P h a r a o h
JF-Expert Member
- Mar 25, 2024
- 785
- 1,413
Zamani kalenda iliyokua ikitumika ilikua haiendani na mzunguko wa dunia kuizunguka jua, kwa hiyo majira yakawa yanabadilika mfano mwaka huu mvua zinanyesha mwezi wa 7, mwaka ujao zinanyesha mwezi wa 12, na kadhalika. Hii ni kwa sababu kalenda ilikua inapishana na jinsi dunia inavyozunguka jua.
Mwaka 45 KK (kama tunavyoujua kwa sasa), Julius Caesar alipanga kalenda upya ili iendane na mzunguko wa dunia.
Akaweka mfumo wa kuwa na mwaka mrefu wenye siku 366 kila baada ya miaka mitatu yenye siku 365. Akaweza kupata wastani wa mwaka wenye siku 365.25 ambao ukawa unaendana na mzunguko wa dunia kwa kiasi kikubwa.
Hii kalenda inaitwa Kalenda ya Julian.
Karne ya 6, takriban mwaka 525 BK, kulikuwa na mwanafunzi wa dini anayeitwa Dionysius Exiguus ambaye alianzisha mfumo wa kuhesabu miaka kutokana na mwaka aliozaliwa Yesu. Baada ya uchambuzi na mahesabu alizofanya, mwaka aliozaliwa Yesu aliuita 1 BK (Anno Domini), 2 BK, 3 BK, na kadhalika. Mwaka mmoja kabla ya kuzaliwa Yesu aliuita 1 KK (Before Christ), 2 KK, 3 KK, na kadhalika.
Kabla ya hapo, miaka ilihesabiwa kutokana na matukio, utawala, na kadhalika. Kwa Dola ya Kirumi, miaka ilihesabiwa kutokana na kuzaliwa kwa Dola ya Roma.
Mfano mwaka 45 KK ambapo Julius Caesar alirekebisha kalenda ulikua ukijulikana kama mwaka 709.
Kwa hiyo iliendelea kuhesabiwa hivyo hadi takriban mwaka 525 BK ambapo mfumo wa huyo mwanafunzi wa dini ukaanza kusambaa wa kuhesabu kuanzia mwaka aliozaliwa Yesu.
Kalenda ya Julian bado ilikua na makosa kwa kiasi fulani. Mwaka 1582 ikazaliwa kalenda mpya iliyorekebisha makosa kwenye Kalenda ya Julian, inaitwa Kalenda ya Gregorian. Hii kalenda tunayotumia sasa inaitwa Kalenda ya Gregorian ilianzishwa na Papa Gregory XIII mwaka 1582 ili kurekebisha mpangilio uliokuwepo kwenye Kalenda ya Julian.
Kalenda ya Julian ilikuwa na wastani wa siku 365.25, ila kiuhalisia dunia inatumia siku 365.2424 kumaliza mzunguko wake kuzunguka jua. Kwa hiyo kutokana na Kalenda ya Julian, baada ya muda mrefu mzunguko wa dunia unapishana na kalenda.
(kafatilie mabadiliko yaliyofanywa ila siku 10 zikapunguzwa)
Kwa hiyo, kulingana na astronomia ya kisasa, upangaji wa miaka kwa kadiri ya mwanafunzi wa dini Dionysius Exiguus ulikuwa na makosa ya miaka 7 ambayo inaweka huu mwaka kuwa 2024 badala ya 2031.

Kwanini Sasa Sio 2024?
- Mwanafunzi wa dini aliyeanzisha mfumo wa kuhesabu miaka kwa kuzingatia mwaka aliozaliwa Yesu aliupanga mwaka aliozaliwa Kristo kuwa 1 BK. Mwaka kabla ya 1 BK aliuita 1 KK, kwa hiyo hakuna mwaka sifuri, maana yake ni lazima kuna mwaka umerukwa hapo kati.
- Kutokana na teknolojia ya sasa, wanasayansi wa anga (astronomers) wanaweza kuunda tena nafasi ya vitu vya anga: sayari, nyota, na kadhalika kama vilivyoonekana miaka mingi iliyopita. Kutokana na vitabu vya Injili vinavyoelezea kuzaliwa kwa Kristo, Injili ya Mathayo inaongelea kuonekana kwa nyota juu ya anga la Bethlehem ambayo iliwaongoza wanajimu. Kutokana na astronomia, mwaka 1 BK hakukuwa na nyota wala kitu chochote kilichoonekana angani.
- Ila mwaka 7 KK sayari Saturn na Jupiter zilikingiliana mara tatu ndani ya miezi tisa juu ya anga la Bethlehem (planetary conjunction), kitu kinachofanya ikiangaliwa kutoka duniani inaonekana kama nyota inayong'aa sana.
Kwanini 7 KK ni Muhimu Zaidi Licha ya Kuwa Conjunction ni Kawaida Kutokea?
Conjunction ya 2 KK ya Jupiter na Venus iliyoonekana kama nyota inayong'aa sana Bethlehem, haina umuhimu sana kwa sababu ilitokea mara moja mwaka 2 KK na imewahi kujirudia sehemu mbalimbali baada ya miaka fulani. Mfano 66 BK, hata mwaka 2021 pia kulikuwa na conjunction ya Jupiter na Saturn.Umuhimu wa Triple Conjunction ya 7 KK
- Conjunction ya 7 KK imejirudia mara tatu ndani ya mwaka mmoja, Triple Conjunction, na haijawahi kujirudia kutokea hivyo tena (mara tatu ndani ya mwaka mmoja).
- Kutokana na Injili ya Mathayo, nyota iliwaongoza wanajimu watatu kutoka sehemu mbali mbali kwenda Bethlehem (ambazo pia zilikuwa ni mbali sana na Bethlehem). Conjunction ya 2 KK ilionekana mara moja tu hivyo isingeweza kuwaongoza. Conjunction ya 7 KK ya Saturn na Jupiter imeonekana mara 3 ndani ya miezi tisa, kwa hiyo ni likely kuwaongoza wanajimu kutoka sehemu ya mbali.