Leo huenda ikawa siyo siku nzuri kwa Rais wa TFF Malinzi kwani Mapacha hawa kuchukua Fomu rasmi

Leo huenda ikawa siyo siku nzuri kwa Rais wa TFF Malinzi kwani Mapacha hawa kuchukua Fomu rasmi

Mkuu hili ni Swali ambalo kiuhakika hata Mimi najiuliza sana kwani hakuna Watu ambao wana Njaa iliyotukuka kama hawa Wajumbe wapiga Kura na kuna Mdau mmoja ambaye yupo karibu na tunayempinga na kumtaka apigwe chini anasema kuwa kwa Hela / Pesa / Fedha aliyoipiga Jamaa anaweza kuwahonga Wajumbe wote Gari mpya aina za IST na akawapa kila mmoja Hela ya Mboga Tsh Milioni Moja Moja.
aseee...itabidi lile faili lake pale Upanga liitwe haraka sana...ila nasikia JM ameungana na Mlamu Mng'ami wa Dodoma ,na anategemea sapoti ya FoS ,ngoja nitarudi kumwaga vitu hapa
 
aseee...itabidi lile faili lake pale Upanga liitwe haraka sana...ila nasikia JM ameungana na Mlamu Mng'ami wa Dodoma ,na anategemea sapoti ya FoS ,ngoja nitarudi kumwaga vitu hapa
Hayo ni maneno tuu hata kwenye khanga yapo. Naona Malinzi anawakosesha sana raha,hamlali wala kula na kunywa vizuri.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Kwa wasiojua mpira unaongozwa na Malinzi as the individual or unaongozwa na kamati ya utendaji as a team ndio watamlaumu Malinzi. Kama walichaguliwa kamati ya utendaji wasiokuwa na meno hayo ndio madhara yake.
 
Nakumbuka uchaguzi wa kwanza uliomuengua Mzee Ndolanga na kumuweka Tenga madarakani! Serikali ikiamua jambo lake na kulisimamia haishindwi kirahisi! Siamini kama serikali itakuwa na Malinzi
Shikamoo mkuu
 
Katika kile kinachoonyesha kwamba Watanzania hasa wapenda Soka / Kandanda wamechoka na Uongozi / Utawala wa sasa wa Rais wa TFF Jamal Malinzi hatimaye leo asubuhi mida ya Saa 5 Viongozi wanaotakiwa kuiongoza TFF wanachukua Fomu rasmi ili kupambana na kumtoa Malinzi madarakani.

Na ili kuonyesha kuwa huenda hawa Watu wawili wakawa ni mwiba mchungu kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi ni kwamba wamepata baraka zote kutoka kwa Wadau wengi wa Soka nchini na hata Serikalini na kuna uwezekano mkubwa mno kwa jinsi mikakati yote ilivyopangwa huu ukawa ndiyo mwisho wa Jamal Malinzi ndani ya TFF.

Watu hao ni Mchezaji na Nahodha wa zamani wa Yanga FC, Mchambuzi mahiri wa Soka, Mdau mkubwa wa Soka na Msomi mzuri wa masuala ya Biashara na Uongozi Ndugu Ally Mayai Tembele ambaye amepangwa kugombea nafasi ya Urais wa TFF na Makamu wake inasemekana amepangwa kuwa ni Mchezaji wa zamani wa Kiungo wa Simba SC na aliyekuwa na mafanikio makubwa, Mdau mkubwa wa masuala ya Soka na Kiongozi wa zamani wa TFF Mzee Mtemi Ramadhan.

Kinachowafanya hawa Watu akina Ally Mayai na Mzee Mtemi Ramadhan wakubalike na Wadau wengi wa Soka / Mpira nchini Tanzania ( GENTAMYCINE inclusive ) ni kwamba kwanza wamecheza mpira katika Kiwango cha juu kabisa hivyo wanajua nini maana ya Soka na Maendeleo yake. Lakini pia hawa Watu wawili ni kweli kuwa mmoja wapo ni mwana Yanga na mwingine ni mwana Simba ila uzuri wao ni kwamba huwa hawana Unafiki na hawatangulizi mapenzi kwa hivyo Vilabu vyao pindi vinapokuwa na matatizo bali wao husimamia Ueledi na Ukweli hasa katika Utendaji wao.

Watoto wa mjini tunasema kwa Kauli mbiu yetu mpya isemayo “ Malinzi pisha njia wenye Mpira wao wamekuja “. Nianze tu kutoa pongezi zangu za dhati kwa hawa Wadau wangu wakubwa wa Soka Kaka yangu Ally Mayai Tembele na Mzee wangu Mtemi Ramadhan kwa kuamua kuwa Viongozi wa TFF na nina uhakika kama Wajumbe wa TFF wataacha Upopoma / Upumbavu wao basi Rais mpya wa TFF atakuwa ni Ndugu Ally Mayai Tembele na Makamu Rais mpya wa TFF ni Ndugu Mtemi Ramadhan.

Nami namalizia kwa kusema “ Malinzi pisha njia wenye mpira wao wamekuja “.

Nawasilisha.
kwenye TFF TUNASEMA BURIAN MALINZI AVEVA AND CO LTD
 
Duuuuh kuna watu inaelekea mnafahamu fitna sana!!!

Nikisema muwe mnanisikiliza na pia muwe makini na niyasemayo. Nashukuru lile nililolisema hatimaye leo limetimia na nimalizie tu kwa kusema kwa Rais wa TFF Jamal Emil Malinzi " Mission has been Accomplished ". Tunamtakia tu kila la kheri kama ni huko rumande Segerea kwa sasa au Gerezani mara baada ya hukumu yake rasmi kutolewa.
 
Mkuu shikamoo maana kwasasa ndio nimekuelewa ulichokuwa unamaanisha. Shikamoo tena

Marahaba na sasa muwe na adabu zote ninapokuwa natahadharisha vitu / mambo hasa yale ' Nyeti ' kabisa humu JF.
 
Frank Wanjiru.. Kiongozi umeingia field nini? Ukitoka field naomba update kuhusu Mr President wa TFF

Ndiyo Yeye aliyeenda kulala jana Segedansi na Jumatatu atakuwepo tena Kisutu ambapo makosa yake hayo 28 yatapunguzwa hadi kubaki 6 au 3 na baada ya hapo atarudishwa tena rumande ' Segadansi ' mpaka baada ya wiki mbili na akirudi tena moja kwa moja kupewa ' Hukumu ' na kuanza maisha yake mapya kati ya Segerea au Keko.
 
Back
Top Bottom