia fedha Arusha yakiwa bado yamefungwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutokana na operesheni ya kukagua biashara hiyo juzi, wadau wa utalii jijini humo wamezungumzia hatua hiyo na maendeleo ya sekta ya utalii.
Mfanyabiashara mkubwa katika sekta ya utalii mkoani hapa Wilbert Chambulo, jana aliliambia gazeti hili kuwa hatua ya BoT haijaathiri sekta ya utalii kwa vile watalii wanaweza kupata huduma hiyo kwenye hoteli wanazofikia.
Chambulo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (TATO) aliyewekeza katika Kampuni za Kibo, Tanganyika, hoteli na kambi hifadhi tofauti nchini, alisema yeye binafsi anakubaliana na utaratibu uliotekelezwa na BoT.
“Kwa ujumla sekta ya utalii haijaathiriwa… Kama athari zipo basi walioathirika ni wale wafanyakazi wa sekta ambao ni Watanzania waliotaka kubadilisha fedha za kigeni wapate shilingi.
“Utaratibu huu, binafsi nakubaliana nao…hata kama ikiwezekana maduka yote yakafungwa na sheria ikatulazimisha kwenda kubadili fedha BoT bado itakuwa ni sahihi.
“Umeona wapi Dola ya Marekani imekuwa ya shida hapa mjini? Nenda kwa wachuuzi wa bidhaa zinazouzwa kwa wageni…wote wanatumia dola. Hoteli za kawaida, shule mpaka migahawa ya kawaida nao wanachaji kwa Dola,” alisema.
Chambulo ambaye pia anamiliki duka la kubadilisha fedha eneo la Mnara wa Saa jijini hapa, alisema operesheni ilichelewa kufanyika kiasi cha kuruhusu wafanyabiashara kulipisha wanunuzi wa huduma mbalimbali kwa kutumia fedha za kigeni.
“Kitu hiki ni aibu na tusi kwa sarafu yetu ya Tanzania, tofauti na jirani zetu sisi tulifanya uzembe. Ukienda Kenya au Afrika ya Kusini hawaruhusu haya mambo holela holela.
“Ukipata dola zako kabadilishe ukajieleze ulivyozipata ndipo uende kulipia huduma unayotaka, si vinginevyo,” alisema Chambulo.
Kuhusu madai kuwa BoT iliondoka na fedha za watalii kwa baadhi ya maduka, alisema madai hayo hayana ukweli kwa sababu watalii hawabebi fedha taslimu bali hulipia huduma zao moja kwa moja kupitia wakala.
“Wengine wanasema eti watalii wanahaha, huo ni uwongo, watalii watahaha vipi wakati wameshalipa huduma zao zote za safari?
Hata kama wana kiasi kidogo cha fedha taslimu wanabaki nazo ndizo wanazolipia ‘tip’ baada ya safari au ununuzi wa vitu mbalimbali na hulipa kwa fedha za kigeni,” alisema.
Nao baadhi ya madereva wa watalii walisema pamoja na umuhimu wa hatua hiyo, bado kwao kulikuwa na usumbufu hususani walipotaka kuacha fedha za matumizi kwa familia zao.
“Hatua si mbaya isipokuwa lilileta usumbufu kwetu, madereva tuliokuwa tunasafiri na wageni. Kama unavyojua ukiwa na familia huwezi kusafiri bila kuiachia familia hela ya matumizi,” alisema Alex Murro na kuongeza:
“Tulipata usumbufu, familia zetu ziliathirika kwa sababu tulikuwa na fedha za kigeni na hapakuwa na mahali pa kubadilisha”.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA), Walter Maenda, alipoulizwa kuhusu wanachama wake walioathirika na hatua hiyo, alisema hakuwa na taarifa yoyote inayoelezea kufungiwa maduka yao.
“Sijapata taarifa zozote kutoka BoT kwa nini hawa wamefungiwa maduka yao, asante sana,” alisema Maeda na kukata simu.
MTANZANIA lilimtafuta kwa simu Mkurugenzi wa BoT Tawi la Arusha, Charles Yamo kufahamu idadi kamili ya maduka yaliyokumbwa na operesheni hiyo lakini alisema bado ni mgeni na ana wiki moja tu kwenye ofisi hiyo.
Wadau utalii wazungumzia BoT kufunga maduka ya kubadilisha fedha Wadau utalii wazungumzia BoT kufunga maduka ya kubadilisha fedha | Mtanzania via Mtanzania
 
Back
Top Bottom